Pre GE2025 Tuseme bila unafiki: Kikwete ni tatizo kwa sasa nchini kuliko wakati wowote

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna watu wake humu ukimgusa tu yeye na samia utaoga matusi. Wao wanaona kikwete ndo kwao ana akili.
Kama ilivyo kwa nyie haters wake ambao hampati usingizi bila kumtukana jk. Aliyesema jk ana akili za kuzidi wote nani?!!!! Si hatujadili akili hapa, isitoshe nyie na hao watu wenu muwasifiao kutwa kucha mna akili gani?!!!!
 
Wewe ni pi...........mbi?

Ni wapi umesoma jina Jiwe?

Njaa mbaya sana babu! Tafuta pesa acha uvivu na wivu wa kijinga we liccm
 
Raisi pekee aliye kuwa na machungu ni mkapa, japo nae hakuwa perfect ila angalau ali umia.
Mkapa kuwa na uchungu na Tanganyika yangu hapana nakataa kwa sauti. Aliuza NBC, iliyokuwa inafanya kazi kwa faida na kuuza mashirika kadhaa. Nyerere peke yake ndiye Rais aliyekuwa na uchungu na nchi hii, amestaafu na mshahara wa Rais tu, hata watoto wake wote wamesoma Kayumba
 
Kama ilivyo kwa nyie haters wake ambao hampati usingizi bila kumtukana jk. Aliyesema jk ana akili za kuzidi wote nani?!!!! Si hatujadili akili hapa, isitoshe nyie na hao watu wenu muwasifiao kutwa kucha mna akili gani?!!!!
Tayari ugomvi umeanza
 
Rais wangu bora wa muda wote wa Tanzania.
Mwacheni ampumzike. Kila unachokiona leo hii ni matokeo ya mpango mikakati ya utekelezaji ya Mzee Kikwete. Hakuwa Rais wa kukurupuka na kuamua cha kufanya bali Kila kitu kilipangwa na kutafiwa njia ya kukamilishwa katika mpango maalum.

ChaDema pambaneni na hali zenu! Sioni hoja ya msingi hapa.
 
Dhana ya ufisadi ishapitwa na wakati. Haipo kwa Sasa kwa sababu Kila mtu anajua mignon ya uwajibikaji kitaasisi ilivyo migumu.
 
Nyerere huyo aliye tapeliwa na muhindi aliye kimbilia uingereza?
 
Mimi naona nikiandika haitoshi nimerekodi voice note👇 sikiliza kwa umakini
Ibonyeze mara mbili kuisikiliza.
Utakayoyasikia yanahuzunisha sana Kuhusu huyu mwamba ila hakikisha una wakili msomi.
🗣️▶︎•|၊|။||||။၊|။|||။03:53
 
Hata US kuna system ndio inaendesha nchi huwezi cheza nao otherwise hukai kileleni,that stuff is everywhere
 
Ktk tawala 5 zilizopita ni utawala upi ulioweka rekodi kwa kuwa na skedo kubwa kubwa za ufisadi?
 
Aisee! Ww ni kiboko! Halafu ww ni mkweli sana!
 
Kongole Mkuu kwa kuona hili. Mimi mwenyewe nimepata fursa ya kusoma na ajira kipindi Cha Jakaya. Nikiangalia vijana wengi wahitimu baada ya yeye kuondoka madarakani waliopo mitaani wanauza matunda au machinga nasikitika sana! Mabinti wapo wanajiuza!

Siku za nyuma elimu ilikuwa sehemu chache hususani Kagera na Kilimanjaro na hii ni kutokana na mfumo wa kikoloni. Siku hizi digrii zipo kila Kijiji Cha Tanzania. Alirahisisha upatikanaji wa elimu kwa kiwango kikubwa sana!
 
Yeye ndiye dalali mkuu na ndugu yake rostam na kinana.na vijana wake makamba Bashe ridhiwan
Jiwe ndiye alimrudisha Rostam baada ya JK kumuondoa yeye na rafiki yake Lowasa kwenye system. Ni kweli walimsaidia JK kuingia madarakani lakini baadae aliwajua ni tatizo kwa nchi. Akwaondoa kiaina. Rostam alitoroka nchi.
 
wote mnaomkandia JK hamjielewi, huyo mwamba alipaswa kuongoza Tz mpaka umauti wake
Kwani dereva mwenye leseni ya gari Tanzania kwa Sasa ni nani? Kwa Nini alaumiwe dereva aliyestaafu na yupo nyumbani kwake akifanya kazi tofauti na udereva? Tuache kugeuza uji kuwa mboga ya ugali.
Pole sana mtoa hoja.
 
Naambiwa pale kwenye deathbed alikuwepo mtu akatoka pembeni mara moja akaenda kuwapigia simu CIA halafu akarudi tena pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…