1. Utawala bora kulenga zaidi watu kupata uongozi kwa sababu ya uwezo wao na pia usimamizi makini wa rasilimali za umma (hati chafu chafu za CAG kuzipunguza zaidi ya 70%), kufuta matumizi ya umma yasiyo na msingi
2. Ningefanya Internet kuwa ya gharama nafuu sana na kupatikana kwa urahisi popote mtu alipo nchini sababu kuna shughuli nyingi tu za kiuchumi zinachochewa na Internet
3. Ningefanya huduma ya umeme kuwa nafuu na ya uhakika sababu uzalishaji mwingi unategemea umeme
4. Ningeondoa vikwazo kwa huduma za malipo za online na kujiimarisha mimi tu kama serikali kucontrol money laundering, kwa mfano nchi kama hii kukosa PayPal au kushindwa kumonetize media kama tiktok ni ukiritimba usio na msingi
5. Ningeongeza kiwango cha wanaotuma hela nchini kutoka nje ya TZ na kupunguza vikwazo vya kijinga hela ya kutoka nje inapotaka kutolewa
6. Ningeweka nguvu ya ziada kwenye kilimo kuwa cha kisiasa na kutengeza opportunity za kuwafaidisha wakulima na wafanyabiashara kwa level zao
7. Ningepunguza kiwango cha kodi, kodi kuwa mara mbili au zaidi ya bidhaa unapoingiza ndani ya nchi ni ujinga wa hali ya juu na haufadishi wananchi zaidi zaidi watu wanakua masikini tu
8. Ningeruhusu uagizwaji wa kutoka nje wa sukari na cement
9. Ningekomesha utumiaji wa watu wa sekta ya burudani kwenye shughuli za kisiasa (kuna tofauti ya shughuli za kiserikali na kisiasa) timu za mpira, waigizaji, wanamuziki, comedians..... etc
10. Ningefuta KKK kuwa kigezo cha ubunge... bali ningeweka kigezo cha elimu na kigezo cha mali anazotakiwa kuwa nazo mgombea