Ooooh ohhh mtoa maada naona umejawa na hofu Sana hasa ya Nini kitatokea endapo CDM hawatashiriki uchaguzi,,,,,,,,,
Pili huoni athari yeyote kwa nchi hasa vijana Hawa watakao kuja kuwa taifa la Tanzania siku zijazo..
Historia mbona inafundisha mengi Sana.....mfano ;chanzo cha mapinduzi ya Zanzibar,mapinduzi ya Cuba, huko Haiti nk. Watawala walipuuza madai madogo kama haya wakaona hayana msingi kwa sababu wao wanashiba hawajui wenzao wapo VP na mawazo Gani
Hivi karibuni nchi ya Siri Lanka maandano yalianzishwa na watoto wa shule mwishowe serikali yote ikaangushwa km masihara vile,,,,
Kumbuka wakati mwl Nyerere anadai uhuru wa Tanganyika Kuna wa Tanganyika waliokuwa wanakula mezani pa mkoloni walimpinga na kumuona zuzu...Hali kdhalika na huko A.kusini, Mozambique,Namibia,Kenya Ghana nk.
Duniani kote duku duku la kudai haki,kuondoa ukandamizaji,kujikomboa kiuchumi ,kifikra na kupata usawa si kazi ndogo na Huwa inaanza na wanyonge Wachache wenye kuthubutu kutetea wenzao.........
Hawa wanyonge wenye kutetea wanyonge ndio Huwa wapo hatarini Sana......kuuwawa,kufungwa,kutekwa,kufirisiwa,kupigwa,kunyongwa,kutishwa,kuny'ang'anywa uraia na maswahibu mengine.
Kusudi waache kudai haki,waendelee kutawaliwa na kula Emma yote ya nchi.....
Pia Kila nchi duniani kwa Sasa inapigana kivyake hakuna familia ya jirani au hata ndugu atamwanglia mwenzake.........hao wa ulaya au china ama Amerika wataangalia kwetu kwa kulinda TU Mali zao walizoweka hapa kwetu na kumuunga mkono yule(upande) utakao onyesha utalinda maslahi Yao
Nitarudi baadae.........