Tuseme ukweli, Gamondi anafeli pakubwa sana Yanga

Changamoto hapa ni mnadhani uto yuko confederations na kina marumo gallants... hii ni champions league. Hata nabi angestruggle...
 
Viungo wanacreate nafasi nyingi sana. Tatizo ni finishing. Hatuna straika.
 
Nabi Nabii huyu alitolewa club bingwa mapema hakuweza kuingia makundi na yanga ,msimu huu akiwa na FAR Rabat bingwa wa Morocco ambaye anaongoza ligi mpaka Sasa Katolewa round ya pili club bingwa na team inayofungwa 2+nyumbani na Al hilal ya ibenge,what so special Abt Nabi ,Hii ni club bingwa Africa mashindano makubwa ya vilabu Africa ,ambayo mamelod anayesifiwa Kila msimu anakombe mmoja na kaingia fainali mara moja.Pokea hii ikufungue akili Nabi sio Elite coach ni wakawaida sana.
 
Maneno yamekuwa mengi Gamond, Gamond hana mbinu ni kutokana na sababu tu ya timu kushindwa kupata magoli. Binafsi mimi sioni tatizo la kocha bali timu haina ma straika wamaana. Yaani Mzize, Konikon na Musonda ndio wakupe matokeo? Kuna clear chances mbili za counter Kibabage anatetemeka tu anashindwa kufanya maamuzi sahihi. Mzize nae kapata clear chance moja kashindwa kuitumia. Na kuna mipira miwili ya counter kashindwa kutulia kutoa pasi ya kupenyeza kwa mwenzie. Zile nafasi zingetumiwa vyema kungekuwa na maneno kuhusu kocha? Mbinu huendana na silaha, kama silaha zako hafifu na butu uta struggle sana kumshinda adui. Tokea mechi ya ngao ya jamii nilisema madhaifu ya timu ni umaliziaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…