Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.
Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla hatujarejea katika mfumo huo wa kiushindani.
Miaka yote hii tokea 1995, zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu limekuwa ni zoezi la kutimiza wajibu tu, ili nasi tuonekane tuna demokrasia ya kuchagua viongozi wetu ilhali uwanja wa ushindani haupo sawa baina ya washiriki wa mpambano.
Walio wahalisia wa mambo kama mimi, tayari ‘tunajua’ ni mgombea yupi kwenye ngazi ya urais atayetangazwa mshindi.
Mgombea huyo atayetangazwa kuwa ndo mshindi, ndo mtu huyo huyo aliyewateua kwenye hizo nafasi zao kwenye tume ya uchaguzi hao wataomtangaza yeye kuwa ndo mshindi.
Sasa nikiona jinsi ambavyo wanachama wa vyama vilivyo nje dola walivyo na hamu na hamasa ya uchaguzi mkuu, nashindwa kuelewa.
Nashindwa kuelewa kama ni wamejitoa tu fahamu kwa muda na kwamba kabla ya uchaguzi akili zitawarudia au wamejitoa kabisa fahamu na kusahau kabisa jinsi vile uwanja wa mapambano haupo sawa!
Kwa sababu, nikionacho hapa ni kwamba, baada ya tarehe 28 Oktoba, tutarudi kule kule tulikokuwa 2005, 2010, na 2015.
Baada ya ‘kushindwa’ watu ndo watagutuka tena kuwa kumbe tunahitaji katiba mpya. Kumbe tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Kumbe tunahitaji uwanja ulio sawa kwa washiriki wote.
Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.
Sasa sijui kama kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua una vikwazo vingi ni jambo la busara au la. Ingekuwa uamuzi ni wangu mimi binafsi, nisingeshiriki mchakato ambao ni wa maigizo.
Wengine wanaweza kuwa na mtazamo ulio tofauti. Hakuna ubaya kwenye hilo.
Ila kwa kadri mtu unapozidi kushiriki mchakato wa jambo ambalo unajua kabisa halitoi fursa sawa kwa wote, unapokosa kupata fursa uitakayo, unakuwa umejipunguzia mamlaka ya kimaadili ya kupinga na kulalamikia matokeo.
Manake kama ulikuwa unajua kabla ya zoezi kuanza kuwa hakuna fursa sawa, kwa nini sasa ulishiriki? Si ungeligomea zoezi zima tu!
Kwa sasa endeleeni kufurahia maneno matamu ya Lissu. Sasa hivi anawapa nyie wapenzi na mashabiki wake kile kiitwacho ‘red meat’, yaani yale maneno mnayotaka kusikia na yanayoziamsha hisia zenu.
Naona na Bw. Membe naye anajitutumua kuwarushia mashabiki wake hizo nyama nyekundu lakini hamfikii Lissu.
Baada ya uchaguzi kuisha na Rais Magufuli kutangazwa mshindi, akili, kama mnazo, labda ndo zitawarudia na kutambua kuwa hamkuwa na lenu kwenye huo uchaguzi!
Kama mnabisha, siku ya siku ikifika tutakumbushana haya maneno yangu. Msije kununa tu.😁