Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Wewe ndiyo kabisa kichefu chefu
Defeatist attitude yako inatia simanzi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Defeatist attitude yako inatia simanzi.
Sasa jambo la msingi likikataliwa na wajinga wengi utaliacha ili uwaridhishe au utawapa wale werevu wachache halafu wale wajinga siku wakiamka akili zao ndio waone walivyopotoka?Mbona inasemwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania walikataa mfumo wa vyama vingi lakini Nyerere ndo akaupigia debe...uongo?
Uwepo wa jengo mahali hauwezi kuwa ndio kipimo pekee cha uwepo/ kukubalika kwa chama cha siasa.Mimi hata siwaelewagi .... wanashangilia vijembe utafikiri vinageuka kura. Kwanza kwa hali iliyopo mwaka huu hata kama uchaguzi utasimamiwa na mabeberu CCM itashinda! Huko mitaani/vijijini Chadema imefutika, matawi yamefungwa mengi sana. Kabla hata ya issue za Katiba na tume chama hakina mizizi ya watu ngazi za chini kama CCM.
Lisu Ni kama bua tu
Watu wana Mcheki anavyo wachezesha watoto Wa Ufipa
Hahaha
Hizo ni Ndoto za Vilaza
Mwenye Akili Anajua Magufuli hana Mshindani hapo
Yaani daahhNchi ya kihuni sana hii
Hata 2010 walikataa wizi wa kura.
2015 napo walikataa wizi wa kura na wakatishia kwenda sijui kwenye mahakama ya wapi wapi huko.
Hawakwenda. Yalikuwa ni maneno matupu tu.
2020 hao tena....wanashiriki tena chaguzi kwa sheria zile zile, tume ile ile, wakishindana na CCM ile ile.
Kila la kheri.
Listern mimi siipendi. Ccm yaani ccm na matope niko radhi niyachague matope yatawaleManeno meeeengi ilhali hoja yako ni kumpigia debe M-kanda ya Ziwa mwenzako. Kama wapinzani wanapoteza muda, why do you even care? Kama Magufuli unayempenda atashinda bila tatizo hapo Oktoba, why should you bother how Wapinzani watavyojiskia baada ya ushindi huo? [emoji35]
Tumelelewa katika mazingira hayo ya kujengewa hofu tangu ccm ilipo anza kutawalaKwa nini? Sisi ni waoga wa kupigwa virungu?
Wakati unamshangilia Padre Slaa akili zako zilifungiwa kabatini?Mimi hata siwaelewagi .... wanashangilia vijembe utafikiri vinageuka kura. Kwanza kwa hali iliyopo mwaka huu hata kama uchaguzi utasimamiwa na mabeberu CCM itashinda! Huko mitaani/vijijini Chadema imefutika, matawi yamefungwa mengi sana. Kabla hata ya issue za Katiba na tume chama hakina mizizi ya watu ngazi za chini kama CCM.
Nyani , kati siku akili zako zilipikurudia ni pamoja na post hii. Lakini nakuona kama msomi asiyependa nchi yake. Kasoro za ki muundo unaziona halafu lawama unawarushia wapinzani !!. Hii akili ya msomi wa aina gani ?!.Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.
Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla hatujarejea katika mfumo huo wa kiushindani.
Miaka yote hii tokea 1995, zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu limekuwa ni zoezi la kutimiza wajibu tu, ili nasi tuonekane tuna demokrasia ya kuchagua viongozi wetu ilhali uwanja wa ushindani haupo sawa baina ya washiriki wa mpambano.
Walio wahalisia wa mambo kama mimi, tayari ‘tunajua’ ni mgombea yupi kwenye ngazi ya urais atayetangazwa mshindi.
Mgombea huyo atayetangazwa kuwa ndo mshindi, ndo mtu huyo huyo aliyewateua kwenye hizo nafasi zao kwenye tume ya uchaguzi hao wataomtangaza yeye kuwa ndo mshindi.
Sasa nikiona jinsi ambavyo wanachama wa vyama vilivyo nje dola walivyo na hamu na hamasa ya uchaguzi mkuu, nashindwa kuelewa.
Nashindwa kuelewa kama ni wamejitoa tu fahamu kwa muda na kwamba kabla ya uchaguzi akili zitawarudia au wamejitoa kabisa fahamu na kusahau kabisa jinsi vile uwanja wa mapambano haupo sawa!
Kwa sababu, nikionacho hapa ni kwamba, baada ya tarehe 28 Oktoba, tutarudi kule kule tulikokuwa 2005, 2010, na 2015.
Baada ya ‘kushindwa’ watu ndo watagutuka tena kuwa kumbe tunahitaji katiba mpya. Kumbe tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Kumbe tunahitaji uwanja ulio sawa kwa washiriki wote.
Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.
Sasa sijui kama kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua una vikwazo vingi ni jambo la busara au la. Ingekuwa uamuzi ni wangu mimi binafsi, nisingeshiriki mchakato ambao ni wa maigizo.
Wengine wanaweza kuwa na mtazamo ulio tofauti. Hakuna ubaya kwenye hilo.
Ila kwa kadri mtu unapozidi kushiriki mchakato wa jambo ambalo unajua kabisa halitoi fursa sawa kwa wote, unapokosa kupata fursa uitakayo, unakuwa umejipunguzia mamlaka ya kimaadili ya kupinga na kulalamikia matokeo.
Manake kama ulikuwa unajua kabla ya zoezi kuanza kuwa hakuna fursa sawa, kwa nini sasa ulishiriki? Si ungeligomea zoezi zima tu!
Kwa sasa endeleeni kufurahia maneno matamu ya Lissu. Sasa hivi anawapa nyie wapenzi na mashabiki wake kile kiitwacho ‘red meat’, yaani yale maneno mnayotaka kusikia na yanayoziamsha hisia zenu.
Naona na Bw. Membe naye anajitutumua kuwarushia mashabiki wake hizo nyama nyekundu lakini hamfikii Lissu.
Baada ya uchaguzi kuisha na Rais Magufuli kutangazwa mshindi, akili, kama mnazo, labda ndo zitawarudia na kutambua kuwa hamkuwa na lenu kwenye huo uchaguzi!
Kama mnabisha, siku ya siku ikifika nitawakumbusha haya maneno yangu. Msije kununa tu...[emoji16]
Hili ndilo tatizo la Watanganyika, unajuwa ni kwa Nini nchi jirani ya Zanzibar mpaka Cuf ya Maalim walitowa makamishina kuunda tume ya uchaguzi Zec?Nyani , kati siku akili zako zilipikurudia ni pamoja na post hii. Lakini nakuona kama msomi asiyependa nchi yake. Kasoro za ki muundo unaziona halafu lawama unawarushia wapinzani !!. Hii akili ya msomi wa aina gani ?!.
Kwamba wewe mamlaka zilizotakiwa kutoa haki kwa wananchi kujichagulia viongozi wao ni wapinzani ?!. Usomi huu mbona bure kabisa Ngabu ?!.
Nchi hii ni yetu sote. Tujiwekee utaratibu mzuri wa watu kuwaweka viongozi bora na wanaowataka. Si hii ya lazima utokane na chama cha ki communist cha Ccm !!. Usomi wako usaidie badala ya kuwazodoa wapinzani wanaopambana kupata haki hiyo [emoji120][emoji120]
Hivi Unamiaka 23Hana mshindani ndiyo mgechpisha fom moja tu kama tochi ya muwindaji?
Sijui ccm mnafurahia nini mazingira mabovu ya uchaguzi na hayo hayo ndio yatawaangusha.Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.
Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla hatujarejea katika mfumo huo wa kiushindani.
Miaka yote hii tokea 1995, zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu limekuwa ni zoezi la kutimiza wajibu tu, ili nasi tuonekane tuna demokrasia ya kuchagua viongozi wetu ilhali uwanja wa ushindani haupo sawa baina ya washiriki wa mpambano.
Walio wahalisia wa mambo kama mimi, tayari ‘tunajua’ ni mgombea yupi kwenye ngazi ya urais atayetangazwa mshindi.
Mgombea huyo atayetangazwa kuwa ndo mshindi, ndo mtu huyo huyo aliyewateua kwenye hizo nafasi zao kwenye tume ya uchaguzi hao wataomtangaza yeye kuwa ndo mshindi.
Sasa nikiona jinsi ambavyo wanachama wa vyama vilivyo nje dola walivyo na hamu na hamasa ya uchaguzi mkuu, nashindwa kuelewa.
Nashindwa kuelewa kama ni wamejitoa tu fahamu kwa muda na kwamba kabla ya uchaguzi akili zitawarudia au wamejitoa kabisa fahamu na kusahau kabisa jinsi vile uwanja wa mapambano haupo sawa!
Kwa sababu, nikionacho hapa ni kwamba, baada ya tarehe 28 Oktoba, tutarudi kule kule tulikokuwa 2005, 2010, na 2015.
Baada ya ‘kushindwa’ watu ndo watagutuka tena kuwa kumbe tunahitaji katiba mpya. Kumbe tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Kumbe tunahitaji uwanja ulio sawa kwa washiriki wote.
Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.
Sasa sijui kama kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua una vikwazo vingi ni jambo la busara au la. Ingekuwa uamuzi ni wangu mimi binafsi, nisingeshiriki mchakato ambao ni wa maigizo.
Wengine wanaweza kuwa na mtazamo ulio tofauti. Hakuna ubaya kwenye hilo.
Ila kwa kadri mtu unapozidi kushiriki mchakato wa jambo ambalo unajua kabisa halitoi fursa sawa kwa wote, unapokosa kupata fursa uitakayo, unakuwa umejipunguzia mamlaka ya kimaadili ya kupinga na kulalamikia matokeo.
Manake kama ulikuwa unajua kabla ya zoezi kuanza kuwa hakuna fursa sawa, kwa nini sasa ulishiriki? Si ungeligomea zoezi zima tu!
Kwa sasa endeleeni kufurahia maneno matamu ya Lissu. Sasa hivi anawapa nyie wapenzi na mashabiki wake kile kiitwacho ‘red meat’, yaani yale maneno mnayotaka kusikia na yanayoziamsha hisia zenu.
Naona na Bw. Membe naye anajitutumua kuwarushia mashabiki wake hizo nyama nyekundu lakini hamfikii Lissu.
Baada ya uchaguzi kuisha na Rais Magufuli kutangazwa mshindi, akili, kama mnazo, labda ndo zitawarudia na kutambua kuwa hamkuwa na lenu kwenye huo uchaguzi!
Kama mnabisha, siku ya siku ikifika nitawakumbusha haya maneno yangu. Msije kununa tu.😁