Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uliugua utapiamlo au kifaduro wakati wa utoto!Kuwa na kipara bila akili ni sawa na kuwa na mswaki bila kuwa na meno mdomoni.
Si unajua kiitikio chenu cha tumeibiwa×6Jiandaeni kisaikolojia maana lissu ndiye ataapishwa baada ya October.
Wananchi wa Tanzania tegemeo lao ni mh Lissu.
Hutaki rudi kwenu Burundi.
Nimependa Sana ulivyomuelezea huyu jamaa,inaonesha Ana uelewa mdogo Sana wa mamboNyani , kati siku akili zako zilipikurudia ni pamoja na post hii. Lakini nakuona kama msomi asiyependa nchi yake. Kasoro za ki muundo unaziona halafu lawama unawarushia wapinzani !!. Hii akili ya msomi wa aina gani ?!.
Kwamba wewe mamlaka zilizotakiwa kutoa haki kwa wananchi kujichagulia viongozi wao ni wapinzani ?!. Usomi huu mbona bure kabisa Ngabu ?!.
Nchi hii ni yetu sote. Tujiwekee utaratibu mzuri wa watu kuwaweka viongozi bora na wanaowataka. Si hii ya lazima utokane na chama cha ki communist cha Ccm !!. Usomi wako usaidie badala ya kuwazodoa wapinzani wanaopambana kupata haki hiyo [emoji120][emoji120]
mkuu nyani, nakuomba uondoe aya ya mwisho kabisa maana hakuna timamu anayeweza kubishana na wewe katika haya uliyoandika!Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.
Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla hatujarejea katika mfumo huo wa kiushindani.
Miaka yote hii tokea 1995, zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu limekuwa ni zoezi la kutimiza wajibu tu, ili nasi tuonekane tuna demokrasia ya kuchagua viongozi wetu ilhali uwanja wa ushindani haupo sawa baina ya washiriki wa mpambano.
Walio wahalisia wa mambo kama mimi, tayari ‘tunajua’ ni mgombea yupi kwenye ngazi ya urais atayetangazwa mshindi.
Mgombea huyo atayetangazwa kuwa ndo mshindi, ndo mtu huyo huyo aliyewateua kwenye hizo nafasi zao kwenye tume ya uchaguzi hao wataomtangaza yeye kuwa ndo mshindi.
Sasa nikiona jinsi ambavyo wanachama wa vyama vilivyo nje dola walivyo na hamu na hamasa ya uchaguzi mkuu, nashindwa kuelewa.
Nashindwa kuelewa kama ni wamejitoa tu fahamu kwa muda na kwamba kabla ya uchaguzi akili zitawarudia au wamejitoa kabisa fahamu na kusahau kabisa jinsi vile uwanja wa mapambano haupo sawa!
Kwa sababu, nikionacho hapa ni kwamba, baada ya tarehe 28 Oktoba, tutarudi kule kule tulikokuwa 2005, 2010, na 2015.
Baada ya ‘kushindwa’ watu ndo watagutuka tena kuwa kumbe tunahitaji katiba mpya. Kumbe tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Kumbe tunahitaji uwanja ulio sawa kwa washiriki wote.
Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.
Sasa sijui kama kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua una vikwazo vingi ni jambo la busara au la. Ingekuwa uamuzi ni wangu mimi binafsi, nisingeshiriki mchakato ambao ni wa maigizo.
Wengine wanaweza kuwa na mtazamo ulio tofauti. Hakuna ubaya kwenye hilo.
Ila kwa kadri mtu unapozidi kushiriki mchakato wa jambo ambalo unajua kabisa halitoi fursa sawa kwa wote, unapokosa kupata fursa uitakayo, unakuwa umejipunguzia mamlaka ya kimaadili ya kupinga na kulalamikia matokeo.
Manake kama ulikuwa unajua kabla ya zoezi kuanza kuwa hakuna fursa sawa, kwa nini sasa ulishiriki? Si ungeligomea zoezi zima tu!
Kwa sasa endeleeni kufurahia maneno matamu ya Lissu. Sasa hivi anawapa nyie wapenzi na mashabiki wake kile kiitwacho ‘red meat’, yaani yale maneno mnayotaka kusikia na yanayoziamsha hisia zenu.
Naona na Bw. Membe naye anajitutumua kuwarushia mashabiki wake hizo nyama nyekundu lakini hamfikii Lissu.
Baada ya uchaguzi kuisha na Rais Magufuli kutangazwa mshindi, akili, kama mnazo, labda ndo zitawarudia na kutambua kuwa hamkuwa na lenu kwenye huo uchaguzi!
Kama mnabisha, siku ya siku ikifika nitawakumbusha haya maneno yangu. Msije kununa tu.[emoji16]
Kwa ujumla WaTz ni wanafki. Na Nyani Ngabu anauwakilisha unafki huo. Kasoro anaziona kwenye katiba na tume , halafu pa kurushia taka ni kwa wapinzani !!! Ajabu na kweliNimependa Sana ulivyomuelezea huyu jamaa,inaonesha Ana uelewa mdogo Sana wa mambo
Asante Sana kiongozi.
Una hekima kubwa Sana.
Hizo dharau sasa! Hata Albashir alikuwa na dharau za aina hiyo na sasa ananyea ndooMagufuli lazima ashinde
Hasiposhinda tutampa ushindi wa lazima halafu tunabadili katiba awe rais wa kudumu
Si unajua kiitikio chenu cha tumeibiwa×6
Nakuona unavyorusha ngumi hewani kudadadeeekiUliugua utapiamlo au kifaduro wakati wa utoto!
Napenyezewa na watu wa karibu kuwa siku ya msiba yule mtu wa burundi ulimsihi sana akuache usirudishwe kwenu!Mwaka huu lazima mtarudi kwenu Burundi
Ndio kwanza chuma kinatafuna mahindi dumila kuonyesha yupo fiti mpaka meno!Nakuona unavyorusha ngumi hewani kudadadeeeki
Ndio kwanza chuma kinatafuna mahindi dumila kuonyesha yupo fiti mpaka meno!
Mwambie yule wenu asimame kwa mguu mmoja kuongoza ni ufiti wa mwili na akiliKwahiyo meno ndiyo yanaongoza?
Napenyezewa na watu wa karibu kuwa siku ya msiba yule mtu wa burundi ulimsihi sana akuache usirudishwe kwenu!
Mwambie yule wenu asimame kwa mguu mmoja kuongoza ni ufiti wa mwili na akili
Ndio kosa kubwa kuwaza kumiliki treni wakati hata mkokoteni wa punda huna!Akili kubwa pale jiandaeni kuwa wapinzani wa kudumu na wenzenu kina Lyatonga na Lipumba
Mbona hukanushi!Naona unataka kujificha kwenye kivuli cha kinu cha nyuklia