Uchaguzi 2020 Tusemezane: Uhalisia wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020

Dogo wakati mwingine unaongea point sana, CDM na ACT walifanya makosa makubwa sana kuingia kwenye uchaguzi huu pasipo kwanza kupatikana TUME HURU YA UCHAGUZI. Walipaswa kujifunza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mark my words: 2025 mambo yatakuwa hivi hivi kama yalivyo sasa!
 
Kabisa Mkuu, kushiriki chaguzi katika mazingira ya namna hii DHARAU KWA WANANCHI na kutupotezea muda wetu tu.
Mimi kamwe sitopiga kura yangu katika mazingira kama haya ya sasa.
 
Naona kidogo makamanda wanaelewa sasa. Labda sasa matusi kwetu yatapungua tujenge upya upinzani. Mlipaswa kujifunza kwa njia ngumu
 
Hahahaa.

Wachache wameanza kuelewa.

Ila kuna wengine bado aisee.

Wana vichwa vigumu sana.
 
Dogo wakati mwingine unaongea point sana, CDM na ACT walifanya makosa makubwa sana kuingia kwenye uchaguzi huu pasipo kwanza kupatikana TUME HURU YA UCHAGUZI. Walipaswa kujifunza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Hawa vingozi wa upnzani huwa wanata mashaka sana kama kweli wana nia ya dhati ya kutaka kuiondoa ccm.
 
Mimi ni mmoja wa watu ambao wanaamini kwamba kama taifa, tulipaswa kuingia katika mfumo wa vyama vingi na katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi.

Sitazungumzia mambo ya kiufundi na ya kimuundo kuhusu hivyo vitu viwili. Lakini kimsingi, hivyo vitu ndo vilipaswa kufanyika kwanza kabla hatujarejea katika mfumo huo wa kiushindani.

Miaka yote hii tokea 1995, zoezi zima la kupiga kura katika uchaguzi mkuu limekuwa ni zoezi la kutimiza wajibu tu, ili nasi tuonekane tuna demokrasia ya kuchagua viongozi wetu ilhali uwanja wa ushindani haupo sawa baina ya washiriki wa mpambano.

Walio wahalisia wa mambo kama mimi, tayari ‘tunajua’ ni mgombea yupi kwenye ngazi ya urais atayetangazwa mshindi.

Mgombea huyo atayetangazwa kuwa ndo mshindi, ndo mtu huyo huyo aliyewateua kwenye hizo nafasi zao kwenye tume ya uchaguzi hao wataomtangaza yeye kuwa ndo mshindi.

Sasa nikiona jinsi ambavyo wanachama wa vyama vilivyo nje dola walivyo na hamu na hamasa ya uchaguzi mkuu, nashindwa kuelewa.

Nashindwa kuelewa kama ni wamejitoa tu fahamu kwa muda na kwamba kabla ya uchaguzi akili zitawarudia au wamejitoa kabisa fahamu na kusahau kabisa jinsi vile uwanja wa mapambano haupo sawa!

Kwa sababu, nikionacho hapa ni kwamba, baada ya tarehe 28 Oktoba, tutarudi kule kule tulikokuwa 2005, 2010, na 2015.

Baada ya ‘kushindwa’ watu ndo watagutuka tena kuwa kumbe tunahitaji katiba mpya. Kumbe tunahitaji tume huru ya uchaguzi. Kumbe tunahitaji uwanja ulio sawa kwa washiriki wote.

Siyo mmoja wa washiriki ndo anakuwa mchezaji yeye, refa yeye, kamisaa yeye, mwajiri yeye, na kila kitu kingine kihusianacho na uchaguzi anaoshiriki, yeye.

Sasa sijui kama kushiriki chaguzi ambazo mtu unajua una vikwazo vingi ni jambo la busara au la. Ingekuwa uamuzi ni wangu mimi binafsi, nisingeshiriki mchakato ambao ni wa maigizo.

Wengine wanaweza kuwa na mtazamo ulio tofauti. Hakuna ubaya kwenye hilo.

Ila kwa kadri mtu unapozidi kushiriki mchakato wa jambo ambalo unajua kabisa halitoi fursa sawa kwa wote, unapokosa kupata fursa uitakayo, unakuwa umejipunguzia mamlaka ya kimaadili ya kupinga na kulalamikia matokeo.

Manake kama ulikuwa unajua kabla ya zoezi kuanza kuwa hakuna fursa sawa, kwa nini sasa ulishiriki? Si ungeligomea zoezi zima tu!

Kwa sasa endeleeni kufurahia maneno matamu ya Lissu. Sasa hivi anawapa nyie wapenzi na mashabiki wake kile kiitwacho ‘red meat’, yaani yale maneno mnayotaka kusikia na yanayoziamsha hisia zenu.

Naona na Bw. Membe naye anajitutumua kuwarushia mashabiki wake hizo nyama nyekundu lakini hamfikii Lissu.

Baada ya uchaguzi kuisha na Rais Magufuli kutangazwa mshindi, akili, kama mnazo, labda ndo zitawarudia na kutambua kuwa hamkuwa na lenu kwenye huo uchaguzi!

Kama mnabisha, siku ya siku ikifika tutakumbushana haya maneno yangu. Msije kununa tu.😁
Hivi huo unazi wenu unawatoa kabisa utu? Yaani katika ubinadamu wako hujaguswa kabisa na uhuni mkubwa uliofanyika jana na leo katika hicho unachoita uchaguzi, sijui ushindi, na upuuzi kama huo?

Sasa ni hivi, ndio mshindi atatangaza lakini dunia imeshuhudia uhuni wa kihistoria uliofanywa na dikteta ambaye licha ya kudhibiti upinzani kwa miaka mitano mfululizo bado amelazimika kutumia hujuma kupata ushindi.

Naomba uhifadhi sehemu maneno haya: kama mnadhani huyo Ngosha mwenzenu ametoboa kirahisi kama alivyoweza kuficha mauaji ya MKIRU na ya korona, kuna mshangao unawasubiri.

Lakini msivyo na aibu mtakuja tena hapa kusema dah lakini Lissu...mliyehindwa kumuua kwa risasi 40 hamuwezi kummaliza kwa sanduku la kura.

Feel free to mark these words.
 
Mbona unanishambulia?

Umesoma na kuelewa kweli nilichokiandika au umetumia tu hisia kunijibu?
 
Kasome zenji ni matunda gani yamepatikana kwa wapinzani kugomea uchaguzi.
Si zamani sana waligoma, na badala yake hal ndio imekuwa ngumu zaidi, watu wamebadilisha sheria n.k

Hakuna kugoma ni kushiriki ili kila mtu aone mapungufu yaliopo.
 
Ahahahaaaaaa

Uncle JuJu anawakumbusha tu.

Karibuni chai ya mchaichai ☕️
 
Hii kata funua ya CCM ni zaidi ya umafia. Wengine tuliwaonya humu mkaishia kututukana.

Maswali ya kujiuliza, ni kwa nini turn up ni ndogo this time. Maana ingekuwa hoja ya kuongeza kura, tungeshuhudia idadi ya wapiga kura ikiwa kubwa.

Ukiyaangalia matokeo haya yanaakisi kabisa zile nyomi za mikutano ya Lissu kwa numbers
 
Hivi huo unazi wenu unawatoa kabisa utu? Yaani katika ubinadamu wako hujaguswa kabisa na uhuni mkubwa uliofanyika jana na leo katika hicho unachoita uchaguzi, sijui ushindi, na upuuzi kama huo?

Sasa ni hivi, ndio mshindi atatangaza lakini dunia imeshuhudia uhuni wa kihistoria uliofanywa na dikteta ambaye licha ya kudhibiti upinzani kwa miaka mitano mfululizo bado amelazimika kutumia hujuma kupata ushindi.

Naomba uhifadhi sehemu maneno haya: kama mnadhani huyo Ngosha mwenzenu ametoboa kirahisi kama alivyoweza kuficha mauaji ya MKIRU na ya korona, kuna mshangao unawasubiri.

Lakini msivyo na aibu mtakuja tena hapa kusema dah lakini Lissu...mliyehindwa kumuua kwa risasi 40 hamuwezi kummaliza kwa sanduku la kura.

Feel free to mark these words.
Mkuu sidhani Kama utakuwa umemuelewa mtoa mada vizuri.
 
Je nchi zingine pia huwa zinafunga mitando ya kijamii wakati wa chaguzi?

Je ufungaji wa mitandoa utakuwa ni jambo la kudumu Tz?
 
Hii kata funua ya CCM ni zaidi ya umafia. Wengine tuliwaonya humu mkaishia kututukana.

Maswali ya kujiuliza, ni kwa nini turn up ni ndogo this time. Maana ingekuwa hoja ya kuongeza kura, tungeshuhudia idadi ya wapiga kura ikiwa kubwa.

Ukiyaangalia matokeo haya yanaakisi kabisa zile nyomi za mikutano ya Lissu kwa numbers

Wapinzani tunaishi nao hapa nchini, lakini hawajawahi kuielewa nchi yetu. Kwenye hii nchi huwezi kushinda uchaguzi kwa kutegemea support ya middle class na upper class ambao ndio wana heavy presence kwenye social media platforms, claiming the “noisiest minority” title.

Mtaji mkubwa wa CCM ni watu wa maisha ya chini ambao ndio wengi zaidi. These people have little or no access to social media platforms. The opposition has failed to meaningfully penetrate and capture this silent majority!
 
Back
Top Bottom