Tushirikiane wote kujifunza neno la Mungu /neno la leo

Tushirikiane wote kujifunza neno la Mungu /neno la leo

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
4,014
Reaction score
4,600
Tunaishi katika nyakati/zama za mwisho kabisa huku unabii kuhusu UNYAKUO WA WATAKATIFU WALIOKO DUNIANI /KURUDI KWA YESU MARA YA PILI kukiwa kumekaribia sana kwa mujibu wa ufunuo na maandiko.

WAKATI WAKATI TULIONAO NI MCHACHE SANA, sisi kama RAIA WA MBINGUNI tunaosafiri safari ya kuelekea MBINGUNI kwenye makao yetu ya kudumu, tukijua hapa duniani sio kwetu na tunapita tu na maisha ya duniani ni ya muda mfupi sana.

1)hatujui saa wala dakika ambayo tutatwaliwa tutaondolewa/MUDA wetu wa kuishi hapa duniani utaisha ama unyakuoa utatokea, hivyo kila dakika ya MUDA tulionayo tukiwa hapa duniani ni mali endapo tuki itumia kwa utukufu wa Mungu, na itakuwa ni hasara tukitumia muda wetu mwingi zaidi na kuwekeza TUKIZITUMIKIA MALI na kupenda pesa na kuzitafuta pesa,
nyakati za mwisho.

Watu watapenda pesa kuliko chochote kuliko kumpenda Mungu, kuliko utu..upendo kati ya mtu na utu UTAPOA ,watu watapenda viti/mali kuliko utu /Mungu..na wengi hali wakiitamani pesa watajifarakanisha na imani yao na kujichomankwa maumivu makali.
PIA wengi sasa watakuwa wanaitumikia pesa badala ya kumtumikia MUNGU ,na huwezi kuwatumikia ma bwana wawili,yani umtumikie Mungu na utumikie Mali,lazima utampenda mmoja zaidi.

Biblia imetupa maneno ya hekima katika hili..kwamba tulinde sana moyo wote kwani ndipo zitokapo chemichemi za uzima kwa maana kule hazina yako iliko ndiko uliko moyo wako yaani kama utawekeza zadi katika kiyafikia mafanikio ya hapa duniani kuliko unavyowekeza katika hazina yako ya mbinguni kwa Mungu, mkwamba ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ilivyo kwa tajiri kwa sababu moyo wako utakuwa zaidi kule ulikowekeza MUDA wako zaidi na hiyo pia ni IBADA YA SANAMU KUTUMIKIA MALI..badala ya Mali zitumike kumtumikia Mungu, ikiwemo MUDA ,muda nao ni mali unagawaje muda wako katika masaa 24 ya siku ,unawekeza zaidi wapi huko ulikowekeza zaidi ndiyo ibada yako ndiyo moyo wako uliko..

watu wengine hatuji kwenye ibada kusali kama kuna kazi ya kuingiza ipo inakuhitaji kufanya MUDA huo ambayo itakuingizia hela au lipo jambo ambalo inaliona ni muhimu kuhudhuria au kufanya MUDA huo,tunakuja kwenye ibada muda ambao tunafikiri hatuna mambo mengine dearest ya kufanya muda huo.

Ila biblia inatumbia tuutafute kwanza ufalme wa mbingu,na mengine yote tutazidishiwa,na kwamba BWANA asipoujenga mji au asipoulinda mji yeye aujengao na kuulindao afanya kazi bure.
Kama unakusanya bila uwepo /kumtanguliza Mungu basi haukusanyi bali UNATAPANYA yani ni sawa na kuweka katika MFUKO ULIOTIBOKA.

Msingi imara wa kujenga/ kufanya jambo lolote ni kujenga juu ya MWAMBA IMARA ambao ni YESU.
hata dhoruba ikija jambo lilojengwa kwa kuanza na msingi imara YESU halitatikisika/halitatetereka halitabomoka.

Na mtu mwenye akili nyingi na aliyechagua fungu lililo JEMA ni yule tu anayemtanguliza na kumtegemea Mungu wakati wote na muda wote..GOD FIRST(MUNGU KWANZA)mengine yote yafuate NYUMA baadae.

Heri anayemtumikia Mungu kuanzia wakati wa UJANA WAKE mpaka mwisho amechagua fungu lililo JEMA.

Hakuna aliyewahi kumtumikia Mungu halafu BWANA akampungukia akamuacha yeye na uzao wa watoto wake.
Kumtumikia MUNGU sio ujinga ,wala sio kupoteza MUDA ,vijana wanaoimba kwaya kanisani au kuhubiri injili au kufanya kazi za kanisa SIO KWAMBA NI WAJINGA au wanapoteza MUDA au hawafanyi kazi au wanachezea muda wao ,ila nawaonea wivu wamechagua fungu lililo jema ,na hawa NDIO WENYE AKILI..na watauona mkono wa Mungu katika maisha yao na watoto wao..SADAKA WALIYOITOA YA MUDA WAO wa ujana wao katika kumtumikia Mungu.

SIOKWELI kwamba watu WOTE ambao tunapitia hali duni za kiuchumi, hatujajipata kiuchumi, bado tuna jitafuta kimaisha kwamba ETI hatufanyi kazi kwa bidii,ama hatuna akili, ama ni wavuvu ama ni wazembe..la hasha ,WAPO bbaadhi yaa masikini wanafanya kazi kwa bidii, wamesoma kuliko wengine ,wanaomba ajira ,wanajishighulisha na wanamtumikia MUNGU lakini bado WAKATI WA BWANA kuwainua hauhafika...SARA alipata mtoto katika uzee wake ..MUNGU huwa anajibu kwa wakati wake ,hachelewi wala hawai.

Tusijipambanie kwa nguvu zetu wenyewe,ipo njia ionekanayo ni njema machoni pa mwanadamu ila mwisho wake ni mauti,

PIA TUSIJILINGANISHE NA MTU YEYOTE
Utaona mwenzako wa umri rika lako ama mnafanya shughuli moja ama mnapokea mshahara sawa ,ama mnalingana elimu,umri ,n.k..lakini ghafla unaona mwenzako mmeanza pamoja ila yeye ana mafanikio makubwa kuliko wewe,
HUJUI hayo mafanikio ameyapataje.

MAISHA SIO MASHINDANO haushindani na yeyote, kila mtu anakusudi lake na ameitwa kutumika kwa nafasi yake na wakati wake na kuna vitu tofauti vipawa na karama tofauti kwa watu tofauti na hata vidole vya mikono yako havilingani.Na kila mtu na kila jambo lina wakati wake.

WAKATI wa Mungu ni sahihi,tuwe na IMANI isiyokuwa na mashaka, TUMAINI, na UVUMILIVU..na yale matunda ya Roho mtakatifu, tukikosa hivi ndio utaona IBRAHIMU na SARA walipofika ukomo wa uwezo na akili za kibinadamu katika kusubiri kupata mtoto wakajipigania wao wenyewe wakaishia kupata mtoto ISHIMAILI lakini Mungu alikuwa amewaandalia ISAKA. ukikimbia kwa haraka ,USIHARAKIE MAISHA ,utajikuta hata kazini unachukua RUSHWA, UNAIBA /ufisadi, wizi, unadhulumu unafanya biashara haramu,madili ili UPATE MAFANIKIO YA HARAKA HARAKA..ukijipambania mwenyewe kwa akili za mwanadamu..na hiyo njia hata kama inaonekana ni njema machoni pa wanadamu ila mwisho wake ni MAUTI

Kwa hiyo hata ukichelewa kupata MAFANIKIO kama mtoto kazi, nyumba na gari ndoa, kazi/ajira, mgonjwa umekosa AFYA,n.k

Mungu ATAKUREJESHEA kicheko (Isaka), atakurejeshea wakati /ataukomboa wakati/muda hiyo AFYA iliyougua atakurudishia afya,na miaka iliyoliwa na tunutu, nzige, madumadu.

YOTE KATIKA YOTE
Tumtangulize Mungu kwanza pamoja na mbio zetu za kutafuta mafanikio ,pesa na misha ya hapa duniani ambapo sipo kwetu tunapita, tuwe na kiasi,tufanye yote kwa utukufu wa Mungu.
GOD FIRST..MUNGU KWANZA.
 
Ujinga , utakufa yatapita mabilioni ya miaka watakuja na wengine watasema kama wewe🚮
 
LUKA 17:34-36
34Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa. 35Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa." 36Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. 37Hapo wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia."
 
Mathayo 24:36-51
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye. Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu. Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina. Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja. Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe. Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.” Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake? Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo. Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote. Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: ‘Bwana wangu amekawia kurudi,’ kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi, bwana wake atakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua. Atamwadhibu vibaya na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.
 
Mathayo 24:36-51
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye. Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu. Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina. Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja. Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe. Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.” Yesu akaendelea kusema, “Ni nani basi mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya watu wake, awape chakula kwa wakati wake? Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakapokuja atamkuta akifanya hivyo. Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote. Lakini kama mtumishi mbaya akijisemea moyoni: ‘Bwana wangu amekawia kurudi,’ kisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, akaanza kula na kunywa pamoja na walevi, bwana wake atakuja siku asiyoitazamia na saa asiyoijua. Atamwadhibu vibaya na kumweka kundi moja na wanafiki. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.
Hiyo Aya haifundishi unyakuo wa Siri

Mifano ya Yesu nyie mnaifanya dhahiri mnatemgeneza mafundisho yenu
 
Unyakuo ulishatokea na sio kama wengi walikuwa wanatarajia kupitia mapokeo ya dini na ukombozi bado unaendlea hadi sasa.

Sasa wote tumerejea direct to the Real Source na sio kupitia intermediary (mtu kati) tena.
 
Unyakuo ulishatokea na sio kama wengi walikuwa wanatarajia kupitia mapokeo ya dini na ukombozi bado unaendlea hadi sasa.

Sasa wote tumerejea direct to the Real Source na sio kupitia intermediary (mtu kati) tena.
Ndugu hivi Unajua hilo fundisho la unyakuo ni kinyume na maandiko ?

Unajua asili ya hilo fundisho ?

Unamjua mwanzilishi wa hilo fundisho?

Turudi kwenye biblia
 
Mafundisho yafuatayo yanapaswa kupimwa kwa Biblia.

1) Fundisho la kumkomboa mzaliwa wa kwanza. (Kuna somo tayari katika Hilo).

2) Fundisho la kujimaliza

3) Fundisho la Unyakuo wa Siri na kujiokoa kwa damu yako katika dhiki kuu, pamoja na utawala wa miaka 1000 ya Yesu pale Palestina.

4) Fundisho la utatu.

5) Fundisho la kuomba kwa jina la mtume ama nabii wa huduma fulani.

6) Fundisho la huduma ya ukombozi. (Hapa Kuna mazagazaga kibao)

7) Fundisho la kugawanya Biblia kwamba Kuna maandiko ya Wakristo na ya Wayahudi

8) Fundisho la kuuza maji na mafuta

9) Fundisho la kuhesabiwa haki kwa matendo.

10) Fundisho la kujazwa Roho huku muhusika anapiga kelele na kulia na kugalagala chini.

11) Fundisho la namna ya utoaji wa Sadaka na Zaka.

12) Fundisho la mtawalio wa Kanisa.

13) Fundisho la mpinga Kristo ni nani?

14) Fundisho la kuzimu. (Hapa Kuna mengi ya ajabu ajabu)

15) Fundisho la ulimwengu wa Roho ni upi?

16) Fundisho la msamaha wa dhambi. (Hapa ni muhimu sana kupachunguza maana wengi wanapotelea hapa).

17) Fundisho la Hawa kupewa mimba na Nyoka na kumzaa Kaini.

18) Fundisho la kusafisha nyota au kurudisha nyota iliyoibiwa.

Mengine unaweza kuongezea wewe hapo ili nayo yawekwe kwenye ratiba ya kujifunza hapa.
 

Attachments

  • Screenshot_20250915-222906.jpg
    Screenshot_20250915-222906.jpg
    97.4 KB · Views: 41
KIBURI
Kiburi ni hali ya moyo wa mtu kuinuka,kujisifu,kujitukuza ,KUJIKWEZA kutokana na kitu fulani alichonacho/anachomiliki ambacho kinamtofautisha yeye na mwingine.

mfano 1.
KIPAWA/KARAMA/KIPAJI alichojaliwa yeye tofauti na wengine.
mfano hapo zamani LUSIFA alikuwa malaika mkuu Wa sifa!(kerubi) Aliongoza jeshi lote la mbinguni kumsifu Mungu alikuwa na kinubi,sauti,na vyombo vya muziki ndani yake

mfano 2
MUONEKANO
Pia Lusifa alikuwa na muonekano mzuri,alikuwa aki ng'aa mngao(nyota ya alfajiri...alikuwa akiangaza nuru)

mfano 2

Sauli alikuwa mfalme wa kwanza wa Israel. Alikuwa mrefu na mzuri, kama watu walivyopenda. Sauli alikuwa mfalme mwema kwa miaka michache ya mwanzoni aliyotawala Israel. Lakini, baadaye alikuwa mfalme muovu ambaye hakumtii Mungu, Kwa hiyo Mungu alimchagua mtu mwingine ambaye angekuwa mfalme badala yake.

Hivyo tunaona KIBURI cha LUSIFA kilitikana na majaliwa ya UZURI WA MUONEKANO WAKE ,kipaji chake cha MUZIKI ,cheo/nafasi yake chake n.k

MALI
mfano 3
Tajiri NABALI mumewe Abigaili,tajiri aliyewajibu jeuri/kibri,dharau vijana waliotumwa na Daudi.

Tajiri aliyevuna mavuno ya chakula mengi akajaza chakula ghala zote zikajaa hata zisitoshe sehemu ya kuhifadhi akajitukuza yeye badala ya kumtumuza Mungu ,akafa usiku huo kabla hajala hata matunda ya mavuno yake.

ELIMU
mfano 4
waandishi na mafarisayo(wasomi wa wakati huo)

mfano 5
Cheo / mamlaka/nafasi ya uongozi.
mfalme Nebucchadnezzer/ nebukadreza,mfalme Farao mfalme PILATO ,mamlaka yote waliyonayo viongozi wamepewa fursa hiyo ya ukuu/utawala aliyewapatia ni Bwana Mungu ,na pia Mungu anaweza kuwapokonya wafalme mamlaka hiyo na kuwapa wengine walio wanyenyekevu.

KIBURI NI DHAMBI MBAYA SANA.
kwa sababu mtu mwenye moyo wenye kiburi,kwanza HATII (kutokutii sheria ya Mungu ni UASI) hashauriki/anajua kila kitu,hasikilizi hata akikosea HAJISHUSHI kutubu..mfano mfalme SAULI hata alipokosea Mungu mara ya kwanza hakutubu..akakosea mara ya pili ...tena.

tofauti na Mfalme Daudi alikuwa MNYENYEKEVU...mwepesi wa kutubu kwa haraka anapokosea,..na moyo wake haukuwa na kiburi bali unyenyekevu.

MADHARA YA DHAMBI YA KIBURI NI MENGI
mwenye kiburi atashushwa chini,atang'olewa ,atapata aibu,ataharibiwa..atapata uharibifu..ni chukizo hafurahishwi Mungu wala wanadamu..Tajiri NABALI aliyekuwa mkali na jeuri/kibri watu hawakumpenda.


TUFANYE NINI ILI TUIEPUKE DHAMBI YA KIBURI /TUSIWE NA KIBURI??
1)Kila tulichonacho tulichokipata,tulichofanikiwa kukipata..ni BWANA MUNGU ndiye aliyetufanikisha..

So neither the one who plants nor the one who waters is anything, but only God, who makes things grow.

si aliyepanda mbegu wala aliyemwagilia maji amefanya kitu bali yeye anayefanya mimea IOTE.

Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa,

Hata sasa BWANA ametusaidia.

2)Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.

MUNGU ATUSAIDIE ili tuepuke dhambi ya kiburi cha uzima,kiburi cha elimu,kiburi cha mali,kiburi uzuri/muonekano (mzuri wa kuvutia),kiburi cha kipawa/karama huduma /vipaji vyetu,kiburi cha nguvu ya cheo/mamlaka au nafasi ya uongozi n.k na chochote ulichojaliwa na Mungu ambacho unacho wengine hawana.
Mungu atusaidie ATUPE MOYO wa UNYENYEKEVU.

DAUDI anasema
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu. Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu

Linda sana moyo wako kwani ndiko zitokako chemichemi za uzima (usiujaze moyo wako kiburi,majivuno ,PRIDE/ni dhambi mbaya sana).
 
Ndugu hivi Unajua hilo fundisho la unyakuo ni kinyume na maandiko ?

Unajua asili ya hilo fundisho ?

Unamjua mwanzilishi wa hilo fundisho?

Turudi kwenye biblia
Unyakuo unaongelewa na kufundishwa ni kupaa mawinguni ila sivyo kama walivyofundishwa bali ni awakening ya ufahamu na kumjua Muumba,maana kama humjui Muumba wako despite ulivyofundishwa wewe ni mfu anaetembea.
 
Unyakuo unaongelewa na kufundishwa ni kupaa mawinguni ila sivyo kama walivyofundishwa bali ni awakening ya ufahamu na kumjua Muumba,maana kama humjui Muumba wako despite ulivyofundishwa wewe ni mfu anaetembea.
Walokole wengi wanafundisha unyakuo wa Siri
 
Back
Top Bottom