Tushirikiane wote kujifunza neno la Mungu /neno la leo

Tushirikiane wote kujifunza neno la Mungu /neno la leo

KIBURI
Kiburi ni hali ya moyo wa mtu kuinuka,kujisifu,kujitukuza ,KUJIKWEZA kutokana na kitu fulani alichonacho/anachomiliki ambacho kinamtofautisha yeye na mwingine.

mfano 1.
KIPAWA/KARAMA/KIPAJI alichojaliwa yeye tofauti na wengine.
mfano hapo zamani LUSIFA alikuwa malaika mkuu Wa sifa!(kerubi) Aliongoza jeshi lote la mbinguni kumsifu Mungu alikuwa na kinubi,sauti,na vyombo vya muziki ndani yake

mfano 2
MUONEKANO
Pia Lusifa alikuwa na muonekano mzuri,alikuwa aki ng'aa mngao(nyota ya alfajiri...alikuwa akiangaza nuru)

mfano 2

Sauli alikuwa mfalme wa kwanza wa Israel. Alikuwa mrefu na mzuri, kama watu walivyopenda. Sauli alikuwa mfalme mwema kwa miaka michache ya mwanzoni aliyotawala Israel. Lakini, baadaye alikuwa mfalme muovu ambaye hakumtii Mungu, Kwa hiyo Mungu alimchagua mtu mwingine ambaye angekuwa mfalme badala yake.

Hivyo tunaona KIBURI cha LUSIFA kilitikana na majaliwa ya UZURI WA MUONEKANO WAKE ,kipaji chake cha MUZIKI ,cheo/nafasi yake chake n.k

MALI
mfano 3
Tajiri NABALI mumewe Abigaili,tajiri aliyewajibu jeuri/kibri,dharau vijana waliotumwa na Daudi.

Tajiri aliyevuna mavuno ya chakula mengi akajaza chakula ghala zote zikajaa hata zisitoshe sehemu ya kuhifadhi akajitukuza yeye badala ya kumtumuza Mungu ,akafa usiku huo kabla hajala hata matunda ya mavuno yake.

ELIMU
mfano 4
waandishi na mafarisayo(wasomi wa wakati huo)

mfano 5
Cheo / mamlaka/nafasi ya uongozi.
mfalme Nebucchadnezzer/ nebukadreza,mfalme Farao mfalme PILATO ,mamlaka yote waliyonayo viongozi wamepewa fursa hiyo ya ukuu/utawala aliyewapatia ni Bwana Mungu ,na pia Mungu anaweza kuwapokonya wafalme mamlaka hiyo na kuwapa wengine walio wanyenyekevu.

KIBURI NI DHAMBI MBAYA SANA.
kwa sababu mtu mwenye moyo wenye kiburi,kwanza HATII (kutokutii sheria ya Mungu ni UASI) hashauriki/anajua kila kitu,hasikilizi hata akikosea HAJISHUSHI kutubu..mfano mfalme SAULI hata alipokosea Mungu mara ya kwanza hakutubu..akakosea mara ya pili ...tena.

tofauti na Mfalme Daudi alikuwa MNYENYEKEVU...mwepesi wa kutubu kwa haraka anapokosea,..na moyo wake haukuwa na kiburi bali unyenyekevu.

MADHARA YA DHAMBI YA KIBURI NI MENGI
mwenye kiburi atashushwa chini,atang'olewa ,atapata aibu,ataharibiwa..atapata uharibifu..ni chukizo hafurahishwi Mungu wala wanadamu..Tajiri NABALI aliyekuwa mkali na jeuri/kibri watu hawakumpenda.


TUFANYE NINI ILI TUIEPUKE DHAMBI YA KIBURI /TUSIWE NA KIBURI??
1)Kila tulichonacho tulichokipata,tulichofanikiwa kukipata..ni BWANA MUNGU ndiye aliyetufanikisha..

So neither the one who plants nor the one who waters is anything, but only God, who makes things grow.

si aliyepanda mbegu wala aliyemwagilia maji amefanya kitu bali yeye anayefanya mimea IOTE.

Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa,

Hata sasa BWANA ametusaidia.

2)Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.

MUNGU ATUSAIDIE ili tuepuke dhambi ya kiburi cha uzima,kiburi cha elimu,kiburi cha mali,kiburi uzuri/muonekano (mzuri wa kuvutia),kiburi cha kipawa/karama huduma /vipaji vyetu,kiburi cha nguvu ya cheo/mamlaka au nafasi ya uongozi n.k na chochote ulichojaliwa na Mungu ambacho unacho wengine hawana.
Mungu atusaidie ATUPE MOYO wa UNYENYEKEVU.

DAUDI anasema
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu. Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu

Linda sana moyo wako kwani ndiko zitokako chemichemi za uzima (usiujaze moyo wako kiburi,majivuno ,PRIDE/ni dhambi mbaya sana).
Pale kwenye hiyo hadithi yenu kwamba Mungu alimtia farao moyo mgumu ili ampige halafu aonyeshe kuwa yeye ni mwamba ni kiburi au sio kiburi?
 
Back
Top Bottom