Mkuu App yako ni nzuri, sababu ni ya nyumbani, na simple kutumia lakini sasa ambacho sijakipenda ni
1. Rangi ulizotumia hasa kwenye calender. Ile blue ya fertility window na blue ya ovolution days kama hazileti muonekano mzuri.
2. Siku za hatari huwa ni siku tatu kabla na siku tatu baada ya ile siku ya kati kati jumla zinakuwa 7 na ongeza siku moja ya kujuhami kabla na baada ya siku ya katikati ( hii ni kwaajili ya wale wanao panga uzazi wa mpango kwa kutumia kalenda) lakini kwenye app naona kama siku za hatari ni chache sana.
Mfano angalia picha hapa chini ni mzunguko wa mtu mmoja katika katika app yako na app inaitwa my calendar
Hapo inaonesha 27 bado yupo safe day ( low chance of getting pregnancy)
Hapa inaonesha yupo siku ya hatari ( medium chance of getting pregnancy)
3. Kipengele cha pin code hakifanyi kazi.