Habari,
Watu wengi hapa Tanzania tunasubiri kwa hamu ujio wa Starlink ila ni wachache wanaojua matumizi yake ni yakoje pamoja na bei zake.
Ningependa kuzungumzia zaid vitu ambavyo tushavijua kupitia watumiaji wa Nigeria,
- Starlink inauzwa $578.93 hivi ni vifaa peke kwa Tanzania ni sawa na 1,351,942./= na utalipia kwa account ya Dollar sijui kwetu itakuaje maana kwa Nigeria card zao za ndani hazikubali.
- Pia Starlink wanakupa 30 days free trial kama hutopata huduma upendavyo unauwezo wa kurudisha na kulipwa pesa yako yote.
- Starlink sio unlimited ila iko limited kwa kiwango kikubwa tofauti na provider wengine, Una kiwango cha kutumia internet cha 1terabyte kwa mda wa asubuhi mpka jioni na Jioni mpka asubuhi hautokuwa na limitation yeyote, Ukifanikiwa kumaliza 1 terabyte speed itapungua ila utakuwa na uwezo wa kununua 1Gb kwa $0.25 ambayo ni sawa na tsh 584.75.
Haya ni machache ambayo tunayajua kwa sasa na kama kuna zaidi unaweza kushare, Je, tutegemee yepi kutoka kwa Starlink ikifika Tanzania?