Tusichokijua kuhusu Starlink

Tusichokijua kuhusu Starlink

Post bora sana ya muda wote hii![emoji122][emoji122][emoji122]
Mkuu Asante sana kawaida tu. Nitaendelea kuwaletea post na nyuzi nyingi zaidi zilizoshehen nondo na madini za kutosha. Kinachotakiwa ukae tu mkao wa kula.

Sauh'waaah?!
 
Habari,

Watu wengi hapa Tanzania tunasubiri kwa hamu ujio wa Starlink ila ni wachache wanaojua matumizi yake ni yakoje pamoja na bei zake.

Ningependa kuzungumzia zaid vitu ambavyo tushavijua kupitia watumiaji wa Nigeria,
  • Starlink inauzwa $578.93 hivi ni vifaa peke kwa Tanzania ni sawa na 1,351,942./= na utalipia kwa account ya Dollar sijui kwetu itakuaje maana kwa Nigeria card zao za ndani hazikubali.
  • Pia Starlink wanakupa 30 days free trial kama hutopata huduma upendavyo unauwezo wa kurudisha na kulipwa pesa yako yote.
  • Starlink sio unlimited ila iko limited kwa kiwango kikubwa tofauti na provider wengine, Una kiwango cha kutumia internet cha 1terabyte kwa mda wa asubuhi mpka jioni na Jioni mpka asubuhi hautokuwa na limitation yeyote, Ukifanikiwa kumaliza 1 terabyte speed itapungua ila utakuwa na uwezo wa kununua 1Gb kwa $0.25 ambayo ni sawa na tsh 584.75.
Haya ni machache ambayo tunayajua kwa sasa na kama kuna zaidi unaweza kushare, Je, tutegemee yepi kutoka kwa Starlink ikifika Tanzania?
Hebu tujuze zaidi. Hao starlink wanatoa hufuma zingine za mwasiliano kama simu sms au ni internet tu.
 
Ili serikali iruhusu ni lazima ijue itafaidikaje
 
Mpaka sasa Elon Musk kapigwa kanzu na tobo haelewi mpira umepitaje pitaje. Kapigwa kihunzi kimoja tu cha kufungua ofisi hapa bongo yupo chali.
#bureaucracy #wahunisiowatu #utajuahujui #huwekutoboa #10% #kitulizekwanza #tibuamshono
 
Mzee una run machine gani kumaliza 1000Gb, hata nikiangalia HD movies kila siku for 2 hours simalizi 50Gb kwa mwezi
Mpka sasa simu yangu inasoma Gb 167 zilotumika na hapo sikai home kutwa kwenye box inasoma 137 gb na hapo pia sio full day na kuna ps hapo kuna kama 150 gb. Sijaendelea kwengine ila ningekuwa heavy user basi unamaliza.
 

Attachments

  • Screenshot_20230517-172404.png
    Screenshot_20230517-172404.png
    42.7 KB · Views: 6
Mpaka sasa Elon Musk kapigwa kanzu na tobo haelewi mpira umepitaje pitaje. Kapigwa kihunzi kimoja tu cha kufungua ofisi hapa bongo yupo chali.
#bureaucracy #wahunisiowatu #utajuahujui #huwekutoboa #10% #kitulizekwanza #tibuamshono
Bongo ni aibu tupu, selfishness na ujinga wa viongozi wetu vinaua kila kitu
 
Hiyo dollar 578 unanunua kifaa gani specifically, na ukishanunua kifaa husika bando ni kiasi gani?
 
Kwa Marekan wana package ya Rv ambayo haitaji location ya mtu ila hupati kipao mbele kma nyengine so ata speed yako inaweza kuwa mbaya. Na package ya home huwezi kuhama hama nayo ukiweka kwako ndo hapo hapo. Ntalifatilia zaid hili kuona uhakisia wake
 
Back
Top Bottom