Tusichokijua kuhusu Starlink

Binafsi Sina uelewa sana na hii starlink..lakini I wish ije ili pawe na competition na hawa watwana wetu akina voda, tigo, na Airtel....Kwa maana ni mateso matupu..labda wakipata mpinzani wanaweza kuboresha huduma
Ni kweli hata mimi nnachokitaka ndio ushindani kwani saa hizi mitandao ya simu yote kwa pamoja wanashirikiana kuwa na ukiritimba kwenye kusambaza mbs hata kama sio starlink yeyote tu aje awa changamshe hawa waliopo kwani wameridhika 1gb kwa buku tatu si wizi huu.
 
Raia wa kawaida hana uwezo wa kutumia Starlink.
Hujajua tu Kuna fulsa hapo....by the way mm sometimes huwaga na endaga kuzurula kwenye forum mbali mbali Africa na ulaya....Kule utapata maarifa...
Before watu kuanzisha nyuzi humu Jf kuhusu starlink nilipanga nianzishe thread ila nilitingwa na majumumu sikuweza kuandika Kwa utulivu...

Kuna mdau mmoja aliuliza ukisha fanyiwa installation Kuna uwezekano ukawa nyumbani let say ubungo alaf still ukaendelea kutumia ukiwa mbagala au mkuranga???

Tumsaidie kumjibu huyo mdau kwenye swali lake? Hapo juu
 
Ukifanikiwa kumaliza 1 terabyte speed itapungua ila utakuwa na uwezo wa kununua 1Gb kwa $0.25 ambayo ni sawa na tsh 584.75.
1 GB kwa Tshs 584.75

Starlink aje hata KESHO tutalipia tu, mitandao yetu 1 GB inauziwa 3000 na hapo siku haiishi bando limekata
 
Hii ni fursa kwa wanaoelewa kukumbatia fursa,
 
Upo sahihi kwa asilimia 100 na 90
 
Mitandao ya simu yatapunguza gharama zao pindi pale watanzania wengi watahamia kwenye Unlimited plans, majumbani na makazin hapo ndo wataona traffic kwao imepungua.
Hata wewe utahamia Starlink?
 
Kwanza kulingana na ukiritimba na uzuzuta wa sera zetu za kikodi tena za kilimbukeni gharama hazitokia sawa na huko nigeria, trust me and thank me later
 
Starlink wawauzie provider wetu in bulks, and then wao waone jinsi gani sisi tutapata huduma nafuu, na kasi ya kuridhisha, ugonjwa wetu mkubwa ni speed, Internet imara isiyokatakata, na affordability!
Labda kwa njia hii! Ila si vinginevyo kwa jinsi ninavyojua hawa wa bongo wa kodi itakua ni huduma ghali sana kuliko huu utupolo tunaosambaziana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…