Mkuu, asante sana kwa maelezo yako yakinifu. Umefafanua vema. Mao hakutaka China ya kuwekewa vikwazo kidogo, uchumi wa nchini unaporomoko kutoka 12% mpaka 2% tena kwa muda mfupi. Na hii inaonyesha unaelewa China historia yake kwa kuangalia mbele tu badala ya kuangalia Historia ya China kwa pande zote, mbele kulia nyuma na kushoto. Usisome historia ya nchi kama herufi a ba che de e.....!
Mkuu, ninaposema Tanzania TUJITEGEMEE kweli kweli ni pamoja na kutojenga uchumi wetu wa nchi kwenye misingi ya 'mpira wa povu la sabuni'. Msingi ambao ukija upepo wa vumbi mpira unapotea. Ni katika mazingira haya Wachina wanalazimika kurejea kiana misingi ya Mao! Na kweli lazima wareje ili watoke hapo walipo kwama.
Mkuu, ni katika muktadha huo tunaitumia historia ya China kwa manufaa; yaani tusirudie makosa waliyofanya.
Mkuu, ninatarajia tutaelewana katika hili.