Najua kabisa umoja wa mataifa wanazo rekodi zao za uhakika kuwa Tanzania ambayo ndio kitovu cha kuhifadhi wakimbizi tangu miaka ya 1960's hajafikia hatua ya kutengeneza wakimbizi wa kisiasa kama Lema.
Tungesikia UN wametoa ripoti juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa Tanzania. Lakini mpaka sasa hakuna UN wapo kimya,sisi wenyewe tunaoishi hapa Tz ni mashuhuda.
Jambo la msingi tunatakiwa kufahamu kuwa kuna aina nyingi za wakimbizi. Wakimbizi wa kiuchumi pia wapo. Hawa ni wale hukimbia nchi zao kusaka matonge baada ya line za kuingiza kipato kukata kamba.
Nchi kama Kanada ni nchi ambayo hupokea wageni wa namna mbalimbali,hasa wakimbizi wa kiuchumi,ndio maana ukienda Kanada utakuta Wahindi walioenda kusaka tonge ni wengi tu.
Kwa ujumla tunafanya vibaya sana kuichafua nchi yetu kuwa kuna mkimbizi wa kisiasa ametusua kwenda Kanada wakati tunajua amesoma alama za nyakati na kujua Ubunge umekata hivyo anatakiwa akatafute mkate na siagi Kanada. Nchi hii haitawaliwi kiimla wala kwa mkono wa chuma. Tuache kukurupuka na kuzalisha uongo mchana kweupe.