Tusimlaumu Rais Samia pekee viongozi wa vyombo vya usalama Tanzania hawana Uzalendo

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Tusimlaumu Raisi Samia pekee viongozi wa vyombo vya usalama TZ hawana Uzalendo

Polisi na usalama kuiba kura wakati wameapa kulinda sheria huo ni uzalendo wa aina gani?
Polisi na usalama kula ruswa huo ni uzalendo wa aina gani?
Polisi na usalama kutumika kisiasa badala ya kuweka maslahi ya nchi huo ni uzalendo gani?

Hivyo tunatakiwa pamoja na Raisi Samia kuhoji hawa viongozi ambao wamegeuzwa kuwa machawa badala ya viongozi

Zambia ilikuwa kama Tanzania mpaka pale vyombo vya usalama vilipo amua kuweka nchi mbele na kusema tutafuata katiba sio siasa walikataa kuiba kura na kupendelea

Lakini vijana wetu sio wale wa 1990's na 2000"s yaani upewo wao ni mdogo pamoja na kuongezeka kwa vyuo. Vijana wengi ni wajinga jinga na washabiki sio kama wenzao wa nchi jirani. vilana wamekuwa legelege sana. Kati ya wazalendo ambao tunawakumbuka mpaka leo ni Nyalali na IGP Mahundi. Walifuata viapo vyao kwa nchi sio Chama chochote au Mtu








Mwema naye alikatisha mkataba wake baada ya Jeshi kutuhumiwa kwa manufaa ya umma.

​

IGP Said Mwema Ajiuzulu. Jeshi la Polisi Limekuwa Jeshi la Mauaji​


Viapo fake kiapo cha nchi unaenda kufanya kazi kisiasa!


View: https://youtu.be/IA_JyIt7W9Y?si=TUOT_dDa8rWXJh_z
 
Tatizo ni kuwa Tanzania rais ni mungu mtu na anachotaka ndiyo kinachofanywa.
 
Tatizo ni kuwa Tanzania rais ni mungu mtu na anachotaka ndiyo kinachofanywa.

Hatujawahi kuona hawa viongozi wa usalama machawa wakisema hapana! mbona viongozi wa zamani wakina Mahundi waliweza kumwambia Mwinyi hatufanyi hivyo. Mbona mkuu wa Polisi Mangu alimkatalia Mgufuli kunyanyasa leo mbona yupo ingawa alihamishwa ni uzalendo tu
 
wamemwingiza chaka, umeona wazungu wa EU walivyojaa, soon trump atasikia.
 
Kama unajua kiingereza naomba sana ukipata muda usome kuhusu hali ya kisaikolijia inayoitwa ''spiral silence''.
 
Hili nalo mkalitazame.

Mafisadi wa kila aina wako kila kona vyombo vimejaa. Je tuvieleweje? Au wanakula sahani moja?
 

Kutaka kumtenganisha huyo na hao ni kutaka kujilisha upepo Bure!

Hiyo ni kama kutaka kufanyia uchambuzi wowote kesi hii ambayo hata wenye nayo wanajua ni ya kubumba!
 
Kila chama cha siasa kifanye siasa kwa kufuata sheria na katiba ya nchi,

ni muhimu sana wakiuka sheria na katiba ya nchi wakashughulikiwa kisawasawa na shaeria hizo hizo bila kujali kelele na mayowe ya vyama vyao ili iwe fundisho kwa vibaka na matapeli wengineo wa kisiasa 🐒
 

Mbona mwongeaji wa CCM alisema Chadema wataleta virusi vya magojwa hata kuhojiwa Polisi hajahojiwa! Watanzania wanaona wenyewe huwezi kuwa na vyombo ambavyo vinapendelea upande mmoja nchi ikabaki sawa . Angalia hawa hapa wanaongea hayo hayo.





View: https://youtu.be/zGj8vGvpLu0?si=qazN8HuoqbF9lzhj



View: https://youtu.be/WzDWfy64fTA?si=j4H0mNUToILQMuoB
 
Samia na vyombo vibalaumiwa Kwa lipi? Kuchukua hatua kuzuia uasi au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…