Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

Ole mushi atoa fact wenye itikadi zenu za siasa njooni mujibu
 
Tuanze na ahadi hewa tuliyopewa na CCM mwaka 2015 ya millioni 50 kila kijiji!!!!!
Yapo mengi sana waliyo tudanganya hasa lile la walimu kupewa laptop.

Hili ni bomu la kutega ambalo litalipuka muda wowote na wana ccm watalia kilio cha ngamia
 
Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.
Wewe mwenyewe mlevi
 
Umesurvey physically au kwenye google !?

Somo 1: sio kila kinachoandikwa mtandaoni ni kweli. Huu utafiti wako hauna supporting documents or links ambazo ni credible.

Marekani wakisitisha misaada wanayoitoa kwa mataifa ya Africa na Asia watashindwa kujimudu !?
Somo2: Marekani haijashindwa kujimudu ktk suala la afya, ni just allocation ya funds na resources i.e. military budgets yao ipo juu, wanatoa misaada mingi sana both serikali na raia wake mf: PEPFAR,USAID, Bill Gates etc.

.....
Next time jipange na uje na facts zikiwa na credible supporting documents/links
 
Yapo mengi sana waliyo tudanganya hasa lile la walimu kupewa laptop.

Hili ni bomu la kutega ambalo litalipuka muda wowote na wana ccm watalia kilio cha ngamia
Imeonekana hawajui kuzitumia..hivyo zitaishia kuuzwa tu.
 
Elimu bure iliwezekana vip. Acheni ubinafsi. Angeahidi Magufuli ingewezekana na ungeshangilia...sasa kwa kuwa kasema Lissu, imekuwa nongwa. Nyerere alitoa huduma ya afya bure mpaka mwaka 1985 aliwezaje.

CCM mnashikiwa akili sana na vilaza. Sera za CCM zinaamini katika ujamaa, na uchumi wa nchi kuendeshwa na serikali kuu. Sasa unashindwaje kutoa health care, au free education, free water services, etc

Kwa kauli yako, unapingana na sera ya ujamaa ya CCM anayoihubiri bepari wa kijamaa Magufuli, Bashiru, na Msanii Slow.
 
Put it differently, ni nchi gani hutoa elimu bure kwa wanafunzi wote wa secondary! Sasa kama jpm aliweza basi lisu ataweza. Ni mipango tu
TUSIMWACHE LISU ATUAHIDI YASIYOWEZEKANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kwenye kampeni za Lisu ana Mambo makubwa mawili anayowaomba watanzania wamchague nayo. Moja ni malalamiko yake ya kupigwa risasi hii Kwake Ni Kama Kete ya kuwaomba watanzania wamuonee huruma aingie Ikulu. Jambo la Pili ni Sera zake anazotakiwa awashawishi nazo watanzania ili wamchague kuwa Rais.

Nilishawahi kusema kuwa hakuna siku nitambeza Lisu kwa kupigwa Kwake Risasi na Wala sintoongea nikimuona analalamika kuwa mwili wake una machuma kila Mahali. Kama watanzania wataamua kumchagua kwa kuwa tu aliwahi kushambuliwa na watu wasiojulikana Hilo nimewaachia. Mimi nitajikita kwenye Sera zake ambazo kwangu ndio kipimo Cha kutoa kura yangu kumchagua Kiongozi katika ngazi zote iwe udiwani, Ubunge, au Urais nitazipima Sera kabla ya kuchagua.

Nimesikikiza Sera za mgombea urais Lisu anayo Mambo makuu matatu anayowaahidi watanzania kubwa kabisa ni kila mtanzania kumiki bima ya Afya, kupunguza Makato ya Wanufaika wa Bodi, kuleta maendeleo ya watu badala ya vitu. Haya ndio anayoyarudia kila Mara anaposhika kipaza sauti Leo tuongele moja kesho tutaongele lingine na leo tuanze na Bima ya Afya kwa kila mtanzania.

BIMA BURE

Nimejaribu ku survey nchi nyingi duniani, Ni nchi ipi yenye uwezo wa kuwapa wananchi wake wote Bima BURE sikuona.

Marekani ilijaribu kupitia Obama Care lakini baada ya Muda mfupi walishindwa na Obama care ikafa. Sababu kubwa Ni gharama za uendeshaji. Kutokana na U.S Census Bureau taifa la Marekeni lina watu milioni 28.1 tu ya wasiokuwa na Bima. Hivyo Obama care ilidhamiria kufanya Coverage ya watu milioni 28 tu kuwalipia huduma za Afya lakini wameshindwa kutokana na gharama zake. Hili ni taifa tajiri kuliko yote duniani limeshindwa kuwalipia watu milioni 28 tu je kwa Tanzania wenye Bima hawafikii milioni kumi je milioni Arobaini iliyobakia wanaofanya kazi wataweza kuwalipia gharama hizo?

Sababu nyingine ya wamarekani kukataa Obama care ni kuwa Kama itafanya kazi Kodi ingelipanda sana nchini marekani hivyo wakaamua kuitupilia mbali. Kuna nchi zinazotajwa kuwa na unafuu wa Bima Duniania lakini sio bure naomba kuzitaja:-

1.Ujerumani.

Ujerumani ndio taifa linaloonekana Kama Bima yake angalau Ina unafuu kwa wananchi wake. Lakini pia sio wajerumani wote ambao Wana Bima ya afya. Wafanyakazi wote nchini ujerumani wanalipia Bima zao kwa kushirikiana na waajiri. Wengine waliobakia wanalipia kiasi kidogo Bima zao.

2. Singapore

Singapore wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa Medshield ambao serikali kwa asilimia kubwa ndio inabeba gharama za matibabu lakini kila mtu nchini Singapore anatakiwa alipie asilimia 10 ya kipato chako kwenye mfuko huo. Kama ni Mkulima wanakupigia mahesabu asilimia 10 ya unachokipata ulipie kwenye mfuko wa bima, Kama ni mfanyakazi vivyohivyo pamoja na kuwa unaonekaba kuwa mfumo Bora kuliko yote duniani lakini bado unalipiwa na wenye kipato kikubwa bado wanaumia sana kukatwa asilimia 10 kwa ajili ya Bima.

3. Japani

Japani wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa SHIS mfumo huu nao watu wanatakiwa kujiandikisha na kulipia.

4. Uingereza.

Wao ndio kwa asilimia kubwa wamefanikiwa kwa kuwa hospital asilimia kubwa zinamilikiwa na serikali na wafanyakazi wote hulipwa na Serikali. Mfumo wao wa Bima wa NHS gharama zake zote hutolewa na Serikali. Ila bado una changamoto na mtu akitaka kutibiwa private ambako Kuna huduma nzuri na za haraka unatakiwa kulipia mwenyewe.

Hizo Zina unafuu Duniania Soma unafuu wake halafu tulinganishe na Tanzania.

Tanzania.

Tuna Bima ya NHIF ambayo huangaika na watumishi wa Umma na wategemezi wao. Huu tunauchangia asilimia Kama mataifa mengine yanavyouchangia. Tena asilimia tatu tu tofauti na mataifa Mengi sana Duniania.

Tuna mfuko mwingine iCHF (Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulio Boreshwa), huduma hii ya Bima ni kwa gharama nafuu kabisa kwa Watanzania wote katika Sekta ya Afya kwa Familia ya watu sita yaani Baba, Mama na watoto wanne kwa Tsh. 30,000/- tu kwa mwaka mzima. Una pata huduma zoote za matibabu kuanzia kituo kidogo cha Afya mpaka Hospital ya Mkoa.

Serikali Ina mpango pia wa kuleta Sheria Bungeni ya kuwataka watanzania wote kuingizwa kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

Mimi nataka kufahamu Lisu anataka kuifanyaje hiyo Bima yake. Sio kwamba nambeza la hasha nataka kufahamu Bima yake anayoihubiri Ina nini ndani na itakuwa inafanana na ya nchi gani.

Tusimwache Lisu atudanganye Kuna haja ya kuchambua haya yanayoongelewa na wanasiasa. Kesho tutachanbua Sera ya Lisu nyingine.

Hoja yangu CHADEMA naomba muwaeleweshe watanzania hiyo Bima yenu ina package gani?

Ole Mushi
0712702602
 
Lissu muongo muongo sana huyu mtu,hana sera kabaki kumlaumu Rais Magufuli mwanzomwisho.
 
Navyoo fahamu ahadi ya UCHAGUZI sio lazima itekelezeke kwa mwaka mmoja
Inaweza kuwa mchakato wa muda mrefu ila lengo kuuu likiwa nikuhakikisha Kila mtanza napata BIMA YA AFYA nazani LISU amesema na nimemsikia hapa Arusha kwamba Kila MTANZANIA atapata bima kwa gharama nafuu Tena shaba ikiwa Kila MTANZANIA kupata bima nazani nisera nzuri usikimbilie kuwaza KUSHINDWA na pia naaamini tukichukulia sera za wagombea positive itasaidia ata serekali itakayo ingia madarakani kuanagali Kama nijambo jema ikalichukua na kutekeleza watanzania tukanufaika
Hi nchi niyetu sote wazo lakujenga niletu sote

KAMA ELEIMU BURE ILIKUWA YA UPINZANI LEO INATEKELEZWA NA CCM
NA MAMBO YANENDA VIZURII

KUWA MTANZANIA WEKA TANZANIA MBELE USIBABAIKE NA VYAMA JALI SERA KWA MASILAHI YA TAIFA TUSONGE MBELE
SIASA ZA KUPINGANA KWENYE MAENDELEO ZITATURUDISHA NYUMA BADALA KWENDA MBELE
 
TUSIMWACHE LISU ATUAHIDI YASIYOWEZEKANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kwenye kampeni za Lisu ana Mambo makubwa mawili anayowaomba watanzania wamchague nayo. Moja ni malalamiko yake ya kupigwa risasi hii Kwake Ni Kama Kete ya kuwaomba watanzania wamuonee huruma aingie Ikulu. Jambo la Pili ni Sera zake anazotakiwa awashawishi nazo watanzania ili wamchague kuwa Rais.

Nilishawahi kusema kuwa hakuna siku nitambeza Lisu kwa kupigwa Kwake Risasi na Wala sintoongea nikimuona analalamika kuwa mwili wake una machuma kila Mahali. Kama watanzania wataamua kumchagua kwa kuwa tu aliwahi kushambuliwa na watu wasiojulikana Hilo nimewaachia. Mimi nitajikita kwenye Sera zake ambazo kwangu ndio kipimo Cha kutoa kura yangu kumchagua Kiongozi katika ngazi zote iwe udiwani, Ubunge, au Urais nitazipima Sera kabla ya kuchagua.

Nimesikikiza Sera za mgombea urais Lisu anayo Mambo makuu matatu anayowaahidi watanzania kubwa kabisa ni kila mtanzania kumiki bima ya Afya, kupunguza Makato ya Wanufaika wa Bodi, kuleta maendeleo ya watu badala ya vitu. Haya ndio anayoyarudia kila Mara anaposhika kipaza sauti Leo tuongele moja kesho tutaongele lingine na leo tuanze na Bima ya Afya kwa kila mtanzania.

BIMA BURE

Nimejaribu ku survey nchi nyingi duniani, Ni nchi ipi yenye uwezo wa kuwapa wananchi wake wote Bima BURE sikuona.

Marekani ilijaribu kupitia Obama Care lakini baada ya Muda mfupi walishindwa na Obama care ikafa. Sababu kubwa Ni gharama za uendeshaji. Kutokana na U.S Census Bureau taifa la Marekeni lina watu milioni 28.1 tu ya wasiokuwa na Bima. Hivyo Obama care ilidhamiria kufanya Coverage ya watu milioni 28 tu kuwalipia huduma za Afya lakini wameshindwa kutokana na gharama zake. Hili ni taifa tajiri kuliko yote duniani limeshindwa kuwalipia watu milioni 28 tu je kwa Tanzania wenye Bima hawafikii milioni kumi je milioni Arobaini iliyobakia wanaofanya kazi wataweza kuwalipia gharama hizo?

Sababu nyingine ya wamarekani kukataa Obama care ni kuwa Kama itafanya kazi Kodi ingelipanda sana nchini marekani hivyo wakaamua kuitupilia mbali. Kuna nchi zinazotajwa kuwa na unafuu wa Bima Duniania lakini sio bure naomba kuzitaja:-

1.Ujerumani.

Ujerumani ndio taifa linaloonekana Kama Bima yake angalau Ina unafuu kwa wananchi wake. Lakini pia sio wajerumani wote ambao Wana Bima ya afya. Wafanyakazi wote nchini ujerumani wanalipia Bima zao kwa kushirikiana na waajiri. Wengine waliobakia wanalipia kiasi kidogo Bima zao.

2. Singapore

Singapore wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa Medshield ambao serikali kwa asilimia kubwa ndio inabeba gharama za matibabu lakini kila mtu nchini Singapore anatakiwa alipie asilimia 10 ya kipato chako kwenye mfuko huo. Kama ni Mkulima wanakupigia mahesabu asilimia 10 ya unachokipata ulipie kwenye mfuko wa bima, Kama ni mfanyakazi vivyohivyo pamoja na kuwa unaonekaba kuwa mfumo Bora kuliko yote duniani lakini bado unalipiwa na wenye kipato kikubwa bado wanaumia sana kukatwa asilimia 10 kwa ajili ya Bima.

3. Japani

Japani wao Wana mfumo wa Bima unaoitwa SHIS mfumo huu nao watu wanatakiwa kujiandikisha na kulipia.

4. Uingereza.

Wao ndio kwa asilimia kubwa wamefanikiwa kwa kuwa hospital asilimia kubwa zinamilikiwa na serikali na wafanyakazi wote hulipwa na Serikali. Mfumo wao wa Bima wa NHS gharama zake zote hutolewa na Serikali. Ila bado una changamoto na mtu akitaka kutibiwa private ambako Kuna huduma nzuri na za haraka unatakiwa kulipia mwenyewe.

Hizo Zina unafuu Duniania Soma unafuu wake halafu tulinganishe na Tanzania.

Tanzania.

Tuna Bima ya NHIF ambayo huangaika na watumishi wa Umma na wategemezi wao. Huu tunauchangia asilimia Kama mataifa mengine yanavyouchangia. Tena asilimia tatu tu tofauti na mataifa Mengi sana Duniania.

Tuna mfuko mwingine iCHF (Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii ulio Boreshwa), huduma hii ya Bima ni kwa gharama nafuu kabisa kwa Watanzania wote katika Sekta ya Afya kwa Familia ya watu sita yaani Baba, Mama na watoto wanne kwa Tsh. 30,000/- tu kwa mwaka mzima. Una pata huduma zoote za matibabu kuanzia kituo kidogo cha Afya mpaka Hospital ya Mkoa.

Serikali Ina mpango pia wa kuleta Sheria Bungeni ya kuwataka watanzania wote kuingizwa kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

Mimi nataka kufahamu Lisu anataka kuifanyaje hiyo Bima yake. Sio kwamba nambeza la hasha nataka kufahamu Bima yake anayoihubiri Ina nini ndani na itakuwa inafanana na ya nchi gani.

Tusimwache Lisu atudanganye Kuna haja ya kuchambua haya yanayoongelewa na wanasiasa. Kesho tutachanbua Sera ya Lisu nyingine.

Hoja yangu CHADEMA naomba muwaeleweshe watanzania hiyo Bima yenu ina package gani?

Ole Mushi
0712702602
Tuliahidiwa nchi ya ahadi na asali sasa nalamba shubiri tu
 
Back
Top Bottom