Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

Uchaguzi 2020 Tusimuache Lissu atuahidi yasiyowezekana

ikabili hoja hapo juu inatekelezeka vip bila jaziba bali kisomi zaidi kwa data na uwaledi bila matusi wala dhiaka
Umesoma na kuelewa nilichoandika? Tunavyosema bima Ina kuwa na masharti yake. Hakuna bima ya 100%.Huwezi kuwa na kansa ya ubongo ukahitaji upasuaji Basi bima haitakusaidia hata use na bima ya namna gani.

Lakini kwa magonjwa haya ya kawaida na kwa ajili ya check up, bima unatumia. Chanzo Ni pesa kutoka hazina, pesa zinazokusanywa na TRA ndizo zitalipa bima.
 
CCM imeahidi ahadi hewa kibao kwa miaka 50 sasa na tumewaacha tu, ngoja tujaribu ahadi za Lissu hata kama haziwezekani

Za kwenu tumezichoka
Jamaa chizi huyo .... Hizo ahadi za CCM anazodai zinazotekelezeka sijui ni zipi? Ajira million 8, au za Million 50 kila kijiji na laptop kwa walimu!!?
 
Unataka utuletee vifurushi vya chuo au sio.?
Itabidi watz wote tuwe wanachuo..
Kwani tofauti Ni Nini? Au unadhani wanachuo wanapata faida? So kweli kwa sababu Kuna mtu Hadi mwaka unaisha hajakanyaga hospitali, akiumwa ataenda na bima kuchukua dawa ambazo Mara nyingi gharama hata elfu 5 hazifiki.
 
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa toka Lissu arudi nchini tabia ya mh Jiwe ilibadilika ghafla; akawa mpoleeeeee.

Huyu jamaa atakuwa mpole zaidi akienda Bukoba kwa Wahaya kuomba kura!! Akidhania wamesahau matusi aliyowatukana baada ya tetemeko.
 
Jamaa ana laana ya Mwenyezi Mungu. Kafanya maovu mengi sana na wengi wamemshtakia Mungu. Bomoa bomoa, kuwafukuza watu kazi, kesi fake, utekaji, utesaji na Mauaji. Sasa kila analogusa HALIFANIKIWI.
Mungu ni mlipaji...
 
MILIONI 50 KILA KIJIJI

Kwa kweli haikua lazima zitolewe awamu ya kwanza ili hali hakuna madawa, mahospitali wala vifaa tiba, hakuna madarasa wala vitabu wala barabara za kufika hivyo vijiji wala maji na nishati umeme.

Pesa zimewekwa kwenye sehemu wenye vipaumbele... na kwakua mkuu atashinda tena awamu ya pili atazitoa hizo hela na zitakua msaada mkubwa kwenye kuboresha shughuli za kiuchumi kwa vijiji
 
Lissu anatoa ahadi zinazotekelezeka sio zile za milion 50 kila kijiji au laptop kila mwalimu.

Lissu alikuaga mbunge lakini jimboni kwake sio ata pa kuongea kwa sauti ni mjini lakini hio aibu basi tu
 
Lissu sera zake anatoa hapa JF kwa washabiki wake, leo kuna mtu kaweka siku kumi za uraisi wake atafanya nini, kesho akiingia jukwaani utasikia ndio habali.

Hakuna tafiti zozote kulingana na ahadi zake

Kwamba hizo bima akishazitoa bure pesa yake itatokana na nini?

Je chanzo kipya atakitoa wapi ili hilo litimie,? je anapo punguza kodi hilo gep ataliziba na nini ili pesa ipatikane bila kuathili shughuli zingine?

Kulipa fidia pesa itatoka wapi? Anapo ongeza mishahara na itakuwa kiasi gani kwa mwezi na itakuwa kiasi gani kwa mwaka na zitatokana na nini?
 
Lisu sera zake anatoa hapa JF kwa washabiki wake, leo kuna mtu kaweka siku kumi za uraisi wake atafanya nini, kesho akiingia jukwaani utasikia ndio habali.
Hakuna tafiti zozote kulingana na ahadi zake,
Kwamba hizo bima akishazitoa bure pesa yake itatokana na nini?
Je chanzo kipya atakitoa wapi ili hilo litimie,? je anapo punguza kodi hilo gep ataliziba na nini ili pesa ipatikane bila kuathili shughuli zingine? kulipa fidia pesa itatoka wapi? Anapo ongeza mishahara na itakuwa kiasi gani kwa mwezi na itakuwa kiasi gani kwa mwaka na zitatokana na nini?

Kwani yale madege yaliyopaki na yanayokuja pesa zake au zile 1.5Tr/- zilizopotea zilitoka wapi?

Je, yule bibi wa kijijini ni lini ata feel impact ya hayo madege?

Acheni kujifanya kuwa pesa za kuliwa au za madege uchwara zipo lakini za kufanyia jamii tija hazipo.

Umeona pesa zitakako toka?
 
Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.
Noah zetu mkuu
 
Mkuu kwani mpaka sasa Tanzania inafanana na inchi gani?

Itoshe kusema, Akili yako inapoishia, yamwenzako ndio inaanzia!

Naomba hii mada tuizungumze kisomi! lengo iwe kutoa mawazo ya kuboresha utoaji wa Afya inchini kwa Kiongozi yeyote atakaye shinda uchaguzi huu!
 
Hebu twende kwa mifano...katika kipindi kifupi Bashite alikuwa RC wa Mkoa wa Dar es Salaam amechota kiasi gani hadi kumiliki mali zote alizo nazo zinazodaiwa zinafika matrilioni?

Lakini pia tujiulize matrilioni ngapi baba yake amekuwa akichota hazina katika awamu yake hii ya kwanza tu ambayo hayana kumbukumbu zozote zilivyotumika tukiacha zile anazogawa kama njugu akiwa barabarani.

Tanzania ni nchi tajiri ambayo haiwezi kushindwa kuwapa bima ya afya watu wake ila tunachokosa ni utawala bora na viongozi bora...#CCMmustGO2020
 
Hiyo millioni 50 imezaa zahanati na umeme wa REA kila kijiji..kumbuka kujiungia umeme ilikuwa 170,000 na sasa ni elf 27 tu..upewe nini?
Kwa hiyo kwenye ilani yenu hapakuwa na hizo issue za zahanati na REA?

Sasa ikawaje muahidi milioni 50 kila kijiji na laptop kwa kila mwalimu wakati hawana hata umeme wa kuzichaji hizo laptop?
 
Ahadi za TL ni sawa na ahadi za mlevi wa Konyagi, kama wameshindwa kujenga hata ofisi ya chama chao wataweza ya kuwajengea Watanzania mahitaji yao? Ruzuku ya 320+ millioni kila mwezi pamoja na michango ya wabunge wao wameshindwa kuwa na ofisi miaka zaidi ya 20 tangu hiki chama kianzishwe na baba mkwe wa mlevi wa konyagi.
Kuandika upuuzi mbele ya jamii ya watu wenye upeo ni kujidhalilisha!Unahisi umeandika cha maana lakini watu timamu tunakuona mpumbav ambaye hujapevuka!JF sio size yako,hamia facebook upeleke mipasho yako!
 
Back
Top Bottom