Hatukutafutana, kila mtu kivyake hakuna kujuana.
Japo kupitia whatsap niliziona status, mara nyingine anipige vijembe mpaka basi.
Kuna siku moja alipost nikaona dalili, kuwa tayari kashapata bwana wapili.
Sikutaka kuumiza kichwa, kwani kila siku alikuwa akipost picha.
Status ziliwekwa maneno ya nyodo, eti chini ya mnazi kaokota dodo.
Sikuwa na wivu nilimuacha atambe, alisema ana date na wasomi sio waliokimbia umande.
Mwanzo alianza kumuita class mate, na kuwa wamefaulu na kupata the same grade.
Hajui mi kwake nishafunga gate, hata anitambie vipi haniumizi head.
Akapost eti walokole wakidate, hawapaswi kuitana baby.
Akamtag na jamaa kimafumbo, akampa sifa za mambo lundo.
Siku zikapita, upepo ukabadilika.
Status sa huzuni zikaongezeka, kuonesha kwenye hilo penzi anateseka.
Zile status za kejeli zilikoma, kuonesha hata yeye namba anaisoma.