Alikuwa ni mtu wa church, hapo ndio nikajua kumpata itakuwa kazi
Nilikuwa tayari kwa lolote nimpate, miondoko yake na upole vilinifanya nidate.
Siku moja alikuwa anakatiza sokoni, nikamfata kumueleza namna alivyonikaa moyoni.
Akashangaa akauliza kwani kulikoni, unanipenda mimi kwani wengine huwaoni?
Nikamwambia mama usiwe na hofu, nakupenda wewe wengine siwaoni nimekuwa mpofu.
Basi nikamjaza maneno kumpa hope, maana nishachoka daily kutumia soap.
Akanipa namba tukaaza kuchart, kesho kutwa nikamualika club ku party.
Akasema hiyo ni dhambi mi nimeokoka, lakini dingi pia ni mkali nikisepa atafoka.
Nikamuambia we ni nguzo ukiacha nita dondoka, sitaki uwende mbali maisha ya upweke nimechoka.
Lakini haikusaidia maana aliniaga kuwa anaondoka, anaenda mkoa wa mbali kusoma.
Akaniahidi kunipa ushirikiano every day, lakini alivyosepa simu zangu akawa hapokei.
Sometimes akipokea ananikalipia, kuwa nimekuwa kero ameshindwa kunivumilia.
Nimpe muda nipunguze simu kumpigia, atanitafuta kwa muda wake yeye akisikia.
Aliambia mengi ya kuudhi, aliniambia nitafute demu mwingine sinabudi.
Masta nikasema huo ni ushenzi, vipo vya kuhangaikia ila sio mapenzi.
Nikaacha kutuma meseji, hata nikituma nikawa simuiti baby.
Kuviziana ndio ikawa mbinu, kila mmoja anamsikilizia mwenzake apige simu.
Sio siri ilikuwa ni zaidi ya mafarakano, ilipita miezi sita bila mawasiliano.