Tusimulie love story yako kwa kifupi tujifunze

Mimi kimya sema status zimefutika muda umeisha ningeuona uzi mapema ningezi screenshot mapema na kuzi attached hapo km hiyo. Noma mm wala simtafuti nasoma tu status zake. Atajijua mwenyewe. Maisha yaendeleee.
Usimfuatilie hata status zake.Akijua atapata kiburi.
 
Miaka mi3 iliyopita! Kama kawaida mida ya jioni hua naenda mazoezi (basketball), nikiwa narudi getto njiani nilijenga mazoea ya kua nampa Hi binti fulani.

Cha ajabu! I always found her in the same place & time kila siku.

Siku moja akanifuata na kunieleza kwamba ananipenda na angetamani niwe mtu wake na hata pengine mume wake. Nilishangaa sana!! ( KE kumtongoza ME!!!![emoji44])

Nilijaribu kumweleza kwamba sina hisia nae lakini hakunielewa (pengine kwa sababu mimi si mtu muongeaji). Kila nafasi aliyopata aliendelea kuniambia the same thing.

Nikaona nimkubalie tu ili pengine akigundua kwamba sina hisia nae kiivyo basi ataamua kuniacha. Baada ya hapo a lot happened mengine hua sitaki kuyakumbuka kabisa.

- Alikua ni mwanamke wa kwanza kulala nae (and it wasn't such a great experience). Baada ya kuona naathirika kisaikolojia ikabidi niamue kumwacha bila kujali hisia zake ( tokea hapo sikuwahi muona tena).

- Na tokea tumeachana 3yrs ago sijawahi kua na KE mwingine, wengi ninaokutana nao hua nawapotezea mwanzoni kabisa kabla ya mahusiano kuanza.

- Bado nina matumaini kwamba siku moja nitampata aliye sahihi zaidi, hata kama ni uzeeni.
 
naona umeamua kumlipua kabisa mwamba Leo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Weka kisa acha story kuquote watu usumbufu huo, huu uzi unatia kisa unapita hivi. Huna, soma vya wenzio inatosha.
 
Oyaaa kwa uandishi umetisha sana.
 
Nampenda ila hanikubali kivile
But nitaendelea kumpenda hivyohivyo till end of time..../

Daily mimi ndiyo wa kwanza kumtxt,
Daily mimi ndiyo wa kwanza kumcall,
Daily mimi ndiyo wa kwanza to apologize to her
But I still love her...../

Sometimes anakuwa kama vile ananielewa,
Ila sometimes kama vile kalogwa ama kavurugwa....
Sometimes analeta longolongo kuhusu familia Yao na life la kwao kiujumla and a lot of stories about herself....
But I still love her...../

Namwomba game anarefuse ,
Namwomba meeting at park anakataa,
Namwomba nimtumie hata hela ya soda or water anakataa,
But Bado naendelea kumpenda tu..../

Mapenzi mapenzi mapenzi kwann unanifanyia hivi .....
Napendwa na wadada wacute yaani wakali kinoma ila Kwa bahati mbaya sikuwahi Wala sijawahi kuwa na hisia nao...../

.ILA HUYU NJIWA MSUMBUFU AMBAYE HATAKI KUTUA KIOTANI MWANGU NDIYO AMBAYE ANAUSUMBUA MOYO NA AKILI YANGU...../

daaaaaaaah....mommy njoo bc .....

Au nikufanyie nini , mbona nikikutumia hela unakataa, vizawadi ndiyo usiseme kbs....vipi mamaa!!!

Anyway SIKOMI , SIKOMI NITAENDELEA KUKUPENDA HADI SIKU AMBAYO UPENDO WANGU KWAKO UTAISHA NA KUHAMIA KWA BINTI MWINGINE....../
 
Alikua Ni rafiki tu pia college mate then workmate tukaja kutana mtaani wakat bado naishi maskani aliniambia mpaka sasa una kazi lakin bado una ishi nyumban ondoka ukapange nikatoka home ushikaji uka endelea Kama kawa nikajikuta naanza kumuelewa maana Mara zote alikua akinishauri fanya hivi fanya vile nikaona huyu atanifaa nika mweleza langu Jambo akanielewa kwa sasa ni mke wangu na first born ana kimbiza mwezi wa4 sasa.
 
Endelea kumlia buyu
 
Wanaboa Sana watu wa hivyo. Kama mtu hauna Cha kucomment, soma then pita kimya kimya
 
Wanaboa Sana watu wa hivyo. Kama mtu hauna Cha kucomment, soma then pita kimya kimya
Ni katika kuwaelekeza tu watu sampuli hiyo.Na bila kutafakari,huwa wanadhani umeamua kuwashambulia tu.Wamejaa ubish tu.Nami nilivyo,siwaachi.Mjadala waweza kwenda kwa masihara ya hapa na pale lakini isizidi.Kila siku mtu anaandika;
-inasikitisha sana,
-acha nicheke tu,
-hawataamini,
-inafurahisha,
-and the blah blah goes on.
Hawabadiliki wala kuchangia vinavyoeleweka!Bure kabisa.
 
Nimemlia buyu kinoma. Wala siweki hata status ya kumpondea maana nilisha move on. Ila akijichanganya anakutana na bomu la NUCLEAR lingine
Endelea kumlia buyu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…