Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Alikoswa koswa kwa Risasi....Sasa tunataka akoswe koswe na Kitanzi.....
Kuficha mashahidi ni utaratibu wa nadra unaoruhusiwa tu pale ambapo mazingira ya kesi yanaonyesha wazi uwepo wa tishio la moja kwa moja kwa usalama wa shahidi au chanzo cha taarifa (source) na hata hivyo, chanzo hicho kinapaswa kuwa binafsi, kisicho rasmi na kisichopatikana kwa urahisi kupitia nyaraka za serikali.
Katika kesi ya uhaini yenye mazingira ya kesi ya TL inayomkabili mtoa kauli ya hadharani, ni jambo lisilo la kawaida kwa upande wa Jamhuri ambaye ndiye mleta mashitaka kutumia mlango wa siri kuficha mashahidi katika kesi yenye maslahi ya umma na inayohitaji uwazi wa hali ya juu.
Wakati Mahakama inapaswa kuheshimiwa, wananchi na wadau wa haki hawazuiliwi kutoa maoni au kukosoa maamuzi pale yanapodhihirika kuwa hayaendelezi haki wala hayalengi kulinda maslahi ya umma.
Ushauri wa Haraka:
1. Mawakili wa TL wakate rufaa mara moja kupinga uamuzi wa kuficha mashahidi katika kesi ya jinai inayohusisha tuhuma nzito kama uhaini, kwani hilo linadhoofisha haki ya washtakiwa kupata taarifa za mashahidi wanaowakabili.
2. Wakati rufaa ikiendelea, chama cha CHADEMA ambacho ni muathirika wa moja kwa moja kifungue shauri mahakamani chini ya hati ya dharula kuomba mchakato mzima wa uchaguzi usimame hadi pale haki za msingi za viongozi na wanachama wake ikiwa ni pamoja na uhuru wa kufanya siasa zitakapopata uamuzi wa mwisho wa mahakama.Kwani ni makosa kutoa zuio kwa chama kimoja huku vingine vikiendelea na Maandalizi.
Hili si suala la mtu mmoja. Ni suala la haki, uwazi, na mustakabali wa demokrasia yetu.
chanzo Na Mwabukusi