Tusimung'unye maneno, tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini Tanzania ni matokeo ya utawala wa Magufuli

Tusimung'unye maneno, tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini Tanzania ni matokeo ya utawala wa Magufuli

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!

Najua kuna watu huwaambii kitu kuhusu Magufuli lakini ngoja niwaambie hata kwa ubabe.

Tatizo la ajira ni global issue lakini kwa Tanzania halikupaswa kutokea sasa, lilipaswa lianze angalau 2030.

Baada ya kuingia Magufuli Ikulu na kuwa Rais cha kwanza kabisa akaenda kupambana na matajiri, aliamini kuwa matajiri ni wezi. Kila mwenye mentality ya kimaskini huamini kuwa matajiri ni wezi

Matajiri wakachakazwa haswa, watu wakapoteza ajira sekta binafsi. Serikalini nako hakuajiri. Ndani ya miaka 7 ya utawala wake ajira alizotoa ni kama zile za Kikwete ndani ya miezi 6 au mwaka.

Kwahiyo wahitimu kuanzia kidato cha 4 mpaka chuo kikuu wakajaa mtaani. Rais Samia kajitahidi kumwaga ajira kila mtu shahidi. Ushahidi uko wazi PSRS, kwenye tovuti za mashirika ya umma na wakala za serikali ambazo zimeajiri zenyewe vijana wengi. Lakini tatizo lingali bado.

Kipindi cha Magufuli hatukuona shule mpya za binafsi zikijengwa.

Kipindi cha Magufuli hatukuona vituo vya afya na zahanati za binafsi vikijengwa.

Kipindi cha Magufuli vilijengwa viwanda hewa ambavyo viliajiri vijana milioni ngapi sijui ambao ni hewa.

Enzi za Kikwete 2015 Januari nimeacha kazi ya serikali, Juni mwaka huohuo nikapata sehemu nyingine.

Enzi za Kikwete watu wengine walikuwa hawaendi kuripoti kwenye vituo na wanaomba mwaka unaofuata wanapata tena.
 
Kosa la huyo jamaa ni kukosa watu Imara wa kumshauri .

Alikuwa ni low thinker yeye pamoja na genge lake

Kitendo cha kuua sector binafsi ,Biashara nyingi kufungwa n.k hii ilionesha hajitambui na hana mikakati bora ya kuinua uchumi wa nchi

Miundombinu inapokuepo inaleta tija na thamani endapo ukiwa umeimarisha uchumi wa MTU mmoja mmoja kwanza.

Sema kipindi chake kimeacha mazuri mengi Sana pia .
 
Pamoja na kwamba Magufuli alikuwa sio mtu aliyefaa kabisa kushika wadhifa mkubwa kama wa urais lakini tatizo kubwa la nchi hii ni kuwa na mfumo mbovu sana wa kiutawala unaokiwezesha chama tawala kuendelea kutawala hata pale kinapokuwa kimekosa kabisa uungwaji mkono wa wananchi waliowengi.

Ukitizama hata kwenye uchaguzi wa juzi wa serikali za mitaa, utaona jinsi wananchi wengi walivyokosa kabisa hamu ya kupiga kura voter apathy na kufanya serikali ibaki kutoa takwimu za uongo kabisa kwa kuzidisha idadi hewa ya watu waliojitokeza kwenda kupiga kura.

Kwenye uchaguzi huo inasemekana idadi kamili ya watu waliojitokeza kwenda kupiga kura haikuzidi milioni sita kwa nchi nzima kati ya watu zaidi ya milioni 30 wenye sifa ya kuweza kupiga kura...!!!

Kwa hivyo shida sio akina Magufuli, Kikwete au Samia bali shida ni hicho chama wanachokitumia pamoja na mfumo mbovu waliouweka.
 
Hello!
Najua kuna watu huwaambii kitu kuhusu Magufuli lakini ngoja niwaambie hata kwa ubabe...
jiwe aliharibu sana ustaarabu na maisha ya watanzania, wanaompa sifa nyingi ni masikini waliokuwa wanatamani matajiri wafilisike ili watu wafanane.

kitu cha ajabu sana. kabla yake, kikwete ilikuwa ukimaliza chuo unapata kazi, ila alivyoingia jiwe kuna watu walimaliza chuo hadi leo hii hawajapata ajira. angekuwa hai tungemuuliza anajisikiaje. however, alikuwa na strength kadhaa kuliko huyu bibi, asingeweza kuuza nchi kwa waarabu na adan namna hiil hapo ndio tunamkumbuka, angeshafukuza mwarabu kitambo.
 
Yule jamaa ange tunyonya hadi damu
alitamka kabisa, kwamba anataka watanzania waishi kama mashetani, hadi waone sh.500 ni kama alfu kumi. hivi ni kiongozi gani anaweza kudhamiria wananchi wake wapata maumivu kama hayo, na kweli kipindi chake pesa ilipotea, kama alivyosema na watuw aliteseka na wengine biashara zilikufa nao wakafa kwa pressure. tundu lisu huwa anaitwa "lile dubwasha".
 
Kosa la huyo jamaa ni kukosa watu Imara wa kumshauri .

Alikuwa ni low thinker yeye pamoja na genge lake

Kitendo cha kuua sector binafsi ,Biashara nyingi kufungwa n.k hii ilionesha hajitambui na hana mikakati bora ya kuinua uchumi wa nchi

Miundombinu inapokuepo inaleta tija na thamani endapo ukiwa umeimarisha uchumi wa MTU mmoja mmoja kwanza.

Sema kipindi chake kimeacha mazuri mengi Sana pia .
Ethiopia ina miundombinu mikubwa na shirika la ndege kubwa Africa. Lakini kila kukicha Raia wake wanakamatwa wakikimbilia Afrika kusini akili kumkichwa.
 
Hello!
Najua kuna watu huwaambii kitu kuhusu Magufuli lakini ngoja niwaambie hata kwa ubabe.
Tatizo la ajira ni global issue lakini kwa Tanzania halikupaswa kutokea sasa, lilipaswa lianze angalau 2030.
Baada ya kuingia Magufuli Ikulu na kuwa Rais cha kwanza kabisa akaenda kupambana na matajiri, aliamini kuwa matajiri ni wezi. Kila mwenye mentality ya kimaskini huamini kuwa matajiri ni wezi .
Matajiri wakachakazwa haswa, watu wakapoteza ajira sekta binafsi. Serikalini nako hakuajiri. Ndani ya miaka 7 ya utawala wake ajira alizotoa ni kama zile za Kikwete ndani ya miezi 6 au mwaka.
Kwahiyo wahitimu kuanzia kidato cha 4 mpaka chuo kikuu wakajaa mtaani. Rais Samia kajitahidi kumwaga ajira kila mtu shahidi. Ushahidi uko wazi PSRS, kwenye tovuti za mashirika ya umma na wakala za serikali ambazo zimeajiri zenyewe vijana wengi. Lakini tatizo lingali bado.
Kipindi cha Magufuli hatukuona shule mpya za binafsi zikijengwa.
Kipindi cha Magufuli hatukuona vituo vya afya na zahanati za binafsi vikijengwa.
Kipindi cha Magufuli vilijengwa viwanda hewa ambavyo viliajiri vijana milioni ngapi sijui ambao ni hewa.
Enzi za Kikwete 2015 Januari nimeacha kazi ya serikali, Juni mwaka huohuo nikapata sehemu nyingine.
Enzi za Kikwete watu wengine walikuwa hawaendi kuripoti kwenye vituo na wanaomba mwaka unaofuata wanapata tena.
Mkuu mbona watu wengi sana wamepata ajira kipindi cha Magu?

Wewe na wenzio hamna ajira sababu ya incompetence wala sio Magufuli. Wenzio wanaitwa interview wanafanya vizuri sana wanapata ajira wewe unamlaumu Magufuli mpaka leo wewe ulienda interview gani ukafaulu? Alikuzuia Magufuli?

Jamani tuwe wakweli watu walio smart wanapata ajira na wanabadilsha kama chupi. Kuna watu toka yupo JK wanaangaika na ajira kazi kulaumu tu mbona wengine wanapata jamani mjifunze kuandika cv na cover letter, muwe mahiri kwenye masomo yenu mjifunze ujuzi English pia inawaangusha sana wala sio Magufuli anauzia wewe kuongea English nzuri ukaeleweka kwenye interview.

Sasa Magufuli amekufa lini mpaka leo huna ajira na Samia ataondoka atakuacha unalalmika
 
Ethiopia ina miundombinu mikubwa na shirika la ndege kubwa Africa. Lakini kila kukicha Raia wake wanakamatwa wakikimbilia Afrika kusini akili kumkichwa.
ethiopia kuna vita upande ule wa tigrey, pia, nje ya nchi kuna waethiopia wengi sana wamefanikiwa, hao jamaa wapo vizuri sana kwenye maduka na mikahawa, hivyo wakifanikiwa kutoroka kufika huko south, na baadaye ulaya na america, huwa wanafikia kwa jamaa zao waliotangulia, na wanasaidiana kutafuta maisha. hao wanaokamatwa tanzania usijefikiri ni maskini sana, kutoka ethiopia hadi south unawezashangaa ametumia milion 5, hiyo sio hela ndogo kwa mwafrika, hivyo usione wanapita na marori hapa ukafikiri ni maskini saana, hapana, ni kama hawa wabongo wanaojiita midle class tu.

utamaduni wa kukimbila nchi nyingine kutafuta maisha haimaanishi nchini kwako kuna shida saana, angalia Nigeria, angalia south america wanavyokimbilia marekani hadi trump anajenga ukuta, wanatafuta maisha. watanzania ni mbumbumbu wanaamini maisha yapo hapa tu, huu ugumu wa kupata pesa ulipo bongo usifikiri nchi zingine zenye viongozi wenye akili kuna ugumu kama huu. kuna nchi zilishatengeneza miundombinu na fursa ukifika tu mwaka mrefu umeshasimama na unapata pesa ndefu kuliko ungepata hapa na unaanza kutuma nyumbani kujenga na kusaidia ndugu zako. na south africa ni njia tu kwa sababu pale wakikukamata unapata asylum, wana uzungu fulani wa kuheshimu haki za binadamu sio kama hapa bongo wanafungwa wakati wanapita tu hata hawana haja kukimbilia hapa bongo. onyesha muethiopia mmoja tu aliyezamia bongo, hakuna, wanapita tu hapa.

kwa waliowahi kusafiri, ukikutana na wasomali popote pale, utaamini kuondoka somalia kwenda huko kumewasaidia, wana maduka makubwa, mahoteli, mikahawa, na biashara kubwa, kwa sababu nchi hizo zingine watu hawafanyi kazi kwa bidii kama sisi, hapa unasota kwa jasho na hupati pesa, jasho hili unatumia hapa bongo ukienda kulitumia nchi zenye fursa unatajirika mapema.
 
Back
Top Bottom