Tusio na adui wa kudumu tunasimama na Dkt. Slaa

Lugha hizi ndizo tunazozielewa:

View attachment 2739972

Hizi ndiyo zile lugha za watu zikiitwa lugha za Mungu. Beberu akiziita:

"Languages of the people."

Hizi humfanya adui macho kumtoka mithili ya mjusi alobanwa na mlango.

Kwamba ni mpigania haki? Mzalendo? Mwenye kukerwa na ghiliba za majizi?

"Ushindwe vipi kumwelewa Dkt. Slaa?"

Kwamba Dkt. Slaa aliwahi kutukosea? So what? Hatuhitaji malaika hapa!

Kwao wote waliowahi kutikosea au ambao hawakuwahi kutukosea: muhimu kwetu ni nini wanafanya au kusema sasa.

"Malaika maisha ya duniani si yao. Hata Messiah hakuja Kwa wenye haki."

Bravo: Dkt. Slaa, Dkt. Nshala, Mwabukusi, Kamanda Mdude na wa namna hiyo.

Mlipo tupo!

Ninakazia:

Dhidi ya ma CCM hatuna rafiki wala adui wa kudumu ila agenda na malengo!
Hoja imeungwa mkono hiyo......Yaliyopita si ndwele, Tugange yajayo.
 
Kitu chochote kama kinaongelewa au hakijawa hubaki kuwa hisia, hata kama kuna tulioona lakini tunaamua kukiongea lakini bila kukitolea maelezo or proif, bado kitabaki hisia.
hivyo upo sahihi, mimi pia nipo sahihi. Subiri wakati ukifika itakapojidhihirisha ndipo ufanye maamuzi, wakati mimi sina cha kusubiri sababu nipo mbele ya wakati.
Kama unakiri nipo sahihi, nawe unashindwa kuweka uthibitisho wa kile unachotetea ili uonekane upo sahihi kwa hoja yako, ni vyema kwa sasa ukiri tu upo wrong, wala usilete kisingizio cha upo mbele ya wakati kisicho na ushahidi, hiyo kwangu ni janja janja tu, sawa na kupiga ramli.
 
Dr. Slaa ndiye ameandaliwa kwenye hicho Chama, na wanachofanya ni ku test mitambo kwa kwa kumuandalia matamko ya kutoa huku wakijifanya kumsumbuasumbua, lengo lao ni kumpatia airtime ili Chama hicho kiweze kupata muitikio na mapokeo.
Bahati mbaya kila wakipima u0epo wanaona hiyo project yao wanayoifanya na Dr. Slaa inaenda kuishia kuwa another Project of Zitto Kabwe like, yaani itabuma tu.
Hata wenyewe wamreona hasara sababu wameishia kuwa na wapinzani aina ya Dovutwa, Shibuda, Zitto Kabwe, Mbatia, Cheyo n.k. Wanaishia kuwalipa for nothing huku kazi kubwa wakiifanya system wenyewe, na watu zama hizi wakishanusa mtu hafai wanamuacha kama alivyom
Uko sahihi, huu mpango wa kuanzisha chama kipya cha upinzani dhidi ya CDM ilishika kasi wakati wa Magufuli, nadhani mazingira yakawa hayafai. Ila huu mpango bado upo, na lengo ni kuanzisha upinzani utakaofanya siasa zitakazoratibiwa na CCM. Ni vizuri kuwa makini na watu walioonyesha kuwa upande wa CCM hata kwa bahati mbaya. Sina imani na Slaa ama Mbatia, hata kama kwa sasa wanaongea lugha za kipinzani.l
 
Kitu chochote kama kinaongelewa au hakijawa hubaki kuwa hisia, hata kama kuna tulioona lakini tunaamua kukiongea lakini bila kukitolea maelezo or proif, bado kitabaki hisia.
hivyo upo sahihi, mimi pia nipo sahihi. Subiri wakati ukifika itakapojidhihirisha ndipo ufanye maamuzi, wakati mimi sina cha kusubiri sababu nipo mbele ya wakati.

Nakuunga mkono kwenye hoja hii. Hii michezo tumekuwa tukichezewa na CC/system kila mara na kuishia kujaa kama mazoba. Kuna uzi uliletwa humu na 2018 kuhusu kuanzishwa chama kipya cha upinzani. Na uzi kama huo huo ukaletwa tena 2021 na 2022 ukielezea ujio wa chama hicho kipya kuelekea uchaguzi wa 2025.

Mwanzoni hii project alipewa Zito wakati wa JK na ACT yake. Lakini alipoingia Magufuli akatupilia mbali maana hakuwa anakubaliana na mipango ya kina JK, na alikuwa hampendi Zito. Kisha Zito alipojiunga na Seif ikawa ngumu zaidi kwa project hiyo. Kwa sasa Slaa na Mbatia wanaweza kuwa kete ya chama hicho cha kimkakati.
 
Uko sahihi, huu mpango wa kuanzisha chama kipya cha upinzani dhidi ya CDM ilishika kasi wakati wa Magufuli, nadhani mazingira yakawa hayafai. Ila huu mpango bado upo, na lengo ni kuanzisha upinzani utakaofanya siasa zitakazoratibiwa na CCM. Ni vizuri kuwa makini na watu walioonyesha kuwa upande wa CCM hata kwa bahati mbaya. Sina imani na Slaa ama Mbatia, hata kama kwa sasa wanaongea lugha za kipinzani.l
Hizi ni hisia au niziite ndoto ndio maana unakiri kuna wakati huwa zinayeyuka. Hiki kizazi cha sasa hata CCM wenyewe wanajua hawawezi kukichezea michezo hiyo, Zitto na ACT yake wamewapa fundisho hilo.
 
Lugha hizi ndizo tunazozielewa:

View attachment 2739972

Hizi ndiyo zile lugha za watu zikiitwa lugha za Mungu. Beberu akiziita:

"Languages of the people."

Hizi humfanya adui macho kumtoka mithili ya mjusi alobanwa na mlango.

Kwamba ni mpigania haki? Mzalendo? Mwenye kukerwa na ghiliba za majizi?

"Ushindwe vipi kumwelewa Dkt. Slaa?"

Kwamba Dkt. Slaa aliwahi kutukosea? So what? Hatuhitaji malaika hapa!

Kwao wote waliowahi kutikosea au ambao hawakuwahi kutukosea: muhimu kwetu ni nini wanafanya au kusema sasa.

"Malaika maisha ya duniani si yao. Hata Messiah hakuja Kwa wenye haki."

Bravo: Dkt. Slaa, Dkt. Nshala, Mwabukusi, Kamanda Mdude na wa namna hiyo.

Mlipo tupo!

Ninakazia:

Dhidi ya ma CCM hatuna rafiki wala adui wa kudumu ila agenda na malengo!
Hata kama ningekuwa sijawahi kumsikia huyu Dr Slaa ni nani, nikawekewa tu hii video mbele yangu kusikiliza anayosema ndani ya video hiyo katika muda huo mfupi...; ninaungana naye kwa mia moja.
Nchi hii imefikia hapa ilipofikia katika ubovu chini ya CCM, kwa ujinga wa kumwona rais kuwa kama yeye ndiye kila kitu.

Sasa watu wameanza kukataa upumbavu huu.
Na hasa anapotokea rais wa hovyo kabisa, asiyejua chochote, anaendeshwa tu na mafisadi yanayomzunguka, yakimtumia tu kama kifaa chao cha maangamizi kwa wengine.
Nchi haiwezi kwenda namna hiyo. Ni lazima watu wakatae, na huku kukataa ndiko kunakoonyeshwa na hawa akina Slaa.
Nami naungana nao moja kwa moja.

Hatuwezi kuishi ndani ya nchi yetu kwa hisani tu ya mtu mmoja, anayeitwa Rais, halafu mtu huyo huyo anatumiwa na genge la majambazi.
 
Nakuunga mkono kwenye hoja hii. Hii michezo tumekuwa tukichezewa na CC/system kila mara na kuishia kujaa kama mazoba. Kuna uzi uliletwa humu na 2018 kuhusu kuanzishwa chama kipya cha upinzani. Na uzi kama huo huo ukaletwa tena 2021 na 2022 ukielezea ujio wa chama hicho kipya kuelekea uchaguzi wa 2025.

Mwanzoni hii project alipewa Zito wakati wa JK na ACT yake. Lakini alipoingia Magufuli akatupilia mbali maana hakuwa anakubaliana na mipango ya kina JK, na alikuwa hampendi Zito. Kisha Zito alipojiunga na Seif ikawa ngumu zaidi kwa project hiyo. Kwa sasa Slaa na Mbatia wanaweza kuwa kete ya chama hicho cha kimkakati.
Hapa kwanza mkumbuke Dr. Slaa mnayemzungumzia mpaka sasa anadai hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote cha siasa, hivyo sioni sababu ya kufuata hisia zenu, na kuyapuuza maneno ya mhusika, kwa sasa akili zielekezwe kwenye ku fight our common enemy, lakini sio hii kazi mnayojipa ya kuogopa vivuli vya watu.
 
Mmawia wewe na wenzio mko wangapi?
 
Sijajua maudhui halisi ya andiko hili, lakini nimependa ulivyo toa mfano na historia ya ulaghai unaofanyika chini ya CCM.
Hii nimeipenda sana.

Haya yanayofanywa na Slaa, na sijui huyo Mbatia (nina matatizo sana na huyu Mbatia siku hizi, kwa sababu haeleweki, kama nilivyoshindwa kumwelewa vizuri Zitto).
Sasa kama haya wanayoyasimamia akina Slaa ndani ya kundi hilo, ni aina ya mpango wa CCM (huenda hapa ndipo sijaelewa vizuri maudhui ya hoja); mimi ningechukua tu hiyo ajenda yao na kuikabidhi kwa watu wanaoeleweka waisukume mbele, halafu tuone CCM watakuja na mbinu zipi baada ya hapo.
 
Nakuunga mkono kwenye hoja hii. Hii michezo tumekuwa tukichezewa na CC/system kila mara na kuishia kujaa kama mazoba. Kuna uzi uliletwa humu na 2018 kuhusu kuanzishwa chama kipya cha upinzani. Na uzi kama huo huo ukaletwa tena 2021 na 2022 ukielezea ujio wa chama hicho kipya kuelekea uchaguzi wa 2025.

Mwanzoni hii project alipewa Zito wakati wa JK na ACT yake. Lakini alipoingia Magufuli akatupilia mbali maana hakuwa anakubaliana na mipango ya kina JK, na alikuwa hampendi Zito. Kisha Zito alipojiunga na Seif ikawa ngumu zaidi kwa project hiyo. Kwa sasa Slaa na Mbatia wanaweza kuwa kete ya chama hicho cha kimkakati.

Chuki yako kwa Slaa kama mtu au maneno anayosema hapa?

Kulikoni kutokujikita na anachosema Slaa hapa utuomyeshe wapi pana tatizo?
 
Hapa kwanza mkumbuke Dr. Slaa mnayemzungumzia mpaka sasa anadai hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote cha siasa, hivyo sioni sababu ya kufuata hisia zenu, na kuyapuuza maneno ya mhusika, kwa sasa akili zielekezwe kwenye ku fight our common enemy, lakini sio hii kazi mnayojipa ya kuogopa vivuli vya watu.
Precisely
 
Tunamtaja Mbowe kwa sababu yeye ndiye mwenyekiti wa Chadema aliyepokea fedha za Lowassa na kumkaribisha agombee uraisi kwa tiketi ya Chadema.

Na hilo likawa chimbuko la Dk Slaa kujiondoa Chadema sababu alitamka wazi kwamba hawezi kutumika kama Dodoki ili kumsafisha Lowassa ambaye alikwisha chafuka toka kwenye list of Shame pale mwembeyanga.

RICHMOND.

Usijitowe ufahamu kwa kuuliza jambo ambalo linajulikana na kila mtanzania.

Hakuna ufahamu kwenye lolote uliloandika hapa.

Bottom line:

Akitokea shetani anaongea anayoyaongea Slaa Leo, tutamwunga mkono.

Akatokea malaika anayapinga, tutamtupia vilago.

Umenisoma ndugu?
 
Sijaelewa unachoniuliza mkuu 'Brazaj'? Hebu fafanua vizuri nielewe unacholenga hapa.

Hapo nimewakaribisha vijana wasiompenda Slaa kwa sura bila hoja watueleze wao waliko wako wangapi?

Tuko pamoja mkuu. Slaa tuko naye Kwa hoja zake SI sura.
 
Nakuunga mkono kwenye hoja hii. Hii michezo tumekuwa tukichezewa na CC/system kila mara na kuishia kujaa kama mazoba. Kuna uzi uliletwa humu na 2018 kuhusu kuanzishwa chama kipya cha upinzani. Na uzi kama huo huo ukaletwa tena 2021 na 2022 ukielezea ujio wa chama hicho kipya kuelekea uchaguzi wa 2025.

Mwanzoni hii project alipewa Zito wakati wa JK na ACT yake. Lakini alipoingia Magufuli akatupilia mbali maana hakuwa anakubaliana na mipango ya kina JK, na alikuwa hampendi Zito. Kisha Zito alipojiunga na Seif ikawa ngumu zaidi kwa project hiyo. Kwa sasa Slaa na Mbatia wanaweza kuwa kete ya chama hicho cha kimkakati.

Mawazo duni kabisa. Kwa ushahidi upi umeandika haya?

Hudhani kuepukana na hadithi za CCM hIzo zenye kutaka mno kutugawa karata yetu ya turufu ingekuwa kutokuwa na rafiki au adui wa kudumu bali agenda?

Ka ndivyo huoni kuwa safari yetu ya ukombozi ingekuwa endelevu?

Kwani Samia, Majaliwa, Kabudi au hata CCM wakiikana IGA wakaona umuhimu wa katiba mpya sasa, wewe hautawaunga mkono?
 
Mwenye Klipu ya huyu babu wakati amehongwa ubalozi na alipoulizwa juu ya haja ya kuwa na katiba mpya na akajibu kuwa Katiba mpya sio muhimu atuwekee hapa.
Yaani huyu Mzee baada ya kutoswa ubalozi ndo anaropla maneno yote haya😃. Cha kufurahisha CHADEMA wameshamshtukia hivyo issue ya IGA na katiba mpya ndo ameona njia yake ya kutokea

Ninakazia:

Hakuna rafiki au adui wa kudumu kwenye siasa Bali agenda.

Samia, Majaliwa, Msukuma na hata CCM ikipinga IGA tutaiunga mkono. Wakitambua katiba mpya ni sasa tutawaunga mkono.

LIssu, Mbowe na wote wakighairi hayo tunawatupia vilago.

Yaliyopita si ndwele!
 
Naunga mkono hoja 100%.

Nape alitamba 2015 kuwa atakanyaga haki zetu za kuchagua kwa kufunga bao la mkono. Lkn alipoonewa na kutishiwa bastola na jiwe tuliungana naye.

Kwann asiwe Dr. Slaa??

kuna hizi mbuzi zikikuelewa nistue mkuu. Nimekaa pale!
 
Hapa kwanza mkumbuke Dr. Slaa mnayemzungumzia mpaka sasa anadai hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote cha siasa, hivyo sioni sababu ya kufuata hisia zenu, na kuyapuuza maneno ya mhusika, kwa sasa akili zielekezwe kwenye ku fight our common enemy, lakini sio hii kazi mnayojipa ya kuogopa vivuli vya watu.
Sipingi anachosimamia Slaa kwa sasa, bali sina ina imani naye. Na lazima niwe na tahadhari na ujio wa chama kipya kitakachoratibiwa na system. Kama Slaa aliweza kuwa upande huo, na Mbatia kwenye uchaguzi wa 2020, kwanini nisiwe na tahadhari?

Labda unionyeshe ni wapi napinga anachosimamia Slaa sasa, lakini ni haki yangu kuwa na tahadhari maana mashaka yangu yana ushahidi wa huko nyuma.
 
Kamwe Slaa hawezi kuaminiwa na wana mageuzi( siasa za upinzani)
 
Chuki yako kwa Slaa kama mtu au maneno anayosema hapa?

Kulikoni kutokujikita na anachosema Slaa hapa utuomyeshe wapi pana tatizo?
Sina chuki na Slaa, acha upotoshaji usio na sababu, na mimi ni baadhi ya wafuasi wa upinzani tuliounga mkono uamuzi wa Slaa kutokubali Lowassa kupewa nafasi ya kugombea urais ndani ya CDM, kwani Lowassa hakuwa msafi. Ila nilitatizika na msimamo wa Slaa pindi Magufuli alipokuwa akiwafanyia ndivyo sivyo wapinzani. Na sina popote ninapopinga msimamo wake wa sasa, ila sina imani naye. Je ni lazima niwe na imani na Slaa?
 
Back
Top Bottom