Tusio na magari tukutane hapa

Tusio na magari tukutane hapa

Huu ndio ukweli mchungu sana ambao watu wengi wenye magari hawapendi kuusema na hawatausema mbele ya watu wasiokuwa na magari.

1/Kununua gari kumewapelekea kwenye madeni kutoka kwenye taasisi za kipesa. Walikuwa hawajawahi kukopa benki lakini kupitia gari walikopa. Na mikopo hiyo ni ya muda mrefu na yenye riba.

2/Gari limepelekea utumwa wa matumizi ya Pesa ili kulihudumia hilo gari au kwenda sambamba na maisha ya kumiliki gari. Gharama za maisha kwao zimekuwa juu wakati huo huo kipato chao ni kile kile au kimepungua.

3/Furaha na Amani ya kumiliki gari ni kidogo sana tofauti kabisa na mategemeo na matazamio yao kabla ya kumiliki hilo gari au mapema wakati ndio wameanza kulimiliki. Kiufupi gari limeleta karaha pia katika maisha yao.

4/Wengi wanajuta kimoyomoyo kuhusu maamuzi ya kununua gari wakati walipaswa kufanya baadhi ya mambo mengine kwanza au aina ya gari walioamua kuimiliki haikuwa sahihi kwao.

5/Kumiliki kwao gari hakukuwafanya kujisikia kupata utoshelevu bali kumeongeza uhitaji wa kutaka kumiliki gari tofauti na hilo au kumeleta unyonge fulani mbele ya watu wengine wenye magari mazuri na bora zaidi yao.
Daaah!! chief umesema yote aisee...[emoji23][emoji23]
 
Wale wote tusio na magari ya kutembelea hapa mjini na mikoani tukutane hapa!

Tuelezane changamoto na faida tuzipatazo tunapotumia public transport hususani daladala

Kwangu mimi kero ni kujazana kwenye basi kama ngombe zizini pia kugombania chansi hasa mida ya jioni na asubuhi kwa wakazi wa gomz, mbagala, mbezi mwisho hii wanaielewa vizuri
lakini pia dharau hapa mjini kwa sisi tusio na gari zimezidi, watoto wengi wa kishua tunawasikia tu



Faida niipatayo ni kukutana na totoz za maana kwenye gari yaani full changanyiko
Pia gharama ndogo hata huwa sioni haja ya kupanda bajaji au bodaboda

Karibuni
Hii inaitwaga kambaja nani[emoji28]
 
Back
Top Bottom