Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, Mwl. Nyerere hakuwa mwanademokrasia!

Watanzania tuache Unafiki.
Nchi za Wenzetu huwa wana Legacy zao.
Nyerere alijitahidi sana Kutuunganisha waTanzania. Nyerere angefuata mfumo wa Kikoloni ni wachache sana wangemudu Elimu. Wakati wa Mkoloni elimu ilikua ni Gharama sana. Kumbuka Missionaries schools.
Kila Binadamu ana mapungufu yake ila Kumbuka Nyerere Hakujilimbikizia Mali.
Nenda Butiama angalia Nyumba aliyojenga Mwalimu unaweza ukalia.
Mwalimu alisaidia nchi za kusini mwa Afrika kuweza kujitawala mfano Msumbiji, South Africa, Zimbabwe, Zambia.
Taifa lazima liwe na Legacy mfano
1. India - Gadhi
2. US- Linkolin
3. China- Mao
Kama kuna mapungufu ya Mwalimu hakuna haja ya Kuya Publisize!!!
 
Ni kweli bali apenda haki aliheshimu utu.
 

Ukiulizwa tetea kuwa Nyerere alikuwa Mwana Demokrasia jibu lake ndio hilo kuwa tuangalie nyumba yake Butiama?
 
Nyerere mzuri ni yule aliyekufa sio yule aliyekuwa hai.

Hii kauli yako inazo maana mbili, ya kwanza ni; Nyerere anaonekana mzuri kipindi hiki ambapo ni marehemu lakini alipokuwa hai hakuonekana mzuri, maana ya pili ni kwamba kipindi alipokuwa hai alikuwa mbaya na kipindi hiki kafariki kaondoka na ubaya wake na katuacha salama.

Hii ni sawa na kauli ya Mugabe aliposema; "A dead white man is a good one". 🤣
 
K

Kabla ya kuhitimisha, ungetuelezea Mwl. Ambavyo hakuwa mdemokrasia kama ulivyo andika kwenye kichwa cha habari.
Maandiko yangu yamebainisha hitimisho unalolitaka kama utayasoma na kuyaelewa vizuri huku ukiangalia rejea ambazo nimezitoa.
 
Mkuu;
Kwa hiyo hilo la kufanya kwa interest za nchini ndilo linamfanya awe mwanademokrasia?
 
Mkuu;
Hoja yangu sio kufanya ulinganisho na waliomtangilia au waliokuja baada yake bali ni kuchambua maisha ya Mwl. Nyerere kama kiongozi anayedaiwa ni mwanademokrasia.
 
Mkuu;
Kosa kwa nani? Sisi sawa kwa nani?

Huenda leo umegundua kwamba umekaa upande wa unafiki kwa muda mrefu na umegundua hiyo hali hailipi. Asubuhi umezungumzia wazi wazi kuhusu rushwa ndani ya ccm. Kisha ukatoa angalizo kabisa la huo mchezo kwani unajua hatari kama taifa tunayotenda kukutana nayo kwa kufumbia macho tatizo la dhahiri la rushwa. Huyo Nyerere kila siku anayesifiwa huwa tunasema alikuwa na mapungufu kibao, ila kwa sasa amegeuzwa mtaji wa kisiasa, na yoyote atakayeweka mapungufu yake wazi anaonekana kama ni kumtusi Nyerere.

Ni hivi, sisi wengine tumebaki upande wa kusema ukweli wa upande wa pili bila kusifia lolote maana tunaona kundi la wanaosifia kinafiki linazidi kukua kwa kasi ya ajabu. Ukweli ni kuwa kiwango cha unafiki kimekuwa kikubwa mpaka kukosoa kumegeuka ni uhaini. Watu wanaona mapungufu ya wazi lakini hawathubutu kuongea, matokeo yake tunajenga taifa la wanafiki huku kila mtu akiona ukweli na kuufumbia macho. Ni vizuri mliokua kwenye list ya kusifia kila kitu mmeamua kutumia akili zenu.
 
"hili ni kundi la vijana ambalo kwa sasa lina watoto wenye umri wa miaka 11 kisheria kwa sababu umri wa kuanza kufanya mapenzi nchini ni miaka 18"
==============
Hivi kunasheria inayozuia raia kufanya mapenzi kabla ya miaka kumi na nane.? [emoji848][emoji848]
 
Msingi wa mawazo yangu uliyo quote ilikuwa ni kupinga kuwa Lissu hana unafiki.

Ni kweli kwenye kujadili maisha ya Mwl. Nyerere kama kiongozi anaweza asijadili kwa unafiki lakini hii haiondoi ukweli kuwa hata yeye ni mnafiki kama wanasiasa wote nchini.

Lissu anachofanya ni kuchagua wapi asionyeshe unafiki na wapi aonyeshe unafiki kwa faida ya kisiasa.
 
Naomba tumuangalia Nyerere kwa 360- degree view.
Tukumbuke Tanzania ilifuata mfumo wa ki Socialism. Mfumo huo najua unaeleweka!!!
Lakini Tukumbuke Nyerere baada ya Kura za maoni Alikubaliana na maoni ya wachache. Minority consideration regardeless of Majority!! Kuna Demokrasia kubwa zaidi ya hii hapa Duniani aliifanya Mwalimu???
Mwalimu alikua International figure tukumbuke kutokana na Mchango wake kwa nchi za Afrika.
 
Baadhi ya Viongozi hapa duniani walio iheshimu Tanzania.
 

Attachments

  • images (9).jpeg
    8.2 KB · Views: 6
  • images (10).jpeg
    17 KB · Views: 7
  • images (11).jpeg
    29.1 KB · Views: 5
Walio mpenda milioni 9, waliotaka kumuondoa 37 tu. Tafakari. Na mara zote walishidwa!

..ilibakia kidogo waTz tuanze kula NYASI.

..na kungekuwa na uhuru wa kisiasa, au wenye mawazo mbadala wangepewa nafasi ya kuzungumza na wananchi, nadhani nchi ingechukua muelekeo tofauti.
 
Mkuu;
Kwa hiyo hilo la kufanya kwa interest za nchini ndilo linamfanya awe mwanademokrasia?

Nimeongea kiujumla na sikuongelea katika mantiki yako pekee. Kingine unapoipima demokrasia yapaswa kujua Demokrasia ni nini na yeye kama Nyerere wakati anakabidhiwa nchi ni mfumo gani wa kidemokrasia aliuona ni sahihi kwa nchi yetu. Kumbuka mfumo wowote hutumika kutokana na mahitaji ya nchi husika na ndio maana utashangaa hata mfumo wa vyama vingi tulionao leo ulipingwa kwa kura za maoni lakini Nyerere aliupitisha kwa kuangalia mantiki ya MINORITY (ingawa ukisoma historia kuna influence kutoka nje)..

Nyerere alikuwa Nyerere kwa Era yake, makosa yake ni muhimu kuwa highlighted kama unavyosema lakini pia tukumbuke forces behind kufanya aliyoyafanya mfano Sera za ujamaa pamoja na threat za mataifa makubwa kipindi cha vita baridi.
 
Mkuu;
Hoja yangu sio kufanya ulinganisho na waliomtangilia au waliokuja baada yake bali ni kuchambua maisha ya Mwl. Nyerere kama kiongozi anayedaiwa ni mwanademokrasia.
Ni vyema aachwe apumzike, huu upuuzi unaoukomalia hauna manufaa kwako au kwa yeyote yule, mana hayupo na hatokuja kuwepo.

Kuicha nchi kwa hiyar yake ni demokrasia tosha, kupigania vyama vingi ni demokrasia tosha... Mengine yalikuwa ni faida kwa nchi.

Watu masikini, elimu hawana, ni vipi angelikubali kila mtu aje na anayotaka, tena kwa nchi changa wakati huo?

Kipindi hicho kila mwenye elimu alitaka madaraka makubwa na alitaka asikilizwe. Angeruhusu leo ungeadika upuuzi huu na kuushupalia?

Nyerere mzuri ni aliekufa, alipokuwa hai alikuwa mbaya....

Ni kama leo tu, Magufuli mbaya ingali yu hai, akifa anabaki kuwa mzuri.

Umekomalia Nyerere, Nyerere, wataka mfundisha nani udikteta wake?
 

Ww hasa ndio walengwa wa huu uzi, nyie ndio msiojua matusi na ukweli, kiasi kwamba upande wa pili wa kiongozi unapowekwa hadharani mnakuja na upotoshaji ionekane ametukanwa. Aina yako ya watu ndio wako mbele na viongozi wa nchi hii mnaotumia kichaka cha kutukanwa ili kufunika ukweli.
 
Ni ukweli mtupu maana hata hao wanaowadai vijana huo mkopo wao walisoma bure. Chakushangaza huo mkopo kila siku interested ina panda na usipo angalia kama umechukua huo mkopo utalipa maisha yako yote. Yaani itakuwa inafanyia kazi mkopo.
RIP Mwalimu wewe ni binadamu ulikuwa udhaifu wako lakini mambo muhimu kwa binadamu yalikuwa mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…