Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, Mwl. Nyerere hakuwa mwanademokrasia!

Nimejiuliza maswali mengi baada ya kumewasikia wachangiaji karibu wote kwenye kusanyiko linaloitwa ‘’ kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ wakitoa mchanganuo wa maisha ya Mwl. Nyerere kama raia wa kawaida na Kiongozi Mkuu wa Tanganyika na Tanzania.

Miaka 29 ni mingi sana tokea Mwalimu Nyerere alipoachia ngazi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na kuwa mwananchi wa kawaida. Hii ina maana kuwa mtu mwenye miaka 28 hapa nchini hakuwahi kuona utendaji kazi wa Mwalimu Nyerere serikalini na ndani ya CCM. hili ni kundi la vijana ambalo kwa sasa lina watoto wenye umri wa miaka 11 kisheria kwa sababu umri wa kuanza kufanya mapenzi nchini ni miaka 18.

Kama wale wachangiaji niliowaona kwenye kongamano ndio tunawategemea sana katika mawazo yao kwenye kulijenga taifa basi hili taifa litaendelea kugubikwa na unafiki mkubwa ambao ni sumu kwa maendeleo chanya.

Bila kuondoa unafiki na kuwa wakweli hatuwezi kujua madhaifu yaliyolifanya taifa hili kupiga hatua za kusua sua katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Tunajua sheria za maumbile(laws of nature)zimetupa angalizo kuwa ili kitu kiwe kamili lazima kiwe na pande mbili. Hata nguvu za kifizikia ziko za aina mbili mbili ambazo ni hasi na chanya.

Nakumbuka wakati nikisoma shule ya ‘’ngumbalu’’ tulikuwa tunafanya makongamano na midaharo ambayo lazima iwe na pande mbili zinazoitwa wanaokubaliana (The affirmative or Aff) na wasiokubaliana (the Negative or Neg).Hii yote ni kukamilisha takwa la sheria za maumbile ambayo ndani yake kuna fikra.

Kamusi ya kiswahili sanifu inasema, kongamano/mdahalo ni majadiliano yanayofanywa na pande mbili zinazokinzana kuhusu suala fulani kwa kueleza sababu na ithibati ya msimamo wao tofauti na kufikia hitimisho la pamoja.

Kile kilichoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ hakikuwa na kiwango kinachokidhi kuitwa kongamano kwa sababu wachangiaji wote walikuwa wanaonyesha upande mmoja wa Mwl. Nyerere katika maisha yake.

Nadhani wale wanataka kumjua vizuri Mwl. Nyerere hawakuweza kupata upande wake wa pili kama ulivyobainishwa katika maandiko mengi na hasa kutoka kwa Mtanzania aitwaye Ludovic S. Mwijage katika maandiko yake kwenye vitabu mbali mbali ambavyo baadhi ni;

1)Dark side of NyerereLegacy-1996.
2) Julius K. Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant?-2010.

Watu kama Ludovic Mwijage walitakiwa pia watoe michango yao katika kongamano hili ili upande wa pili wa Mwl. Nyerere ueleweke na kueleweka kwa upande wa pili ungesaidia kutoa fundisho zuri kwa vizazi vijavyo.

Waandaaji wa kongamano walishindwa vipi hata kumualika James Brennan ambaye amefanya utafiti na kukusanya mawazo ya watu mbali mbali kuhusu Mwl. Nyerere na kuyaweka katika kitabu kinachoitwa , Nyerere through the Eyes of His Critics, 1953-2013

Wangeweza hata kumuarika mwanaJamiiforums mwenzetu, Mzee Mohamed Said ambaye ni mwandishi na mhariri wa maandiko mengi yenye mlengo wa kushoto kuhusu Mwl. Nyerere.

Tuache kuufanya mijadala kama hii iwe niya kinafiki kisiasa kama sehemu ya kuifundisha jamii yetu bali tufanye mijadala yenye pende mbili zenye mitazamo tofauti kama sehemu ya kuchambua ''pumba na mchele'' katika kuujua ukweli kwa sababu ukweli hujenga.

Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.

Tuache unafiki, tulitendee haki taifa letu na vizazi vijavyo!
Mkuu mapambio na vigelegele ndio uzalendo asilia...
Hatupaswi kuwa na akili fikirishi bali akili dumazi zenye ganzi ili mambo yasikwame...
 
Usiweke mwanvuli wa mawazo yako kwa watu wengine. Sema NAMSAMEHE na sio TUNAMSAMEHE!

Hoja yangu sio kumuhukumu Mwl. Nyerere bali kuonyesha mapungufu ambayo yapo lakini hayakusemwa kwa makusudi kwenye kongamano.

Kuna kongamano nchi hii utathubutu kuweka madhaifu ya Nyerere ueleweke? Kuweka mapungufu ya Nyerere hadharani ni kama tusi fulani hivi. Hata wanaoujua ukweli hawathubutu maana ni kama mungu fulani. Hiyo hunifanya nione Watanzania 90% ni wanafiki.
 
Nasikia majaribio ma4 ya kumwondoa magogoni yalishafanyika japo yalifeli,enzi ya utawala wake sikuepo najiuliza km Leo hii anapendwa kila kona ya dunia enzi ya uhai ilikuwaje wakataka kumwondoa
Katika kumbukizi na historia yake hayasemwi hayo wala hutayaona...
 
Nimejiuliza maswali mengi baada ya kumewasikia wachangiaji karibu wote kwenye kusanyiko linaloitwa ‘’ kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ wakitoa mchanganuo wa maisha ya Mwl. Nyerere kama raia wa kawaida na Kiongozi Mkuu wa Tanganyika na Tanzania.

Miaka 29 ni mingi sana tokea Mwalimu Nyerere alipoachia ngazi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na kuwa mwananchi wa kawaida. Hii ina maana kuwa mtu mwenye miaka 28 hapa nchini hakuwahi kuona utendaji kazi wa Mwalimu Nyerere serikalini na ndani ya CCM. hili ni kundi la vijana ambalo kwa sasa lina watoto wenye umri wa miaka 11 kisheria kwa sababu umri wa kuanza kufanya mapenzi nchini ni miaka 18.

Kama wale wachangiaji niliowaona kwenye kongamano ndio tunawategemea sana katika mawazo yao kwenye kulijenga taifa basi hili taifa litaendelea kugubikwa na unafiki mkubwa ambao ni sumu kwa maendeleo chanya.

Bila kuondoa unafiki na kuwa wakweli hatuwezi kujua madhaifu yaliyolifanya taifa hili kupiga hatua za kusua sua katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Tunajua sheria za maumbile(laws of nature)zimetupa angalizo kuwa ili kitu kiwe kamili lazima kiwe na pande mbili. Hata nguvu za kifizikia ziko za aina mbili mbili ambazo ni hasi na chanya.

Nakumbuka wakati nikisoma shule ya ‘’ngumbalu’’ tulikuwa tunafanya makongamano na midaharo ambayo lazima iwe na pande mbili zinazoitwa wanaokubaliana (The affirmative or Aff) na wasiokubaliana (the Negative or Neg).Hii yote ni kukamilisha takwa la sheria za maumbile ambayo ndani yake kuna fikra.

Kamusi ya kiswahili sanifu inasema, kongamano/mdahalo ni majadiliano yanayofanywa na pande mbili zinazokinzana kuhusu suala fulani kwa kueleza sababu na ithibati ya msimamo wao tofauti na kufikia hitimisho la pamoja.

Kile kilichoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ hakikuwa na kiwango kinachokidhi kuitwa kongamano kwa sababu wachangiaji wote walikuwa wanaonyesha upande mmoja wa Mwl. Nyerere katika maisha yake.

Nadhani wale wanataka kumjua vizuri Mwl. Nyerere hawakuweza kupata upande wake wa pili kama ulivyobainishwa katika maandiko mengi na hasa kutoka kwa Mtanzania aitwaye Ludovic S. Mwijage katika maandiko yake kwenye vitabu mbali mbali ambavyo baadhi ni;

1)Dark side of NyerereLegacy-1996.
2) Julius K. Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant?-2010.

Watu kama Ludovic Mwijage walitakiwa pia watoe michango yao katika kongamano hili ili upande wa pili wa Mwl. Nyerere ueleweke na kueleweka kwa upande wa pili ungesaidia kutoa fundisho zuri kwa vizazi vijavyo.

Waandaaji wa kongamano walishindwa vipi hata kumualika James Brennan ambaye amefanya utafiti na kukusanya mawazo ya watu mbali mbali kuhusu Mwl. Nyerere na kuyaweka katika kitabu kinachoitwa , Nyerere through the Eyes of His Critics, 1953-2013

Wangeweza hata kumuarika mwanaJamiiforums mwenzetu, Mzee Mohamed Said ambaye ni mwandishi na mhariri wa maandiko mengi yenye mlengo wa kushoto kuhusu Mwl. Nyerere.

Tuache kuufanya mijadala kama hii iwe niya kinafiki kisiasa kama sehemu ya kuifundisha jamii yetu bali tufanye mijadala yenye pende mbili zenye mitazamo tofauti kama sehemu ya kuchambua ''pumba na mchele'' katika kuujua ukweli kwa sababu ukweli hujenga.

Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.

Tuache unafiki, tulitendee haki taifa letu na vizazi vijavyo!
Mazingira ya kisiasa ya miaka ya 60's, 70"s na 80's ni tofauti kabisa na ya sasa. Huwezi kutumia vigezo vya kisasa vya kidemokrasia ili ukapate tathimini sahihi. Ukitaka kutambua ugwiji wa Mwalimu katika masuala ya kisiasa na kijamii, ebu jaribu kuangalia changamoto za umoja wa kitaifa ambazo tunazozipitia hivi sasa.
 
Bila kumung'unya maneno, mwalimu hakuwa mwanademokrasia. Likatiba lake lilikuwa bovu tu. Hata vyama vingi alilazimisha viwepo baada ya kuona kalikoroga na siasa zake za Ujamaa lakini vyama vingi vyenyewe alianzisha kinafiki kwani Mali nyingi alizigawa kwa CCM.
 
Back to Histoey!! Nyerere alikuwezesha Kusoma mpaka University with Government grants hakukua na Loan Board. Ulikua

Back to History!! Nyerere alikuwezesha Kusoma mpaka University Bure!!! (with Government grants hakukua na Loan Board). Ulikua Unakula + kulala Bure+ pesa ya kujikimu.
Leo Unakuja Jamii forum with Protuding Eyes Kumtusi Mwalimu.
Shame on You!!
RIP J.K. Nyerere.
Hakunilipia nyeyrere, ni tax walizolipia baba na mababu zetu
 
Mkuu;
Hoja yangu sio kufanya ulinganisho na waliomtangilia au waliokuja baada yake bali ni kuchambua maisha ya Mwl. Nyerere kama kiongozi anayedaiwa ni mwanademokrasia.
Comparative analysis ndio chimbuko la hoja yako usikwepe ndugu,unaposema hákuwa mwanademokrasia ni nan mwanademokrasia
 
Kuna kongamano nchi hii utathubutu kuweka madhaifu ya Nyerere ueleweke? Kuweka mapungufu ya Nyerere hadharani ni kama tusi fulani hivi. Hata wanaoujua ukweli hawathubutu maana ni kama mungu fulani. Hiyo hunifanya nione Watanzania 90% ni wanafiki.
Ndio maana hata katika historia ya nchi yetu , tunachaguliwa historia ya kulishwa... Kila kitu Mwalimu, Mwalimu utafikiri alikuwa anaongoza peke yake.

Hakuna tofauti na sasa kila kitu Magufuli Magufuli utafikiri anatoa hela zake mfukoni.
 
Ungeweza gharama za shule za kizungu kabla ya kutaifishwa??
Tunajisahau sana!!
Kuna mtu alinisimulia Waliuza Ng'ombe zaidi ya 10 ili aweze kusoma shule za MISHENI kipindi hicho.
Tuishi kwa Uhalisia!
Hivi unajua Wakati wa Mkoloni kulikua na kodi ya Kichwa??
Kwa nini ilikua ngumu kwa Natives kupata Elimu na Matibabu bure???
 
Watanzania tuache Unafiki.
Nchi za Wenzetu huwa wana Legacy zao.
Nyerere alijitahidi sana Kutuunganisha waTanzania. Nyerere angefuata mfumo wa Kikoloni ni wachache sana wangemudu Elimu. Wakati wa Mkoloni elimu ilikua ni Gharama sana. Kumbuka Missionaries schools.
Kila Binadamu ana mapungufu yake ila Kumbuka Nyerere Hakujilimbikizia Mali.
Nenda Butiama angalia Nyumba aliyojenga Mwalimu unaweza ukalia.
Mwalimu alisaidia nchi za kusini mwa Afrika kuweza kujitawala mfano Msumbiji, South Africa, Zimbabwe, Zambia.
Taifa lazima liwe na Legacy mfano
1. India - Gadhi
2. US- Linkolin
3. China- Mao
Kama kuna mapungufu ya Mwalimu hakuna haja ya Kuya Publisize!!!
Mkuu;
Haya ambayo umeorodhesha yanahusiana nini na hoja ya demikrasia? Kwa hiyo kwa kufanya hiki ulichokiorodhesha kinabainisha kuwa alikuwa mwanademokrasia?

Inawezekana sijaelewa mantiki ya hoja yako! Nielimishe!
 
Nikuulize wewe kwanza nipe Tafsiri ya neno Demokrasia!! Then We can Argue kama unavyotaka!
 
Nimejiuliza maswali mengi baada ya kumewasikia wachangiaji karibu wote kwenye kusanyiko linaloitwa ‘’ kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ wakitoa mchanganuo wa maisha ya Mwl. Nyerere kama raia wa kawaida na Kiongozi Mkuu wa Tanganyika na Tanzania.

Miaka 29 ni mingi sana tokea Mwalimu Nyerere alipoachia ngazi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na kuwa mwananchi wa kawaida. Hii ina maana kuwa mtu mwenye miaka 28 hapa nchini hakuwahi kuona utendaji kazi wa Mwalimu Nyerere serikalini na ndani ya CCM. hili ni kundi la vijana ambalo kwa sasa lina watoto wenye umri wa miaka 11 kisheria kwa sababu umri wa kuanza kufanya mapenzi nchini ni miaka 18.

Kama wale wachangiaji niliowaona kwenye kongamano ndio tunawategemea sana katika mawazo yao kwenye kulijenga taifa basi hili taifa litaendelea kugubikwa na unafiki mkubwa ambao ni sumu kwa maendeleo chanya.

Bila kuondoa unafiki na kuwa wakweli hatuwezi kujua madhaifu yaliyolifanya taifa hili kupiga hatua za kusua sua katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Tunajua sheria za maumbile(laws of nature)zimetupa angalizo kuwa ili kitu kiwe kamili lazima kiwe na pande mbili. Hata nguvu za kifizikia ziko za aina mbili mbili ambazo ni hasi na chanya.

Nakumbuka wakati nikisoma shule ya ‘’ngumbalu’’ tulikuwa tunafanya makongamano na midaharo ambayo lazima iwe na pande mbili zinazoitwa wanaokubaliana (The affirmative or Aff) na wasiokubaliana (the Negative or Neg).Hii yote ni kukamilisha takwa la sheria za maumbile ambayo ndani yake kuna fikra.

Kamusi ya kiswahili sanifu inasema, kongamano/mdahalo ni majadiliano yanayofanywa na pande mbili zinazokinzana kuhusu suala fulani kwa kueleza sababu na ithibati ya msimamo wao tofauti na kufikia hitimisho la pamoja.

Kile kilichoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ hakikuwa na kiwango kinachokidhi kuitwa kongamano kwa sababu wachangiaji wote walikuwa wanaonyesha upande mmoja wa Mwl. Nyerere katika maisha yake.

Nadhani wale wanataka kumjua vizuri Mwl. Nyerere hawakuweza kupata upande wake wa pili kama ulivyobainishwa katika maandiko mengi na hasa kutoka kwa Mtanzania aitwaye Ludovic S. Mwijage katika maandiko yake kwenye vitabu mbali mbali ambavyo baadhi ni;

1)Dark side of NyerereLegacy-1996.
2) Julius K. Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant?-2010.

Watu kama Ludovic Mwijage walitakiwa pia watoe michango yao katika kongamano hili ili upande wa pili wa Mwl. Nyerere ueleweke na kueleweka kwa upande wa pili ungesaidia kutoa fundisho zuri kwa vizazi vijavyo.

Waandaaji wa kongamano walishindwa vipi hata kumualika James Brennan ambaye amefanya utafiti na kukusanya mawazo ya watu mbali mbali kuhusu Mwl. Nyerere na kuyaweka katika kitabu kinachoitwa , Nyerere through the Eyes of His Critics, 1953-2013

Wangeweza hata kumuarika mwanaJamiiforums mwenzetu, Mzee Mohamed Said ambaye ni mwandishi na mhariri wa maandiko mengi yenye mlengo wa kushoto kuhusu Mwl. Nyerere.

Tuache kuufanya mijadala kama hii iwe niya kinafiki kisiasa kama sehemu ya kuifundisha jamii yetu bali tufanye mijadala yenye pende mbili zenye mitazamo tofauti kama sehemu ya kuchambua ''pumba na mchele'' katika kuujua ukweli kwa sababu ukweli hujenga.

Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.

Tuache unafiki, tulitendee haki taifa letu na vizazi vijavyo!
Kwahiyo wewe twambie mwana demokrasia ni yupi?
 
..TL amejitahidi kumjadili Mwalimu kama unavyopendekeza ktk hoja yako.

..amefafanua kwamba Mwalimu wa 1962 mpaka 1984 aliondoa vyama vingi, aliongoza bila bill of rights, aliweka watu kizuizini bila ukomo.

..lakini vilevile TL amesema anamkubali Mwalimu yule mwaka 1990 mpaka anafariki kwasababu ya mchango wake ambao uliwezesha kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

..Mjadala unaomhusu Mwalimu Nyerere mara nyingi unaharibiwa na makada wa CCM ambao wamezoeshwa utamaduni wa kuimba mapambio ya kusifia tu, na siyo kufanya uchambuzi wa kina na kisomi kuhusu mada mbalimbali.
Na huo utamaduni wa kuimba na kusifia umeanzishwa na huyohuyo mnayemjadili....itikadi za kijamaa ambazo zinatutafuna mpaka sasa.
 
Kuna kongamano nchi hii utathubutu kuweka madhaifu ya Nyerere ueleweke? Kuweka mapungufu ya Nyerere hadharani ni kama tusi fulani hivi. Hata wanaoujua ukweli hawathubutu maana ni kama mungu fulani. Hiyo hunifanya nione Watanzania 90% ni wanafiki.
Uko vizuri sana mkuu "conscience" yako iko juu. Wasiwasi wangu usije kubadilika tu, maana nchi ina upungufu sana wa watu kama wewe.
 
Ungeweza gharama za shule za kizungu kabla ya kutaifishwa??
Tunajisahau sana!!
Kuna mtu alinisimulia Waliuza Ng'ombe zaidi ya 10 ili aweze kusoma shule za MISHENI kipindi hicho.
Tuishi kwa Uhalisia!
Nyerere hakudai uhuru peke yake, aliodai nao uhuru ambao ni babu zetu, hizo ni miongoni mwa ajenda zao. tax zetu itumike kutupatia elimu na matibabu bure.
 
Nyerere alikuwa Dikteta Mnafiki
Upande mmoja alikuwa kibaraka wa Urusi na China upande wa pili alikuwa Kibaraka wa Mabepari kuzuia Znz isiangukie kwenye Ukomunist
Mkuu;
Kwa kiwango kikubwa ninakubaliana na angalizo lako!
 
By then, Foreign Policy ya TZ ilikuwa ni kutofungamana na bloc yoyote (East au West).

Back
Top Bottom