"MsemajiUkweli, post: 33260843, member: 91662"]Wangeweza hata kumuarika
Kumuarika= Kumualika
Tuache kuufanya mijadala kama hii iwe niya kinafiki kisiasa kama sehemu ya kuifundisha jamii yetu bali tufanye mijadala yenye pende mbili zenye mitazamo tofauti kama sehemu ya kuchambua ''pumba na mchele'' katika kuujua ukweli kwa sababu ukweli hujenga.
Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.
Tuache unafiki, tulitendee haki taifa letu na vizazi vijavyo!
Kinachokukera ni kusikia mazuri ya Mwalimu yakielezwa hivyo huenda yakafunika mengine au kutuonyesha matundu mengine.
Tayari kuna pande mbili!
Upande wa kwanza ni ule unamtuhumu Mwalimu kwa kutojenga ''Vituo vya afya 300 hata kama hatukuhitaji''.
Ni ule usiosema changamoto na mafanikio ya Mwalimu
Upande huu hudhani Tanzania ya 1961 ni sawa na ya 2019 ambako wasomi hawana kazi
Hawaelewi Tz ya Mwalimu kumpata mkuu wa Wilaya ilikuwa taabu sana
Upande huu wa kwanza unamhukumu Mwalimu kwa kujenga taasisi na miundo mbinu kwa kumsumanga tu. Hauelezi Mwl alifanya nini kiuchumi, kijamii na kisiasa!
Kwa ufupi Mwalimu akiwa amepumzika kaburini anatukanwa na kusumangwa na upande huu wa kwanza ili kumshushia heshima na hadhi yake. Kufanya hivyo kutarahisha kazi nyingine...
Upande wa Pili ni huu wa Kongamano la Mwalimu.
Upande huu umeishi na kuona ya Mwl, wanachokifanya ni kusahihisha upotoshaji unaoenezwa kuhusu Mwl na upande wa kwanza
Hivyo Kongamano linajibu kadhia, indhara na matusi dhidi ya Mwalimu
Ni kongamano linalomsemea Mwalimu kutoka kabarini
Hadi hapo matusi, indhara, kadhia na kashfa dhidi ya Mwl zitakapoachwa, tutaona Mwl asiyeweza kujitetea kwa kuwa ni marehemu akitetewa na waliomfahamu
Utetezi wa Mwl anayehukumiwa hauhitaji pande mbili, huu ni uetetezi unamweleza Mwalim