Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, Mwl. Nyerere hakuwa mwanademokrasia!

Tusipakane mafuta kwa mgongo wa chupa, Mwl. Nyerere hakuwa mwanademokrasia!

Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.
Hili lilikuwa kongamano lao, kwa nini uwapangie cha kufanya.
Nenda na wewe kaandae la kwako uwaalike unaotaka waje kuwasilisha mada. Shida ipo wapi?
 
Nyerere alikuwa dikteka kwa sababu moja tu. Kura za maoni wengi walichagua kuendelea na mfumo wa chama kimoja...demokrasia inatuambia alipaswa kufuata maoni ya wengi, hata kama hawako sahihi.
 
Back to Histoey!! Nyerere alikuwezesha Kusoma mpaka University with Government grants hakukua na Loan Board. Ulikua

Back to History!! Nyerere alikuwezesha Kusoma mpaka University Bure!!! (with Government grants hakukua na Loan Board). Ulikua Unakula + kulala Bure+ pesa ya kujikimu.
Leo Unakuja Jamii forum with Protuding Eyes Kumtusi Mwalimu.
Shame on You!!
RIP J.K. Nyerere.
Na ni hawa hawa, "vijana waliotumwa kijiji cha pili wakahemee, kuepusha njaa iliyokikumba kijiji chao kisiangamie;" badala yake wakawa ndio maadui wakubwa wa kijiji chao na kuharibu kila mradi waliopewa kuuendesha!

Leo hii wanakuja hapa na kujibaraguza kwa kushindwa kwa kutekelezwa kwa ufanisi mipango mingi ya maendeleo iliyowekwa, na kutoa shutuma kwa mtu mmoja kana kwamba ni yeye pekee aliyetakiwa kutekeleza kila sera iliyotungwa.

Na wakati huo huo, mtu huyo anayejidhani anazo za kumtosha anashindwa kujiuliza inakuwaje mtu huyo huyo aliyeondoka miaka 29 iliyopita bado anakumbukwa na kuthaminiwa na watu aliowaongoza kwa miaka yote ile.

Hataki kujiuliza na kulijibu hilo.
 
Nimejiuliza maswali mengi baada ya kumewasikia wachangiaji karibu wote kwenye kusanyiko linaloitwa ‘’ kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ wakitoa mchanganuo wa maisha ya Mwl. Nyerere kama raia wa kawaida na Kiongozi Mkuu wa Tanganyika na Tanzania.

Miaka 29 ni mingi sana tokea Mwalimu Nyerere alipoachia ngazi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na kuwa mwananchi wa kawaida. Hii ina maana kuwa mtu mwenye miaka 28 hapa nchini hakuwahi kuona utendaji kazi wa Mwalimu Nyerere serikalini na ndani ya CCM. hili ni kundi la vijana ambalo kwa sasa lina watoto wenye umri wa miaka 11 kisheria kwa sababu umri wa kuanza kufanya mapenzi nchini ni miaka 18.

Kama wale wachangiaji niliowaona kwenye kongamano ndio tunawategemea sana katika mawazo yao kwenye kulijenga taifa basi hili taifa litaendelea kugubikwa na unafiki mkubwa ambao ni sumu kwa maendeleo chanya.

Bila kuondoa unafiki na kuwa wakweli hatuwezi kujua madhaifu yaliyolifanya taifa hili kupiga hatua za kusua sua katika nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Tunajua sheria za maumbile(laws of nature)zimetupa angalizo kuwa ili kitu kiwe kamili lazima kiwe na pande mbili. Hata nguvu za kifizikia ziko za aina mbili mbili ambazo ni hasi na chanya.

Nakumbuka wakati nikisoma shule ya ‘’ngumbalu’’ tulikuwa tunafanya makongamano na midaharo ambayo lazima iwe na pande mbili zinazoitwa wanaokubaliana (The affirmative or Aff) na wasiokubaliana (the Negative or Neg).Hii yote ni kukamilisha takwa la sheria za maumbile ambayo ndani yake kuna fikra.

Kamusi ya kiswahili sanifu inasema, kongamano/mdahalo ni majadiliano yanayofanywa na pande mbili zinazokinzana kuhusu suala fulani kwa kueleza sababu na ithibati ya msimamo wao tofauti na kufikia hitimisho la pamoja.

Kile kilichoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ hakikuwa na kiwango kinachokidhi kuitwa kongamano kwa sababu wachangiaji wote walikuwa wanaonyesha upande mmoja wa Mwl. Nyerere katika maisha yake.

Nadhani wale wanataka kumjua vizuri Mwl. Nyerere hawakuweza kupata upande wake wa pili kama ulivyobainishwa katika maandiko mengi na hasa kutoka kwa Mtanzania aitwaye Ludovic S. Mwijage katika maandiko yake kwenye vitabu mbali mbali ambavyo baadhi ni;

1)Dark side of NyerereLegacy-1996.
2) Julius K. Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant?-2010.

Watu kama Ludovic Mwijage walitakiwa pia watoe michango yao katika kongamano hili ili upande wa pili wa Mwl. Nyerere ueleweke na kueleweka kwa upande wa pili ungesaidia kutoa fundisho zuri kwa vizazi vijavyo.

Waandaaji wa kongamano walishindwa vipi hata kumualika James Brennan ambaye amefanya utafiti na kukusanya mawazo ya watu mbali mbali kuhusu Mwl. Nyerere na kuyaweka katika kitabu kinachoitwa , Nyerere through the Eyes of His Critics, 1953-2013

Wangeweza hata kumuarika mwanaJamiiforums mwenzetu, Mzee Mohamed Said ambaye ni mwandishi na mhariri wa maandiko mengi yenye mlengo wa kushoto kuhusu Mwl. Nyerere.

Tuache kuufanya mijadala kama hii iwe niya kinafiki kisiasa kama sehemu ya kuifundisha jamii yetu bali tufanye mijadala yenye pende mbili zenye mitazamo tofauti kama sehemu ya kuchambua ''pumba na mchele'' katika kuujua ukweli kwa sababu ukweli hujenga.

Walioandaa kinachoitwa ‘’kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere’’ haikuwa ni kongamano bali ni mkusanyiko wa wapiga propaganda zenye unafiki.

Tuache unafiki, tulitendee haki taifa letu na vizazi vijavyo!
Kiongozi yupi ni mwana demokrasia? Tupe mfano.
Halafu lengo lako ni lipi? Au umeamua tu kumjadili J.K.Nyerere (RIP)
 
By then, Foreign Policy ya TZ ilikuwa ni kutofungamana na bloc yoyote (East au West).

Huo ni unafiki mwingine

Unapokea mafungu ya urusi kupiganisha vita Africa

Unasimama kidete kutetea Wajamaa kupata kiti Chan kudumu UN then unataka kuaminisha watu Wewe ni ‘Non aligned Movement’
 
Ukiulizwa tetea kuwa Nyerere alikuwa Mwana Demokrasia jibu lake ndio hilo kuwa tuangalie nyumba yake Butiama?
Mkuu;
Nimesoma maoni yako nikacheka sana!

Kuna baadhi ya watu mnajua kujibu hoja!

Akirudi tena naomba unitag!
 
Mkuu;
Nimesoma maoni yako nikacheka sana!

Kuna baadhi ya watu mnajua kujibu hoja!

Akirudi tena naomba unitag!
Nikuulize tena???
Hivi unaweza kuwa Mwanademokkrasia wakati umejilimbikizia ukwasi wa Utajiri +Majumba ya Kifahari????
Wakati Wananchi wako ni Mafukara wa Kutupwa???
Ndo maana nikakuuliza
Unaelewaje maana ya Neno Demokrasia????
 
..TL amejitahidi kumjadili Mwalimu kama unavyopendekeza ktk hoja yako.

..amefafanua kwamba Mwalimu wa 1962 mpaka 1984 aliondoa vyama vingi, aliongoza bila bill of rights, aliweka watu kizuizini bila ukomo.

..lakini vilevile TL amesema anamkubali Mwalimu yule mwaka 1990 mpaka anafariki kwasababu ya mchango wake ambao uliwezesha kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini.

..Mjadala unaomhusu Mwalimu Nyerere mara nyingi unaharibiwa na makada wa CCM ambao wamezoeshwa utamaduni wa kuimba mapambio ya kusifia tu, na siyo kufanya uchambuzi wa kina na kisomi kuhusu mada mbalimbali.


Uko sahihi.
Na pia, mijadala ya kumhusu huyu Mzee, inaharibiwa na watu wanaomtazama kidini. Kuna watu kadhaa wameanzisha threads hapa kwa vile tu wanamhusisha na upendeleo/uonevu na dini fulani. As a result, most of them present seemingly objective views which are in reality subjective.
 
Ww hasa ndio walengwa wa huu uzi, nyie ndio msiojua matusi na ukweli, kiasi kwamba upande wa pili wa kiongozi unapowekwa hadharani mnakuja na upotoshaji ionekane ametukanwa. Aina yako ya watu ndio wako mbele na viongozi wa nchi hii mnaotumia kichaka cha kutukanwa ili kufunika ukweli.

..wanatumia kichaka cha "kutukanwa" kufanya mambo mabaya kwa waTz wenzao ikiwemo KUDHALILISHA, na KUTESA
 
Nyerere ndiye architect wa kuharibu chaguzi za Zanzibar

Hata hivyo tunamsamehe kwa sababu ndiye muasisi wa Taifa hili jambo hilo ni kubwa mno kuliko makosa aliyotenda akiwa madarakani
hebu elezea hapo kwenye uasisi wa taifa hili,huwa sielewi,maana mipaka ya nchi hii walichora wazungu
 
Watanzania tuache Unafiki.
Nchi za Wenzetu huwa wana Legacy zao.
Nyerere alijitahidi sana Kutuunganisha waTanzania. Nyerere angefuata mfumo wa Kikoloni ni wachache sana wangemudu Elimu. Wakati wa Mkoloni elimu ilikua ni Gharama sana. Kumbuka Missionaries schools.
Kila Binadamu ana mapungufu yake ila Kumbuka Nyerere Hakujilimbikizia Mali.
Nenda Butiama angalia Nyumba aliyojenga Mwalimu unaweza ukalia.
Mwalimu alisaidia nchi za kusini mwa Afrika kuweza kujitawala mfano Msumbiji, South Africa, Zimbabwe, Zambia.
Taifa lazima liwe na Legacy mfano
1. India - Gadhi
2. US- Linkolin
3. China- Mao
Kama kuna mapungufu ya Mwalimu hakuna haja ya Kuya Publisize!!!
Kuna haja kubwa ya kutangaza mabaya ya mwalimu kuliko hata mazuri yake. Leo CCM wanaogopa kujitangaza kuwa siyo chama cha ujamaa kwasababu ni kama kumpinga mwalimu japo wakina Serukamba et al hawaamini tena ujamaa. Hilo linatuathiri wote, tuna taasisi za kijamaa kwenye ulimwengu wa kibepari. Hatuwezi songa mpaka tutakapoacha kuongozwa na mzimu wa Mwalimu.
 
Msingi wa mawazo yangu uliyo quote ilikuwa ni kupinga kuwa Lissu hana unafiki.

Ni kweli kwenye kujadili maisha ya Mwl. Nyerere kama kiongozi anaweza asijadili kwa unafiki lakini hii haiondoi ukweli kuwa hata yeye ni mnafiki kama wanasiasa wote nchini.

Lissu anachofanya ni kuchagua wapi asionyeshe unafiki na wapi aonyeshe unafiki kwa faida ya kisiasa.

..pamoja na mtizamo hasi ulionao dhidi ya TL ktk hoja hii mawazo yenu yanafanana.😁
 
Nyerere alishasema tunachukua mabaya yake na kuacha mazuri yake. Alishatuambia tunalikatiba libaya cha ajabu akatuachia likatiba hilo hilo na uchama dola wa CCM ambao sasa unatupa shida. Kuhusu demokrasia sijui nitamuweka wapi lakini watanzania walimuita "Mzee haambiliki" na waliompinga tunajua yaliyowakuta. Sasa kwenye midahalo wasemaji wanachaguana wao kwa wao ndiyo maana upande wa pili huwezi kuusikia. Tofauti kuu ya Nyerere ambayo hufanya watu wafunge macho ni hakuwa mbinafsi wa maendeleo ya familia wala nchi style ya project Bagamoyo na Project Chato acha familia za viongozi wetu etc.
 
Huo ni unafiki mwingine

Unapokea mafungu ya urusi kupiganisha vita Africa

Unasimama kidete kutetea Wajamaa kupata kiti Chan kudumu UN then unataka kuaminisha watu Wewe ni ‘Non aligned Movement’
Ita unafiki, wenye uelewa tunaita 'bloc politics'...
Ita kupokea mafungu kupiganisha vita, wenye uelewa tunaita TZ's Foreign Policy.. liberation of fellow african countries
 
Back
Top Bottom