Tusipende kutumia msemo kwamba Mungu amempa huyu na fulani hajampa, Mungu hana upendeleo na huenda anahusika kidogo sana kwenye mafanikio yetu duniani

Tusipende kutumia msemo kwamba Mungu amempa huyu na fulani hajampa, Mungu hana upendeleo na huenda anahusika kidogo sana kwenye mafanikio yetu duniani

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Msemo huu hupendwa sana kutumika hasa na watu kanda ya mikoa ya pwani ya bahari. Utasikia hili sio fungu langu, fulani kapewa fulani kanyimwa.

Hizi ni fikra za kimasikini sana za kumfanya mtu anafikia mpaka kuridhika na hali yake na kushindwa kupambana kwa njia tofauti za kufikia malengo yake.

Mtu kahangaika kupanda miti huko njombe miaka ya 2010 leo anavuna miti account yake inasoma milioni 100 ila mwaka ule 2010 wewe uliamua kutumia pesa kuponda starehe badala ya kuwekeza, Mungu anahusika vipi hapo.

Mwenzako ni msafi na mtanashati na huenda umemzidi kipato, wewe nimrafu rafu tu unalalamika huna mvuto, Mungu anahusika vipi hapo.

Mwenzako anaishi vizuri na jamii, anashiriki shughuli za jamii, anaisaidia jamii kwa uwezo alionao, n.k.

Wewe hata misiba hushiriki unatoa tu rambi rambi, hujitolei kwenye shughuli za kijamii, unaishi kivyako vyako, n.k unalalamika kwamba fulani kapewa upendeleo, una akili wewe!

Mungu kashakupa akili ya kuishi kwenye mazingira ni wewe kujua sasa uitumie akili ama usiitumie.
 
"Njia rahisi ya kufanikiwa ni kufanyia kazi ushauri unaowapa wengine na kuuishi"

Anonymous
 
Kila mtu anapewa kwa wakati wake na siyo wote watapewa au kufurahia mali.
 
Back
Top Bottom