nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,035
- 2,938
Pole Sana. Kanda ya Ziwa linapofika suala la Kura ni wamoja. Acha kujitekenya.Unapoizungumzia Kanda ya Ziwa kwa maana ya block moja yenye wingi wa kura nadhani tunajidanganya mchana kweupe.
Kanda ya Ziwa kuna Wasukuma ( makabila madogo madogo mengi ndani yake).
Wapo Wahaya ambao wana utamaduni wao usioingiliana na Wasukuma kabisa.Ukienda Kagera Wahaya wanajiona kama Wahaya hawajinadibishi na Wasukuma hata kidogo.Wahaya wana Lugha yao,wana mila zao,wana matambiko yao ambayo ni tofauti kabisa na Wasukuma !.
Kanda ya Ziwa wapo Wakurya sijaona mfano wao na Wasukuma au Wahaya.Wakurya ni Wakurya hawajioni ni sehemu ya Wahaya ama Wasuma.
Kanda ya Ziwa ina idadi kubwa ya watu ambao si wamoja wala hawapigi kura as a block kama wafanyavyo Wazanzibari au Wakikuyu wa Kenya ama Wakamba wa Kenya.
Ni ushamba wa Kiwango cha kustaajabisha kujaribu kutuambia Tanzania ina viwango vya ukabila sawa na Majirani wetu wa Kenya ambao kila uchaguzi unapofika suala la ukanda na ukabila linachukua nafasi kubwa.