Tusipoangalia kanda ya ziwa itatuletea tyranny of the majority

Tusipoangalia kanda ya ziwa itatuletea tyranny of the majority

Wasukuma watakutesa sana! Ukisikia kanda ya ziwa ndo makao makuu ya Sukuma gang!
Makonda hakulamba viatu vya Samia!
Samia kaona anamuhitaji wewe ni nani ubeze uteuzi wake!
Mwanza kesho na jumatatu tuko na mtoto wa nyumbani!
Karibu Igoma nyumbani kwa wazazi wa Makonda kipenzi chetu!
Duu,Mama Samia kachezesha dishi kidogo tuu, Wasugusu wote wamejaa kwenye channel moja tuu tena ya bure. Duu,
 
Hainess Kiwia alikuwa mbunge wa Ilemela ni mchaga mbona naye ni Kapuku tu!
Mafanikio ni mtu binafsi acha kukariri maisha!
Rejea post yangu nilisema maisha ya siasa ni ya kubahatisha. Sawa siangalii kabila ila nimeandika facts unakuwaje waziri unapiga hela ndefu zaidi ya "billion kwenye matangazo unakuja kufanya biashara ya kuuza na kunua mazao ? H:K alishindwa hata kununua bonds za South Africa kweli ? Aisee narudia tembea uone maana hata Mbunge Kishimba Zimbabwe alijifunza mengi sana. Kila mtu anaweza kufanikiwa na ninafanya biashara na kila mtu. Nimeshawai kupiga dili na mhindi anaewachukia watu weusi lakini sikujali ili mkono uende kinywani leo hii ananipa hela kuliko wahindi wenzake. Amenifundisha mpaka caste system wanazotumia nchini mwao. Wahindi waogope sana kule kwao kuna makabila yamepangiwa kazi zao ni kufanya usafi mpaka kufa wanaitwa "dalit". Jamani we acha tu Tanzania ni nchi nzuri sana tatizo watanzania hawataki kuizunguka nchi yao. Usishangae wahindi kuacha nchi yao kuja huku kwetu kule kwao kuna watu wanakufa kwa njaa. Exposure ni kitu muhimu sana, hata ule mji wa NHC chato ulifeli kwa ushamba wa wasukuma. Maana wenye hela ya kununua mjengo wanazurula na ng'ombe kila mkoa. Nampongeza JPM maana alijitahidi kuwapa kipaumbele kwenye scolarship kanda ya ziwa, najua kuna wasukuma walisoma nchi za U.k, New Zealand, Marekani na Australia kipindi chake alijitahidi sana kwa kweli. Nilikuwa kwenye system najua.
 
Wasukuma ni 16% ya Watanzania wote ni kubwa ndiyo lakini tusikuze hivyo😂

Mfano watu wa kaskazini hatupo wengi kwenye siasa lakini uchumi unatuhusu

Wamasai, wameru, wachaga, wasambaa, wapare, wazigua na waswahili wetu wa Tanga mjini tupo vizuri sana kwenye uchumi. Tunachangia.

Kanda ya kusini inakuja juu
Watu waliotokea kule Mbeya, Iringa , ….. nao wanakuja kasi kiuchumi.

Kanda zilizolala ni kule Mtwara, lindi…. na kigoma huko wamajaa wavivu yupu. Utamaduni wa wao ndiyo tatizo huko

Hivyo tuache ukabila
We ndiyo umeanza kuzungumzia makabila.
 
Kanda ya ziwa itakuja kutamba siku mzee wa .......akienda peponi. Lkn kama bado anaishi haitatokea
Huyo mzee hana chake! Alimponda Chalamila kwenye mkutano mkuu wa CCM baada ya mwezi mama akampa promotion kuwa mkuu wa mkoa wa Dar!
Kizazi kimabadilika mda wake uko ukingoni! 2030 kanda ya ziwa itatamba sana tu!
 
Kanda ya ziwa itakuja kutamba siku mzee wa .......akienda peponi. Lkn kama bado anaishi haitatokea
Umesahau ilitamba akiwepo,sema Mzee huyo kazi yake ni kueliminate. Sema Magufuli aliwachanganya hadi wakaona wamuue tu .
 
Kanda ya ziwa wameishaujua mtaji wao kwenye siasa za Tanzania. Wanajua jinsi walivyo wengi. Na bahati mbaya au nzuri ndiyo wanaongoza kwa kuzaliana nchini. Dalili zinaonyesha wanataka kuutumia mtaji huo kukandamiza wengine. Leo hii hata wabunge wao ni kama hawasemehi majimbo yao tena bali kanda ya ziwa yote. Ni kama kila mbunge wa eneo hilo anawakilisha kanda yote.

Tusipokuwa makini watatukandamiza nchi yote sababu ya wingi wao. Watataka lazima mtu fulani mkubwa serikalini atoke kwao. Watalazimisha gawio kubwa la miradi nk. Nadhani huko mbeleni mfumo wa majimbo hautaepukika.
Unapoizungumzia Kanda ya Ziwa kwa maana ya block moja yenye wingi wa kura nadhani tunajidanganya mchana kweupe.

Kanda ya Ziwa kuna Wasukuma ( makabila madogo madogo mengi ndani yake).
Wapo Wahaya ambao wana utamaduni wao usioingiliana na Wasukuma kabisa.Ukienda Kagera Wahaya wanajiona kama Wahaya hawajinadibishi na Wasukuma hata kidogo.Wahaya wana Lugha yao,wana mila zao,wana matambiko yao ambayo ni tofauti kabisa na Wasukuma !.

Kanda ya Ziwa wapo Wakurya sijaona mfano wao na Wasukuma au Wahaya.Wakurya ni Wakurya hawajioni ni sehemu ya Wahaya ama Wasuma.

Kanda ya Ziwa ina idadi kubwa ya watu ambao si wamoja wala hawapigi kura as a block kama wafanyavyo Wazanzibari au Wakikuyu wa Kenya ama Wakamba wa Kenya.

Ni ushamba wa Kiwango cha kustaajabisha kujaribu kutuambia Tanzania ina viwango vya ukabila sawa na Majirani wetu wa Kenya ambao kila uchaguzi unapofika suala la ukanda na ukabila linachukua nafasi kubwa.
 
Wapigania Uhuru 90% walikuwa wenyeji wa Pwani na Moslems na ndio maana Kuna baadhi ya Picha zinamuonesha Mwl Amevaa barakashia,
Hivi unawajua Matajiri wa kutoka Pwani Kina Dossa Azizi walivyotoa pesa zao kupigania Uhuru?
Mlipigania uhuru na mkaupata mapema ni kipi mlichofaidika nacho baada ya kuwatoa wakoloni? Mada zako ni kupondea wasukuma, kupondea wakristo, na kuwainua waislamu hasa watu wa pwani, acha kejeli acha kudharau watu na hujui nguvu zao na udhaifu wao.
 
Aliyeanza kutugawa ni Mwalimu Nyerere, miaka ya i930 tulikuwa na mkakati wa kujenga chuo kikuu WEST LAKE tulipopata uhuru mwalimu akatutaka tusubili kwanza kwa madai tulikuwa tumepiga hatua kubwa tulikuwa tunasomesha watoto kwa hela zetu za ushirika na mabo mengi tu tulikuwa mbele tuliendelea kusubili maendeleo hadi leo tuliminywa ili tuwasubili wenzetu waliokuwa na hali mbaya zaidi le hata makao makuu ya mkoa hayana stendi hayana hospitali tukiacha zile za kanisa, mbali na Barongo wakati wa mwalimu sikumbuki waziri aliyeteuliwa kutoka kagera tukiacha manaibu, wasomi wengi wa kanda ya ziwa walilazimika kwenda uhamishoni niite intellectual exile kwa sababu hawakutakiwa hawakupewa nafasi kwa hofu ya Mwalimu. sasa hivi ziara zote hizo za Paulo kuanzia huko ni kujaribu kufanya toba ya ukandamizaji wa maendeleo uliofanywa, bado kuna ukumgu mioyoni mwao na kuna hofu wanaweza kutoa adhabu kwa serikali, Makonda anaanza kanda ya ziwa kimkakati, Biteko ameteuliwa kimkakati. yetu macho tujiandae kuona mengi.
Nimekumbuka zaidi ya tillion 2 zilozokwapuliwa kwa nguvu kutoka kwa wafanyabiashara wa kagera...nyumba nyingi bukoba mjinu kutaifisha kisa watu wa bukoba hawakukubaliana na ujamaa...
Wafanyabiashara na wasomi walikimbia bukoba miaka ya 1980 baada ya operation hiyo...na mji wa bukoba ukastack hadi leo..
Ni juzi juzi tu Bukoba imeanza kuinuka tena na nakwambia baada ya miaka michache bukoba haitakamatika tena kimaendeleo kama ile mipango ya maendeleo iliyopangwa ikikamilika...mfano ni upanuzi wa bandari, ujenzi wa uwanja mpya kajunguti, ujenzi barabara ya njia nne, soko, stendi nk...
 
Mlipigania uhuru na mkaupata mapema ni kipi mlichofaidika nacho baada ya kuwatoa wakoloni? Mada zako ni kupondea wasukuma, kupondea wakristo, na kuwainua waislamu hasa watu wa pwani, acha kejeli acha kudharau watu na hujui nguvu zao na udhaifu wao.
- hujui tulichofaidika baada ya kupata Uhuru? Nimeamini kuwa wewe ni mbumbumbu usiyejitambua na usiyejua thamani ya Uhuru wa Nchi yako.
-Kwani ni Uongo Wapigania Uhuru wengi walitokea Ukanda wa Pwani?
  • Makao Makuu ya TAA/TANU yalikuwa bariadi?
  • kwani ni Uongo TANU ilishikiliwa na Moslems kwa asilimia kubwa? Hadi salamu ndani ya TANU ilikuwa 'asaalm aleykum '?
-Endelea kukaa hapo Burigi
 
Mwalimu Nyerere alimaliza ukabila na Ukanda Nchi hii. Sasa hivi umetokea wapi tena? Imekuwaje mpaka watu wanaongea kilugha majukwaani? Wakati wa Nyerere ukiongea kilugha jukwaani unaonekana hufai, mkabila na mshamba!

Kwa Upande wa majimbo, lazima yatakuja huko mbeleni! Haiwezekani Waziri wa Ujenzi anaulizwa Kuhusu km 5 za lami huko Bukoba; haiwezekani Waziri wa Kilimo anaulizwa swala la Nyani kula mahindi ya Wana Kijiji huko Manyara, au Waziri wa Maliasili anaulizwa Kuhusu watu kuliwa na namba huko ziwani Victoria au mtoni Kilombero! Haiwezekani!! Hayo ni mambo yanatakiwa yashughulikiwe huko locally, sio kitaifa!

Kanda ya ziwa wameishaujua mtaji wao kwenye siasa za Tanzania. Wanajua jinsi walivyo wengi. Na bahati mbaya au nzuri ndiyo wanaongoza kwa kuzaliana nchini. Dalili zinaonyesha wanataka kuutumia mtaji huo kukandamiza wengine. Leo hii hata wabunge wao ni kama hawasemehi majimbo yao tena bali kanda ya ziwa yote. Ni kama kila mbunge wa eneo hilo anawakilisha kanda yote.

Tusipokuwa makini watatukandamiza nchi yote sababu ya wingi wao. Watataka lazima mtu fulani mkubwa serikalini atoke kwao. Watalazimisha gawio kubwa la miradi nk. Nadhani huko mbeleni mfumo wa majimbo hautaepukika.
 
Back
Top Bottom