Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Ni kweli mkuu lakini binafsi. Ikitokea siku akapatikana kiongozi wa kuiondoa political supremacy iliyopo Tanzania, huyo ndo nitamuona yupo serious na kuikomboa hii nchi.

Naheshimu baadhi ya hoja anazozisema polepole hususani kutengeneza mfumo wa viongozi kuwa accountable kisheria na hata lissu pia anavyopambania kile anachokiamini. Lakini mwisho wa siku kama hatotokea kiongozi wa kuona umuhimu wa kuitoa nchi katika mikono ya vyama na kuirudisha kwa wananchi. Sioni hii nchi ikibadilika

Ni sawa na Kenya kwenye siasa za ukabila, huko Uganda na Rwanda tunajua kinachoendelea ila tatizo la Tanzania ni uvyama. Watanzania wengi kushindwa kutofautisha maslahi au uzalendo wa vyama vs taifa. Ubaya Nyerere ndiye aliyetuachia hiki kitu kwa kuunganisha mamlaka ya Nchi na CCM huku wanachi wakiwa powerless and obidient kwa mamlaka kwa imani ya kuwa CCM itabaki safi milelel. Hali imekuwa tofauti kiasi and now, taifa linalipia hiyo gharama
 
Haya WAKUU, mimi NIWATAKIENI KILA LA KHERI

===================================================
​
Mkuu, tulipofikia hapa ni pagumu, na ukweli tulipofikia ni pabaya. Njia pekee ya Tanzania kunusurika ni kuuacha ujinga utugharimu. Tukishapata madhara makubwa sana nafikiri litakuwa somo kubwa. Kwa akili ya mtu mweusi athari huwa anaihisi ikimgusa moja kwa moja kwenye ngozi na wala si kwenye akili yake.

Kwa hatua tuliyoifikia Tanzania binafsi sitaki kuumiza akili.
 
Mkuu kumlaumu Nyerere kwa makosa yetu wenyewe ni kukwepa uwajibikaji uleule unaotaka tuupoganie.

Nyerere hayupo tangu 1999 - 27 years ago!

Kuna nn alichoweka Nyerere ambacho sie hatuna ubavu wa kukibadilisha?

Huo hilo ni sawa na kijana anayeendelea kuwalaumu wazazi wake kwa madhila ya maisha yake, huku akikwepa uwajibikaji wake mwenyewe?

Nyerere alifanya mengi mazuri mangapi? Umewahi kusoma vitabu vyake? Hotuba zake je?

Alionesha mfano wa uongozi, alikemea maovu waziwazi (rushwa, ukabila, udini, ubadhirifu, uzembe, ubinafsi).

Je katika hayo mazuri tumetekeleza mangapi?

Kwani tulitegemea Nyerere atufanyie kila kitu??? Spoonfed little babies ndo sisi leo bila shaka!!!

Tatizo la Watanzania wengi wanatamani mabadiliko, lakini yaletwe na mtu fulani hukooo - wao wakiwa wamejiketisha wakichati, wakibeti na kuburudika!!!

Huu ni wakati wa kuacha malalamiko na kuweka mikakati madhubuti ili kila mmoja wetu aingie kazini kuikomboa upya nchi nzuri ya Tanzania.

Hakuna mjomba fulani atakayekuja kutujengea nchi hii.

Time to wake up, and do so seriously & bravely!!!
 
Tanganyika Iko wapi? Katavi au
 
I guess I'm too fast to agree with you here. Acha tunyoroshwe kwanza mpaka dawa ituingie vizuri.

Akili zikirudi tutajipambania tu ila kwa sasa bado akili zipo likizo.
 

Kuirejea historia haina maana ya kulalamika lakini pia mtu aliejenga msingi, ndie anaamua uimara wa nyumba ambayo kama nayo ni dhoofu, hakuna wa kufanya repair bila kuivunja na kuisuka upya.

Mimi pia sio shabiki wa kumsubiri "Hero" Ila kutokana na structure na mfumo wa maisha ya watanzania wengi. Ni ngumu mabadiliko yatokee kutoka chini kwenda juu unless kizazi cha "kidumu chama" Kiondoke au la maisha yawe magumu kiasi tabaka la chini liiingie barabarani.

Kwa hiyo unachokiongelea nakielewa ila tofauti yetu ni moja. Wewe unaongelea mambo kutokana na watanzania wanavyotakiwa kuwa na mimi naongelea kutokana na watanzania walivyo. Hivyo tu mkuu
 
Sasa hiyo katiba mpya itapatikana vipi?? Yani mie leo ninufaike na Katiba iliyopo halafu leo hii niibadili hiyo katiba ili inibane nitakuwa mwendawazimu.
 
Tanzania inatakiwa ipate kiongozi aina ya Rais wa China,yani Rais awe jeuri but anayehakikisha sheria zinafuata.

Ili upate maendeleo kama nchi,ni lazima kuhakikisha sheria inakuwa msumeno kwa kila mtu.moja ya Tatizo kubwa linaloikumba nchi nyingi za Afrika ni rushwa.
Rushwa kuanzia juu mpaka chini,hii yote ni hakuna wa kumfunga paka kengele.
 
Mkuu wasomi wengi walikuwa wanaenda kusoma nje kwa kupelekwa na Serikali ya Nyerere na wengi wao walikua wanaenda kusoma vyuo vya Russia, Israel na China, Uingereza, na kwa miaka hiyo ya 1975 ilikua rahisi kusafisha udara kwasababu idada yao ilikua ni chache na mifumo yao haikua haijajichimbia kwenda mbali, tofauni na sasa ambapo Magufuli alishindwa kwasababu wana mtandao wametapaka ndani na nje kwa wingi ili kuwasafisha Magufuli aliitajika kukaa madaraka zaidi ya miaka 10 na anayempokea kijiti awe wa mfumo wake. KingineMagufuli kilichokua kinampa tabu ni kutokana na jamii aliyotoka hawakua sehemu za vyombo vya Usalama ndiyo shida ilipoanzia. Kwa mfano Heche akiwa Rais ataweza kuumaliza mtandao kwa urahisi kutokana na jamii aliyotoka itamsaidia kupambana na wanamtandao na kuua kabisa.
 
Mkuu mimj ndiyo Raisi nakuita wewe Mskamo wangu wa Raisi nakuambia sitaki kufanya kazi na wewe andika barua sasa hivi ya kujiuzulu ina maana utakataa?
 
Kweli Mkuu Nyerere alifata mifumo ya China na Russia kuunganisha Chama na Serikali kuwa kitu kimoja,ndiyo maana ukiwa mpinzani unaonekana adui na unahujumu nchi na lakini wao wakihujumu nchi hawaoni.
 
Mkuu mimj ndiyo Raisi nakuita wewe Mskamo wangu wa Raisi nakuambia sitaki kufanya kazi na wewe andika barua sasa hivi ya kujiuzulu ina maana utakataa?
Kinadharia inawezekana lakini kichama na kikatiba haiko hvo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…