Tusipochukua maamuzi magumu Taifa letu la Tanganyika litapotea kabisa

Nani wa kufanya mabadiliko ikiwa tiss Iko chini ya Dgis na mkubwa?

Unaongea na nani wachukue hatua?

Ni mabaka?

Ni wananchi?
 
Na Polepole anahesabu maneno yake, hhajavuka line kustahili asemacho Malcolm
 
Indeed, Crime Never Dies.
But surely Dead Criminals Do Not Offend.
SIMPLE SOLUTION: Less Criminals, Less Crime.
​
 
I beg to differ.

Lissu = JPM

Ndiyo maana hawapatani hadi kesho.

Ulishaona matokeo ya pande mbili zinazofanana katika sumaku?
 
KATAA WAHUNI, OKOA TANGANYIKA.✍️📌
 
Kuhusu Lissu kuwa mropokaji hilo nakataaa. Tena Lissu anamzidi sana Magufuli kwa sababu Lissu anapenda mapambano ya hoja. Lissu ni mwanademokrasia kweli na haamini kwenye kumuumiza mtu ili hoja yake ipate nguvu.
Katika hili hebu twende kwa ushahidi.

Mosi, Tundu Lissu aliwahi kuzua taharuki nchi nzima kwa kusema kwamba anachokifanya JPM kwenye RIPOTI ZA MAKINIKIA vilikuwa ni upumbavu na Prof Mruma aliandika Professorial Rubbish. Akatishia kwamba Tanzania itashitakiwa MIGA ilhali kesi ilipelekwa LCIA. Mwishowe ukweli ulifahamika kwamba ACACIA ilikuwa inafanya kazi Tanzania kama kampuni ndogo ya BARRICK bila kuwepo na Certificate of Compliance, huku wakikwepa kodi na kuiba madini kinyume na utaratibu wa kwenye mkataba.

Tanzania ilifanikiwa kuwalazimisha BARRICK, ambao ni wamiliki wa ACACIA kuifanya ACACIA itoe kesi LCIA kisha BARRICK yenyewe irejee kwenye meza ya mazungumzo. Kwenye INVESTMENT LAW, walichokifanya BARRICK na ACACIA kinaitwa TREATY SHOPPING, ambapo unatengeneza kampuni moja nchi nyingine na linamilikiwa na kampuni jingine la nchi nyingine, huku wakitumia vipengele vya kwenye Bilateral Investment Treaty (BIT) kuumiza nchi.

Aina ile ya kampuni ambalo BARRICK na ACACIA walitengeneza kisheria hiitwa MULTI-STOREY CORPORATION ambayo hutumika kukwepa kodi na kuhujumu nchi. Kisheria, wawekezaji wa nje tu ndiyo wanalindwa siyo wa ndani, lakini kwenye Multi-Storey Corporations, raia wa nchi husika wanaweza kwenda nchi nyingine na kuwapa watu mapesa halafu wakaja hapa nchini kama wawekezaji hewa, ila nyuma na wananchi wazawa. Ndicho tulichofanyiwa kwenye DP WORLD.

Tundu Lissu alikosea na mwisho wa siku kuna mwandishi wa habari alimtumia ujumbe kule Belgium, ambapo mwenyewe alikiri kwenye makundi ya WhatsApp kwamba "Haya kaka sawa, naona umeshinda". Sasa kama haukuwa UROPOKAJI, hiki ni NINI ???

Pili, mwaka 2017 Tundu Lissu ashawahi kuliongopea BUNGE zima na kuliaminisha taifa kwamba Zanzibari ni koloni la Tanganyika ambalo haliwezi kusaini mikataba yoyote ile ya kimataifa. Mzee Andrew Chenge akamtolea uvivu na kumwasha. Ikaonekana kwamba Zanzibar ina uwezo wa kuingia mikataba ya kimataifa hata kukopa fedha chini ya udhamini wa Serikali ya JMT. Kanuni za sheria za kimataifa bado zinaipa nafasi Zanzibar kutambulika kama DOLA (COMPOSITE STATE), hivyo inaweza ikaingia mikataba mikubwa tu ya kimataifa. Siku ile namsikiliza nikajiulizwa hivi ni kwamba Lissu hafahamu kabisa Principles of Public International Law. AU ni UZANDIKI AU ni UROPOKAJI TU ???

Haya MAWILI ni MAKUBWA, mengine sina muda kuyaandikwa kwa leo. Hili ni TATIZO, na endapo litaendelea kufugwa siku anakuwa kiongozi mkubwa hapa nchini anaweza kufanya kile ambacho Arthur Zimmerman aliifanyia Ujerumani mwaka 1917. Unamfahamu Arthur Zimmerman ??? Katafute jinsi UROPOKAJI wake ulivyoiponza Ujerumani.
​
 
100%✓
 
okay sawa .

ikiwa lissu atatoka gerezani na kuanza kumsema hp huku akimshukuru mketaji wake,
Basi jua hio ni kazi ya wana mtandao.ndio maana ra alihairisha press , wazee wamemwambia
wana plan nzuri so tulia kwanza.

na kwakua wa tz ni wasaulifu due elimu ya kukariri madesa na ulaji wa vyakula vibovu
ni wepesi wa kusahau. wataanza kumsikiliza lisu. hii movie tunaifuatilia kwa karibu.

lakini hata lisu mwenyewe ametumika sana na wana mtandao kumuhujumu jiwe.
na sisi sote tunalijua hilo, kwa hiyo huwezi sema Eti lissu yuko sehemu salama.

kama unataka kuwa salama timiza wajibu wako kwa kufuata sheria pasi na msukumo
toka kundi fulani.

ukweli na uwazi ni jambo muhimu sana kwenye jamii yoyote ile. ie South Korea maraisi wa hii nchi tume washuhudia wakiwajibishwa kwenye vyombo vya sheria. hapa tz?

tofauti kabisa na hapa tz, Rais hata akivunja katiba hastakiwa , ni katiba ya mwalimu Nyerere ,yeye mwenyewe alinukuliwa akisema kuwa tz ikipata Rais kichaa au dictator basi
wananchi watapata shida.

so unaweza kujiuliza how mwalimu atengeneze katiba ya kihuni namna hii, alikuwa na malengo gani kwa miaka 100 ya tz, alijua viongozi wa ccm ni Malaika ? ni wazi hakuwa mbunifu na muwajibikaji kwa anayoyafanya.

ulisikia maneno ya mwisho ya hp ? kwamba wahusika wote wa idara wasipoteze Ushahidi (ina maana hata hp yumo ndani) ili ile siku isiyo julikana , atakapo kuja kiongozi mwingine kila kitu kiwekwe mezani.
 
Ukweli mchungu huu
 
Tatizo lenu kubwa ni hili, kutafuta suluhu rahisi kwenye majawabu magumu.

Mzee Nyerere aliposema Tanganyika itaimeza Zanzibar, hakuwa mkweli kwa asilimia 100%. Aidha alikuwa ni mwoga, alifikia ukomo wa kufikiri au alikuwa na ajenda yake ya siri. Jambo ambalo hatupendi kulisema ni kwamba kisheria neno SERIKALI lina maana kubwa sana. Tunaposema serikali ya Tanganyika hatumaanishi chombo kingine (A New Entity) ila kufahamika kwa Tanganyika pamoja na uwezo watu wake kusimamia mambo yao (Historical Identity and Ability to decide our affairs).

Serikali ya Tanganyika ikiwepo siyo lazima tuunde SHIRIKISHO (A Federation). Duniani kote neno serikali humaanisha vitu vikuu viwili: Serikali Kuu (The Central Government) ambayo huwa inatambulika kimataifa kama msimamizi mkuu na mdhibiti wa dola, na Serikali Ndogo (Local Government), ambazo huongoza jamii husika kuanzia ngazi ya kijiji, kitongoji, tarafa, wilaya hadi mkoa.

KAMA MNAOGOPA SERIKALI TATU BASI FANYENI HAYA YAFUATAYO:
Federate at Local Levels.

Tengenezeni majimbo maalumu ndani ya Tanganyika ambayo yatakuwa yanajisimamia yenyewe chini ya WIZARA MAALUMU YA TAMISEMI. Tanganyika haitakuwa na Raisi au Waziri Mkuu, bali itakuwa ina chombo maalumu chini ya TAMISEMI ambacho kitasaidia kuratibu sera mbalimbali chini ya Uangalizi wa WAZIRI MWENYE DHAMANA.

Haya majimbo yatakuwa na wawakilishi wake kwenye BUNGE LA JMT, huku yakiweza kuchagua na viongozi wao wa maeneo husika ambao watasimamia maslahi ya wananchi wao. Hili la kulazimisha kwamba kila kitu kifanywe na Serikali na Bunge halina afya na litaendelea kuleta maneno.

Waruhusuni Watanganyika wapewe serikali zao (Semi-Autonomous) walau kwenye ngazi za majimbo, ambazo watazichagua wao, na zitasimamiwa na chombo maalumu chini ya TAMISEMI.TAMISEMI siyo suala la MUUNGANO hivyo tuanzie hapa. Mambo ya msingi ya Tanganyika hayatakiwi hata yaamuliwe hata na serikali ya Tanganyika bali watu wenyewe kwenye serikali zao (Local Governments), huku wakishirikiana na serikali ya JMT.
===============================================================
Mkiamua mnaweza kuigeuza TAMISEMI leo kuiita THE TANGANYIKA OFFICE, ambayo itasajili serikali za majimbo ambazo ni (Semi-Autonomous) kupitia, A Special Charter/ Act of Parliament. Hili likifanyika kutakuwa na ufanisi mkubwa mno kwenye utendaji. Kwanza kabisa hata makelele ya CHADEMA hayatakuwepo maana watakuwa wametingwa huku na kuwaachia CCM Serikali Kuu.

Lakini, pia ufisadi mwingi unasababishwa na kukosa udhibiti imara wa serikali ndogo (Local Government). Hizi serikali zikisajiliwa na kuanza kujitegemea kuna mambo mengi mno kama rushwa na uzembe vitapungua kwa kasi, na watu hawatadirikia kufanya ujinga. Mtapata wasomi hadi kwenye ngazi za vijiji wakifanya kazi kwasababu serikali za majimbo zitakuwa zinaweza kusimamia mapato yake.

Hebu tujaribu hili, nimelifuatilia sana na kutafiti na kuona kwamba linaweza kuzaa matunda makubwa. Tunaweza kuendelea kulifanyia tafiti.
​
 
Congratulations my friend you're enlightened.

Lissu is in a similar position which Nelson Mandela was in 1980's.
​
 
1975 kulikua na vyuo vikuu vingapi?
 
Walichokifanya kina Mzee Nelson Mandela na Desmond Tutu hakikuwa Transitional Justice, bali kitaalamu kilichofanyika tunaita APPEASEMENT. Japo kwa sehemu yao walijitahidi, kilichotakiwa kufanyika ni kuhakikisha Reparations are economic and monetary.

Mbali na kuuwawa, kunyang'anywa ardhi (Land Alienation) ndiyo changamoto kubwa ambayo iliwakuta weusi wa Afrika Kusini. Ilitakiwa serikali ihakikishe kwamba weusi wenye uwezo wa kuzalisha wanapewa ardhi au wanaingizwa kwenye umilikwaji wa pamoja na wakulima weuepe ambao wanamiliki utajiri mkubwa wa mashamba na migodi.

Kama TRUTH COMMISSION, imeshindwa kutoa Fair and Equittable Reparations to victims, basi hiyo ni APPEASEMENT, ambayo huishia kuleta huko mbele. Halafu, hata kama tunasamehe (Amnesty), wanaosamehewa ni wale waliofanya makosa ya kawaida, siyo makosa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu kama mauaji ya kimbari, utekeji, uuaji au utumwa. Hawa walitakiwa kufungwa na kunyongwa kama ilivyofanyika kule Nuremberg na Tokyo mwaka 1945.
​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…