Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Mwaka 2022/23 niliandika mada nzito sana kuhusu mambo yanayopaswa kufanywa bandarini kufuatia suala la kubadilishwa kila mara wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari.
Nashukuru pendekezo langu nililolitoa la kufanya bandari zetu kuendeshwa kwa sehemu kubwa kwa mfumo wa PPP (Serikali na sekta binafsi) limefanyiwa kazi na sasa tutaanza kuona matunda yake.
Leo naomba kuishauri kwa mara nyingine Serikali ya Tanzania baada ya kusikiliza hotuba ya Rais Samia jana akimpa maelekezo kamishna mpya wa TRA baada ya kumuapisha.
Rais wa Tanzania, kama una nia ya kweli kufanya mapinduzi makubwa katika makusanyo ya kikodi na kuhakikisha nchi inapata makusanyo yake ya kikodi inayostahili wala usihangaike kubadili Makamishna Wakuu wa TRA, we fanya hili tu
**Toa maelekezo kwa BOT ndani ya miaka 2 wahakikishe nchi inaondoka katika mfumo wa kutumia pesa taslimu kufanya malipo yote( cash economy). Malipo yote ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa yafanyike kwa njia ya kielektroniki. Wenye maduka wawe na mashine tu. Mtu akinunua bidhaa halipi kwa pesa taslimu. Anaswap kadi au analipa kwa simu au kwa ku scan barcode. Hili linaweza kuanza mikoa michache michache yenye uhakika wa mtandao na umeme na baadae kufanyika nchi nzima.
Hili likifanyika mamlaka za kodi hazitakuwa na haja ya kumfanyia mfanyabiashara makadilio ya kodi. Kila kinacholipwa kitakuwa kinaonekana na kodi inayopaswa kulipwa itaonekana na mfanyabiashara anailipa moja kwa moja TRA.
Ni wakati sasa tuambiane ukweli! Kwa hulka ya binadamu( Wizi, Ubinafsi na Ufisadi) kamwe tusitegemee kupata mapato tunayostahili endapo tutaendelea kutumia mfumo wa pesa taslimu( cash economy) kwenye uchumi wetu.
Lord denning,
Qatar
**Mada inayokuja itahusu nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi kwa Serikali na Viongozi wake