Tusipofanya haya kila siku tutabadili Kamishna wa TRA

Tusipofanya haya kila siku tutabadili Kamishna wa TRA

Kwamba bandari kupewa sekta binafsi lilikua pendekezo lako na likafanyiwa kazi?
Huu ni zaidi ya uongo. Ukiandika kitu kikatokea baada ya muda haimaanishi ushauri wako wewe umefanyiwa kazi, bali mipango hiyo ilikuwepo kabla. Mfano Kuna mtu humu aliandika kidata aondolewe TRA, nae leo atajisifia huo ulikua ni ushauri wake na umefanyiwa kazi?

Lakini pia ushauri uliotoa kuhusu TRA ni ushauri wa hovyo kulingana na nchi yetu ilivyo na namna watu wanavyopata vipato vyao
Acha wivu. Huo ndo ukweli

Mipango inaweza kuwepo ila unaweza kutoa ushauri leo ikaonekana ndo wakati sahihi wa kufanya jambo hilo na ikatekelezwa.

Usione wivu. Kikubwa ushauri unachukuliwa na kufanyiwa kazi
 
Ila pia tusiishie kwa wafanyabiasara tu, tuunganishe mifumo ya malipo na tin.
Account namba, mpesa, tigo pesa ziwe attached na tin.

Kusiwe na miamala yoyote ambayo ni ghost kwenye jicho la kodi, then urasimishaji ufanyike.

Haiwezekani upo mjini hapa na kodi unayolipa ni indirect tax tu ilihali wewe ni mc na kila weekend una sherehe.

Kila mtu ambaye hajaajiriwa tin yake isome business tin ili alipe direct tax pale anapotengeneza faida katika mihangaiko yake na asiwepo raia mtu mzima ambaye hana tin otherwise asiwe na access ya miamala.

Madalali na watoto wote wa mjini walipe kodi. Mtu kadalalia uuzwaji wa ghorofa M900 na kapewa M90 ya udalali halipi kodi ila mfanyabiashara ambaye mpaka atoboe kutengeneneza faida ya M10 keshahangaika na mamikopo wee na riba ndo kalundikiwa makodi yote.
Sahihi kabisa
 
Acha wivu. Huo ndo ukweli

Mipango inaweza kuwepo ila unaweza kutoa ushauri leo ikaonekana ndo wakati sahihi wa kufanya jambo hilo na ikatekelezwa.

Usione wivu. Kikubwa ushauri unachukuliwa na kufanyiwa kazi
Hadi hapa nimeijua tayari akili yako ilivyo
 
Africa needs strong institutions and strong systems not strong people.

Tukifanya haya yanayopendekezwa haya yote yataondoka.

Tunahitaji mifumo thabiti kudhibiti wizi sio watu. Watu wanapita na watu hawako consistent.
Wewe ni mzalendo. Hata wenzetu walioendelea wamewekeza Sana kwenye Technology ktk taasisi zao. Haya yote ni kutokana na maswala hayo.
Lakini pia tusisahahu kuwa tinahitaji mabadiliko makubwa Sana ya kiutamaduni, hasa kwenye eneo la ukweli na uwajibikaji. Mifuko nayo Kama itakuwa inaendeshwa na watu ambao ni corrupt haliwezi kutatua tatizo.
Ukiangalia kwa mawanda mapana unaweza kugundua hata kwenye sector binafsi Watanzania wengi hawafanyi vizuri, kitu kinachopelekea wenye taasisi zao kutafuta watu wa nje.
Unakuta mtu amepewa kazi ya kuhesabu bati kiwandani, mteja Ana order ya bati 100 bosi anapewa hesabu ya bati 60. Tatizo ni kubwa. Mtu anajiibia mpaka pesa yake mwenyewe ali mradi tu mkewe asijue katumizi yake yapoje. Eneo la ukweli na uwajibikaji ni tatizo.
 
Kwa hiyo kwa nini nchini zingine zimekuwa na mfumo wa cashless kufanya malipo na manunuzi na zingine hazina huo mfumo? Kwa nini tunaziona zingine zikienda kwenye mfumo wa cashless kwa maamuzi tu ya viongozi wao na sera za nchi?

Kwa nini sie tushindwe?

kawaulize nigeria walijaribu cashless society imewashinda, fanya utafiti kidogo khs cashless ya Nigeria na changamoto zake …
 
Wewe ni mzalendo. Hata wenzetu walioendelea wamewekeza Sana kwenye Technology ktk taasisi zao. Haya yote ni kutokana na maswala hayo.
Lakini pia tusisahahu kuwa tinahitaji mabadiliko makubwa Sana ya kiutamaduni, hasa kwenye eneo la ukweli na uwajibikaji. Mifuko nayo Kama itakuwa inaendeshwa na watu ambao ni corrupt haliwezi kutatua tatizo.
Ukiangalia kwa mawanda mapana unaweza kugundua hata kwenye sector binafsi Watanzania wengi hawafanyi vizuri, kitu kinachopelekea wenye taasisi zao kutafuta watu wa nje.
Unakuta mtu amepewa kazi ya kuhesabu bati kiwandani, mteja Ana order ya bati 100 bosi anapewa hesabu ya bati 60. Tatizo ni kubwa. Mtu anajiibia mpaka pesa yake mwenyewe ali mradi tu mkewe asijue katumizi yake yapoje. Eneo la ukweli na uwajibikaji ni tatizo.
Suala la uwajibikaji dawa yake ni katiba inayoweka misingi ya kuwawajibisha viongozi wa kisiasa pale wanapoikiuka au kufanya lolote kinyume chake
 
Mwaka 2022/23 niliandika mada nzito sana kuhusu mambo yanayopaswa kufanywa bandarini kufuatia suala la kubadilishwa kila mara wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari.

Nashukuru pendekezo langu nililolitoa la kufanya bandari zetu kuendeshwa kwa sehemu kubwa kwa mfumo wa PPP (Serikali na sekta binafsi) limefanyiwa kazi na sasa tutaanza kuona matunda yake.

Leo naomba kuishauri kwa mara nyingine Serikali ya Tanzania baada ya kusikiliza hotuba ya Rais Samia jana akimpa maelekezo kamishna mpya wa TRA baada ya kumuapisha.

Rais wa Tanzania, kama una nia ya kweli kufanya mapinduzi makubwa katika makusanyo ya kikodi na kuhakikisha nchi inapata makusanyo yake ya kikodi inayostahili wala usihangaike kubadili Makamishna Wakuu wa TRA, we fanya hili tu

**Toa maelekezo kwa BOT ndani ya miaka 2 wahakikishe nchi inaondoka katika mfumo wa kutumia pesa taslimu kufanya malipo yote( cash economy). Malipo yote ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa yafanyike kwa njia ya kielektroniki. Wenye maduka wawe na mashine tu. Mtu akinunua bidhaa halipi kwa pesa taslimu. Anaswap kadi au analipa kwa simu au kwa ku scan barcode. Hili linaweza kuanza mikoa michache michache yenye uhakika wa mtandao na umeme na baadae kufanyika nchi nzima.

Hili likifanyika mamlaka za kodi ha,zitakuwa na haja ya kumfanyia mfanyabiashara makadilio ya kodi. Kila kinacholipwa kitakuwa kinaonekana na kodi inayopaswa kulipwa itaonekana na mfanyabiashara anailipa moja kwa moja TRA.

Ni wakati sasa tuambiane ukweli! Kwa hulka ya binadamu( Wizi, Ubinafsi na Ufisadi) kamwe tusitegemee kupata mapato tunayostahili endapo tutaendelea kutumia mfumo wa pesa taslimu( cash economy) kwenye uchumi wetu.

Lord denning,
Qatar

**Mada inayokuja itahusu nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi kwa Serikali na Viongozi wake
Hapo Upo sawa
 
usijali cashless inakuja post samia, nina uhakika P.Mpango (PhD) 2025/35 ataintroduce cash less kwa maana ndivyo globalist walivyopanga …
Suala sio mtu, bali ni ni kuanzisha mfumo na kuhakikisha unafanya kazi.

Hiyo post Samia umesema wewe!! Ushauri wangu usiweke mategemeo sana kwa mwanadamu. Utakuja kuwa dissapointed vibaya sana.

Chama kimeshasema 2025-30 ni Samia, hayo mategemeo yako yanaweza kukufanya uzimie isipokuwa hivyo!
 
Lord Denning ni jina kubwa sana katika tasnia ya sheria, nilitarajia ntakuta "mawe" ya sheria
 
Back
Top Bottom