Tusipofanya haya kila siku tutabadili Kamishna wa TRA

Mwaka 2022/23 niliandika mada nzito sana kuhusu mambo yanayopaswa kufanywa bandarini kufuatia suala la kubadilishwa kila mara wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari.

Nashukuru pendekezo langu nililolitoa la kufanya bandari zetu kuendeshwa kwa sehemu kubwa kwa mfumo wa PPP (Serikali na sekta binafsi) limefanyiwa kazi na sasa tutaanza kuona matunda yake.

Leo naomba kuishauri kwa mara nyingine Serikali ya Tanzania baada ya kusikiliza hotuba ya Rais Samia jana akimpa maelekezo kamishna mpya wa TRA baada ya kumuapisha.

Rais wa Tanzania, kama una nia ya kweli kufanya mapinduzi makubwa katika makusanyo ya kikodi na kuhakikisha nchi inapata makusanyo yake ya kikodi inayostahili wala usihangaike kubadili Makamishna Wakuu wa TRA, we fanya hili tu

**Toa maelekezo kwa BOT ndani ya miaka 2 wahakikishe nchi inaondoka katika mfumo wa kutumia pesa taslimu kufanya malipo yote( cash economy). Malipo yote ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa yafanyike kwa njia ya kielektroniki. Wenye maduka wawe na mashine tu. Mtu akinunua bidhaa halipi kwa pesa taslimu. Anaswap kadi au analipa kwa simu au kwa ku scan barcode. Hili linaweza kuanza mikoa michache michache yenye uhakika wa mtandao na umeme na baadae kufanyika nchi nzima.

Hili likifanyika mamlaka za kodi hazitakuwa na haja ya kumfanyia mfanyabiashara makadilio ya kodi. Kila kinacholipwa kitakuwa kinaonekana na kodi inayopaswa kulipwa itaonekana na mfanyabiashara anailipa moja kwa moja TRA.

Ni wakati sasa tuambiane ukweli! Kwa hulka ya binadamu( Wizi, Ubinafsi na Ufisadi) kamwe tusitegemee kupata mapato tunayostahili endapo tutaendelea kutumia mfumo wa pesa taslimu( cash economy) kwenye uchumi wetu.

Lord denning,
Qatar

**Mada inayokuja itahusu nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi kwa Serikali na Viongozi wake
Kwakifupi Hakuna haja ya TRA tutaokoa fedha nyingi kuwalipa wafanyakazi wa tra pia tutapanua wigo wa makusanyo ya Kodi
 
Kwa kweli jana Mhe. Rais kaniangusha. Kwa alivyomsifia kidata vile basi hakukuwa na sababu ya kumuondoa.

Hata hivyo hata awekwe malaika pale TRA hatuwezi kufikia katika kiwango tunachopaswa kufikia katika makusanyo ya kikodi.

Wizi utaendelea na wafanyakazi wa TRA wataendelea kuwa na ukwasi unaotokana na ufisadi.

Tufanye mfumo wetu wa ununuzi na uuzaji wa bidhaa kuwa wa kiektroniki na hapo ndipo tutaweza kukata mzizi wa fitna.
kwani wenzetu wanatumia digital/online pekee au mkazo ni electronic na cash transaction ipo pia. kwa uchumi wetu wa- rural economy ni vigumu kutegemea uchumi wa online payment pekee.
 
Tukiamua tunaweza!

Ni kukomaa tu hakuna lisilowezekana!

Internet inapatikana hadi vijijini saivi. Bibi yangu ana hadi WhatsApp saivi. Umeme upo sehemu nyingi kwa sasa Tanzania almost vijiji vyote. Kwa hiyo inawezekana!
 
Mfumo wa fedha nchi hii ni bado wa kizamani ndg!
Mfano ndogo tu, dunia ina miongo mitatu tangu mageuzi ya internet, Ila kuna maeneo mengi tu hata kupiga simu ni tabu; maeneo mengine ndani tu ya nyumba kuna sehemu moja tu internet inashika; ...
Bado sijagusia black market. Kuna tofauti kubwa baina ya ndoto na uhalisia
 
Mbona malipo ya Serikali imewezakana?

Mbona saivi tunalipa malipo ya Serikali kwa control No?

Hakuna lisilowekezana. Ni kuamua na kufanya tu! Akili ya mtu mweusi ndo uchawi wake wa kwanza kwake kutoendelea!
 
Systems za kizamani za miaka ya 60 ndizo zinazozorotesha na kudumaza maendeleo ya kiuchumi ya taifa hili.
Dunia ina evolve kwa kasi kila kukicha while nchi yetu bado ipo na inaendeshwa kama ilipata uhuru jana.

Ufisadi na rushwa unadhibitika kwa asilimia 90+ kama nchi itaamua kuswutch to full Technology.

Huu utakuwa mwanzo mzuri. Only kama atatokea mtu mwenye uwezo wa kuona kitu obvious kama hicho. Kwa viongozi waliopo sasa usitegemee chochote cha maana.

Badala ya kudeal na mambo crucial na ya uzito kama hayo, wapo bize kupeleka pesa kwenye timu za mpira na campaign za vyoo.

It's an optimistic dream.
 
Mwaka 2022/23 niliandika mada nzito sana kuhusu mambo yanayopaswa kufanywa bandarini kufuatia suala la kubadilishwa kila mara wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari.

Nashukuru pendekezo langu nililolitoa la kufanya bandari zetu kuendeshwa kwa sehemu kubwa kwa mfumo wa PPP (Serikali na sekta binafsi) limefanyiwa kazi na sasa tutaanza kuona matunda yake.

Leo naomba kuishauri kwa mara nyingine Serikali ya Tanzania baada ya kusikiliza hotuba ya Rais Samia jana akimpa maelekezo kamishna mpya wa TRA baada ya kumuapisha.

Rais wa Tanzania, kama una nia ya kweli kufanya mapinduzi makubwa katika makusanyo ya kikodi na kuhakikisha nchi inapata makusanyo yake ya kikodi inayostahili wala usihangaike kubadili Makamishna Wakuu wa TRA, we fanya hili tu

**Toa maelekezo kwa BOT ndani ya miaka 2 wahakikishe nchi inaondoka katika mfumo wa kutumia pesa taslimu kufanya malipo yote( cash economy). Malipo yote ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa yafanyike kwa njia ya kielektroniki. Wenye maduka wawe na mashine tu. Mtu akinunua bidhaa halipi kwa pesa taslimu. Anaswap kadi au analipa kwa simu au kwa ku scan barcode. Hili linaweza kuanza mikoa michache michache yenye uhakika wa mtandao na umeme na baadae kufanyika nchi nzima.

Hili likifanyika mamlaka za kodi hazitakuwa na haja ya kumfanyia mfanyabiashara makadilio ya kodi. Kila kinacholipwa kitakuwa kinaonekana na kodi inayopaswa kulipwa itaonekana na mfanyabiashara anailipa moja kwa moja TRA.

Ni wakati sasa tuambiane ukweli! Kwa hulka ya binadamu( Wizi, Ubinafsi na Ufisadi) kamwe tusitegemee kupata mapato tunayostahili endapo tutaendelea kutumia mfumo wa pesa taslimu( cash economy) kwenye uchumi wetu.

Lord denning,
Qatar

**Mada inayokuja itahusu nidhamu katika matumizi ya kodi za wananchi kwa Serikali na Viongozi wake
Ni unafiki kumtoa kamishina TRA na kuipongeza serikali kwa kuongeza ukusanyaji kodi hypocrisy 😑
 
Systems za kizamani za miaka ya 60 ndizo zinazozorotesha na kudumaza maendeleo ya kiuchumi ya taifa hili.
Dunia ina evolve kwa kasi kila kukicha while nchi yetu bado ipo na inaendeshwa kama ilipata uhuru jana.

Ufisadi na rushwa unadhibitika kwa asilimia 90+ kama nchi itaamua kuswutch to full Technology.

Huu utakuwa mwanzo mzuri. Only kama atatokea mtu mwenye uwezo wa kuona kitu obvious kama hicho. Kwa viongozi waliopo sasa usitegemee chochote cha maana.

Badala ya kudeal na mambo crucial na ya uzito kama hayo, wapo bize kupeleka pesa kwenye timu za mpira na campaign za vyoo.

It's an optimistic dream.
You nailed it
 
Pamoja na ushauri mzuri unaotolewa humu. Bado viongozi wetu wa kisiasa wanaendelea kuunda Tume badala ya kuchukua hatua.
 
Tume zinaundwa nyuma ya mikamera majibu ya tume nyuma ya pazia
Tunapoteza muda na rasilimali tu kuunda matume kila siku wakati matatizo hanajulikana na hata suluhisho kwa hayo matatizo lipo na linajulikana.

Badala ya kuchukua hatua wanapoteza muda tu!
 
Hiyo inaitwa zuga fala kwa jamu, kitaalamu, (expecting results from what you know), kutegemea matokea chanya kumbe unafahamu hayawezi kuwa chanya ama unayajua
 
Siasa ni sanaa yaani unatengeneza tatizo kisha unajiweka kando unaunda tume ichunguze tatzo ulilotengeneza kisha ije iripoti kwako.
 
Back
Top Bottom