Tusipofanya haya kila siku tutabadili Kamishna wa TRA

Daaah hakika unaona mbali.....
 
Kumbe Kuna vitu nilikuwa sivijui.....lakini Kwa wazo hili tutaomba poo.
 
Niseme kitu.
Nisubiri mada inayokuja
 
Changamoto mda mwingine kodi sio rafiki. Ndio mana tunaona wafanya biashara wanakwepa
 
Daaah hakika unaona mbali.....
Teknolojia imerahisisha kila kitu siku hizi. Ni kutumia tu teknolojia. Bado tuna operate kizamani sana kwenye kukusanya kodi.

Tunaweka wenyewe mianya ya kuendekeza rushwa na kutopata mapato ya kikodi sahihi
 
Hilo la cashless payment ndiyo nimekuelewa! Yamenikuta hapa India nina account ya uanafunzi wiki iliyopita nikaenda na cash bank kudeposit walichoniuliza hiyo pesa umeitoa wapi?? Nikajibu kwa rafiki yangu, wakasema tunakata trasaction online ili kumonitor transaction kwenye account. Narudi kwenye point hii hata wafanyabiashara wasiruhusiwe kwenda kuweka pesa cash, wafanye transaction online ili kumonitor, akija na cash aje na kitabu cha mauzo, kihakikiwe kama malipo yanatally na cash anayodepost.
 
Hiyo itasaidia kwa kiwango kidogo sana. haitomaliza tatizo.

Solution ni sheria ya kifo tu kwa wabachirifu wa mali za serikali. Kama China.

Hakuna nchi duniani ilikuwa corrupted kama israel, hhawamsahau Waziri wao mkuu wa kike alilimaliza hilo tatizo ndani mwezi mmoja tu. Alifanya nini?

Aliunda kikosi kazi cha wasiojulikana. Wakawa wakijuwa fulani anafanya ufisadi, anaandikiwa hukumu kabisa na yote aliyoyafanya, anauliwa kimya kimya, nakalainapelekwa kwa watu wake,nakala inapelekwa vyuombo vya habari na nakala inapelekwa mahakamani ya kwanini kauliwa.

Waliuliwa namba hihyo kama watu saba tu, baada ya mwezi tu nchi ikawa haian rushwa na kila mtu hataki mchezo wa kodi wala ubadhirifu, maana walichomolewa kila ufisadi mmoja mmoja wakauliwa. Mpaka leo mama anakufa mama yule anakataa kuwa yeye alikuwa hajuwi nani wanaofanya hayo, hakuna aliyetiwa siri mpaka leo na hawajulikani kina nani lakini watu wanaamini ni siri ya mama na ukosi kazi chake alichokiamini.
 
Sahihi kabisa. Nchi za wenzetu ndo mana ni ngumu sana kusikia Wafanyabiashara wanakwepa kodi sijui wanalalamika kutozwa zaidi maana kila unachouza na kununua kinarekodiwa na kodi inakatwa huko huko juu kwa juu
 
Nakubaliana na wewe!
Tuanzie hapa alafu twende kwenye Katiba na Sheria kali dhidi ya Wizi na Ubadhirifu
 
Umenena vyema sana mkuu. Lakini hiyo mianya ya upigaji imewekwa na kuachwa makusudi na viongozi wenyewe. Sio rahisi wakubali kujizibia mirija ya ulaji, Kwa hiyo ushauri wako hawatauzingatia. Na kama watauzingatia itakuwa ni Bahati Kwa nchi yetu maana ni ushauri unaofaa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…