Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Habari ya Kenya? Jueni tu Tanzania haijalala, mipango yenu ya kuiua Ngorongoro ili Kenya mchukue soko la Utalii haitafanikiwa
Wenzako wengine wanasema wamasai waondoke sababu wanaliwa na simba, we unasema simba wanakimbia,nadhani mnge jiorganizes kwanza ili muwe na kauli moja.
 
Hata hao Wamaasai walihamishwa kutoka Serengeti(Siringet) kuja hapo ambapo ninyi kwa tamaa zenu mnataka waondoshwe. Inatakiwa ikishindikana co-existence kati ya watu na wanyamapori pale, basi wanyamapori na shughuli zote za utalii ndio zingehamishiwa Siringet.
 
Habari ya Kenya? Jueni tu Tanzania haijalala, mipango yenu ya kuiua Ngorongoro ili Kenya mchukue soko la Utalii haitafanikiwa
Wakenya wana akili. Wanaweza kupromote utalii bila kuiua serengeti. Wakenya wahangaike na ngoma zisizokuwa na utu wala kukubali kutofautiana. Sisi wabongo bado ni primitive sana. Hakuna tofauti wa mwenye elimu na asiyekuwa nayo. Tunatanguliza njaa na tamaa mbele.
 
Mapori yote yaliyojaa Tanzania si wapelekwe uko wamasai, waishi na ng’ombe wenziwao
 
Mapori yote yaliyojaa Tanzania si wapelekwe uko wamasai, waishi na ng’ombe wenziwao
Kwanini msiwapeleke Wanyama? Kwanini muone shida wao kuishi pale, halafu wanyama wahamishwe? Wanyama wapelekwe Tarangire, Lake Manyara na Serengeti(Siringet)?
 
Kama ambavyo mababu zake na Manongi waliona Same na milima ya upare ndio the best kwa maisha yao, vile vile Wamaasai waliona Ngorongoro ndio the best kwa maisha yao pamoja na uwepo wa wanyamapori wakali kama Simba, Tembo na Nyati.
Wamaasai waliipata Ngorongoro kwa kupigana na jamii zingine. Manake waliona ndio the best kwao. Ndio ya kufa na kupona kwao.
 
Kama jibu unalo why kelele nyingi kiasi hicho, and how wakulya na waikoma hawakupiga kelele kama hizi zenu?.
 
Kama jibu unalo why kelele nyingi kiasi hicho, and how wakulya na waikoma hawakupiga kelele kama hizi zenu?.
Eneo walilohamishiwa haikuwa na maisha mseto na hifadhi. Mbona huelewi? Huna concept ya kinachogombaniwa hapa?
Hilo eneo haligombaniwi tu. Kuna sababu. Jielimishe kwanza. Soma sana. Usiwe kama Kitenge.
 
kama kisiwa cha Zanzibar kingekuwa na wanyama ambao wangekuwa wanatoweka kulingana na kuongezeka kwa shughuli za binadamu basi tungesema binadamu wahamishwe
Hujui kuwa human activities in Zanzibar inahatarisha uhai wa kisiwa hicho? Mfano, sasa hivi mchanga wanaagiza toka bara. Je, ni salama kwa kwa kisiwa?
 

Kuishi na wanyama hao ilikuwa zamani kabla ya population ya wamasai kuongezeka.. sasa hiv idadi ya wamasai waishio huko ngorongoro inaongezeka na hii ni hatarishi sana maana wanaweza kudhurika na hao wanayama wakali
 
Kuishi na wanyama hao ilikuwa zamani kabla ya population ya wamasai kuongezeka.. sasa hiv idadi ya wamasai waishio huko ngorongoro inaongezeka na hii ni hatarishi sana maana wanaweza kudhurika na hao wanayama wakali
Waaarabu wanataka eneo la kuwinda. Wanyama watakwisha hadi Serengeti. Uongozi wa Juu wa Nchi uwe makinj sana katika hili.
 
Mimi nashauri tena kwa mara nyingine watu wote wahamishwe ndani ya Ngorongoro crater sio wamasai peke yao watu wote na mifugo yao. Wafanyakazi wa NCCA wote, wafanyakazi wa mahoteli na lodges wote, watalii wote, magari yote, karakana zote zihamishwe, kiruo cha polisi, shule zote. Yaani huduma zote za binadamu zifanyike nje ya crater. Watalii wawe wanaingia kutalii na kurudi kulala nje ya crater hivyo hivyo wafanyakazi wote. Wamasai wahamishiwe mapori mengine vinginevyo baada ya miaka michache ijayo hakutakuwa na ngorongoro crater tena . Machinga wa kimasai wapo huko wanauza magadi, asali na shanga. Chonde chonde jamani hoteli zote zibomolewe au zitoe huduma ya chakula tu basi. Mtu yoyote akitoa kibali cha kujenga hoteli ndani ya crater anyongwe hadi kufa
 
Hata wakikaa wanyama wakapotea tutafaidika nini? Hili jambo sio la kisiasa. Tuliangalie vizuri kwa interest za Taifa letu
Interests za aina hio hazijawahi kuwa za taifa bali za Royal families zilizopo kwenye System!

Hao wamasai wanatakiwa waondolewe sababu eneo lishauzwa uarabuni!
 
Waaarabu wanataka eneo la kuwinda. Wanyama watakwisha hadi Serengeti. Uongozi wa Juu wa Nchi uwe makinj sana katika hili.
Uongozi wa juu ni sawa na kichwa cha Mwendawazimu kwa sasa! Kila mtu anajifunzia kunyoa tu ile structure ya uongozi ni kama haipo.

Sasa mnafukuza wamasai kwa sababu watafanya population ya wanyama ipungue sababu watakimbia eneo ila at the same time kuna hoteli za kitalii ndani ya hifadhi, kuna ofisi ndani ya hifadhi, on top of all mnataka eneo ambalo wamasai wapo muwaondoe halafu mulete warabu waje kufanya poaching!

Laiti kama Nyerere angefufuka huko alipo leo angeweza kuzirai!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…