Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Tusipofanya sasa, Tutajuta Milele, ni lazima Wamasai waondoke Ngorongoro

Habari ya Kenya? Jueni tu Tanzania haijalala, mipango yenu ya kuiua Ngorongoro ili Kenya mchukue soko la Utalii haitafanikiwa
Wenzako wengine wanasema wamasai waondoke sababu wanaliwa na simba, we unasema simba wanakimbia,nadhani mnge jiorganizes kwanza ili muwe na kauli moja.
 
Bahati mbaya hutaki kulisha chakula ubongo wako kujua kabila gani liliwahi kuamishwa toka hifadhini kupelekwa eneo lingine.

Ila kwa sababu tecknolojia imekuwa kwa kasi kwenye umri wenu ndiposa mnaona maasai wanaonewa although kuna Watanzania wengine huko nyuma waliwahi kuamishwa na HAKUKUWEPO kelele kama hizi.

Hata hao unaopigia kelele hawakuwepo pale bali walihamishiwa pale, don't ask you're self but give brain work!.
Hata hao Wamaasai walihamishwa kutoka Serengeti(Siringet) kuja hapo ambapo ninyi kwa tamaa zenu mnataka waondoshwe. Inatakiwa ikishindikana co-existence kati ya watu na wanyamapori pale, basi wanyamapori na shughuli zote za utalii ndio zingehamishiwa Siringet.
 
Habari ya Kenya? Jueni tu Tanzania haijalala, mipango yenu ya kuiua Ngorongoro ili Kenya mchukue soko la Utalii haitafanikiwa
Wakenya wana akili. Wanaweza kupromote utalii bila kuiua serengeti. Wakenya wahangaike na ngoma zisizokuwa na utu wala kukubali kutofautiana. Sisi wabongo bado ni primitive sana. Hakuna tofauti wa mwenye elimu na asiyekuwa nayo. Tunatanguliza njaa na tamaa mbele.
 
Kwa nini wanaharakati wanafurahia binadamu wenzetu kuishi kama wanyama? Mwanadamu amepita stage nyingi za maendeleo kuanzia
Dryopithecus,
Ramapithecus,
Australopithecus,
Homo Erectus,
Homo Sapiens na hatimaye
Civilization

Kwa nini tunapenda watanzania wenzetu wabakie kama Sanaa ya kutazamwa na watalii? Wamasai watoke tu Ngorongoro
Mapori yote yaliyojaa Tanzania si wapelekwe uko wamasai, waishi na ng’ombe wenziwao
 
Mapori yote yaliyojaa Tanzania si wapelekwe uko wamasai, waishi na ng’ombe wenziwao
Kwanini msiwapeleke Wanyama? Kwanini muone shida wao kuishi pale, halafu wanyama wahamishwe? Wanyama wapelekwe Tarangire, Lake Manyara na Serengeti(Siringet)?
 
Kama ambavyo mababu zake na Manongi waliona Same na milima ya upare ndio the best kwa maisha yao, vile vile Wamaasai waliona Ngorongoro ndio the best kwa maisha yao pamoja na uwepo wa wanyamapori wakali kama Simba, Tembo na Nyati.
Wamaasai waliipata Ngorongoro kwa kupigana na jamii zingine. Manake waliona ndio the best kwao. Ndio ya kufa na kupona kwao.
 
Hata hao Wamaasai walihamishwa kutoka Serengeti(Siringet) kuja hapo ambapo ninyi kwa tamaa zenu mnataka waondoshwe. Inatakiwa ikishindikana co-existence kati ya watu na wanyamapori pale, basi wanyamapori na shughuli zote za utalii ndio zingehamishiwa Siringet.
Kama jibu unalo why kelele nyingi kiasi hicho, and how wakulya na waikoma hawakupiga kelele kama hizi zenu?.
 
Kama jibu unalo why kelele nyingi kiasi hicho, and how wakulya na waikoma hawakupiga kelele kama hizi zenu?.
Eneo walilohamishiwa haikuwa na maisha mseto na hifadhi. Mbona huelewi? Huna concept ya kinachogombaniwa hapa?
Hilo eneo haligombaniwi tu. Kuna sababu. Jielimishe kwanza. Soma sana. Usiwe kama Kitenge.
 
kama kisiwa cha Zanzibar kingekuwa na wanyama ambao wangekuwa wanatoweka kulingana na kuongezeka kwa shughuli za binadamu basi tungesema binadamu wahamishwe
Hujui kuwa human activities in Zanzibar inahatarisha uhai wa kisiwa hicho? Mfano, sasa hivi mchanga wanaagiza toka bara. Je, ni salama kwa kwa kisiwa?
 
Kabla ya kuandika huu upupu ungejiuliza wamasai wameishi na hao wanyama Kwa miaka mingapi? Hivi huko Kenya wanakohamia hakuna "wamasai"?

Wakiwapa fisi mizoga Yao shida nini Kwako? Mbona wapo wanaochoma Wapendwa wao kwa moto? Ni life style Yao.

Tukiwatoa wamasai tunaweka waarabu, CCM ni mashetani aiseeee

Kuishi na wanyama hao ilikuwa zamani kabla ya population ya wamasai kuongezeka.. sasa hiv idadi ya wamasai waishio huko ngorongoro inaongezeka na hii ni hatarishi sana maana wanaweza kudhurika na hao wanayama wakali
 
Kuishi na wanyama hao ilikuwa zamani kabla ya population ya wamasai kuongezeka.. sasa hiv idadi ya wamasai waishio huko ngorongoro inaongezeka na hii ni hatarishi sana maana wanaweza kudhurika na hao wanayama wakali
Waaarabu wanataka eneo la kuwinda. Wanyama watakwisha hadi Serengeti. Uongozi wa Juu wa Nchi uwe makinj sana katika hili.
 
Amani iwe nanyi

Kama kichwa cha uzi kinavyosema, Kama Mtanzania ninayeipenda nchi yangu, ninayejali maendeleo ya Watanzania wote vizazi na vizazi, leo nasema kwa Sauti moja, Kama tunajali maendeleo ya Tanzania yetu, Ni lazima wamasai waondoke Ngorongoro ili lile eneo liendelee kuwa na wanyama wengi na kuvutia watalii ambao ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato kwa Taifa letu

Kwa nini nasema haya?

1. Ngorongoro ni moja ya sehemu chache hapa Tanzania ambazo mtalii ana uhakika wa kuona wanyama walio kwenye hatari ya kupotea Duniani yaani Tembo, Faru, Simba, Nyati na Chui.

Nimefika ngorongoro kusema ukweli hadi Tour guides wanakwambia hivi karibuni imekuwa ngumu sana kuwaona baadhi ya hawa wanyama na sio tu hawa bali hata wanyama wengine ambao huko mwanzoni walikuwa ni wengi na wanaonekana kirahisi na kuvutia watalii wengi na kuongeza mapato mf pundamilia, pofu na wengineo. Hii ni kwa sababu wanadamu wameongezeka sana Ngorongoro na asili ya wanyama pori ni kuwa hawapendi kuchangamana na binadamu na shughuli za kibinadamu zikizidi huwa wanahama.

2. Kuna taarifa za uhakika kuwa Wanyama wanaohama Tanzania wanahamia upande wa pili yaani Kenya hivyo Kenya anafaidika kwa kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu Ngorongoro ambazo zinahamishia wanyama wetu Kenya. Hii ni hatari sana kwa uchumi wa Tanzania kwa sababu siku si nyingi, Watalii hawataona umuhimu wa kuja Ngorongoro na hivyo kwenda Kenya na kufanya nchi yetu kukosa Mapato.

3. Kuna taarifa za uhakika pia kuwa Wamasai waishio Ngorongoro hawana hata makabuli. Hivyo ikitokea mmasai amefariki anaachwa aliwe na fisi na mbweha. kibinadamu hii si sawa.

Napenda kumaliza kwa kusema imefika wakati sasa kwa maslahi mapana ya Tanzania, Wamasai wahamishwe Ngorongoro. Eneo hili ni nyeti na Tanzania nzima tunalitegemea kimapato. Likiangamia, Tanzania imeangamia. Ni wakati sasa Fedha zinazotengwa kuwalisha wamasai takribani bilioni 3-4 kwa mwaka zielekezwe sasa kuwajengea makazi ya kudumu wamasai hawa eneo jingine na kuwapatia teknolojia ya kufuga wanyama wachache tena kibiashara na kuachana na Maisha yale ya kijima

Naomba kuwasilisha!
Mimi nashauri tena kwa mara nyingine watu wote wahamishwe ndani ya Ngorongoro crater sio wamasai peke yao watu wote na mifugo yao. Wafanyakazi wa NCCA wote, wafanyakazi wa mahoteli na lodges wote, watalii wote, magari yote, karakana zote zihamishwe, kiruo cha polisi, shule zote. Yaani huduma zote za binadamu zifanyike nje ya crater. Watalii wawe wanaingia kutalii na kurudi kulala nje ya crater hivyo hivyo wafanyakazi wote. Wamasai wahamishiwe mapori mengine vinginevyo baada ya miaka michache ijayo hakutakuwa na ngorongoro crater tena . Machinga wa kimasai wapo huko wanauza magadi, asali na shanga. Chonde chonde jamani hoteli zote zibomolewe au zitoe huduma ya chakula tu basi. Mtu yoyote akitoa kibali cha kujenga hoteli ndani ya crater anyongwe hadi kufa
 
Hata wakikaa wanyama wakapotea tutafaidika nini? Hili jambo sio la kisiasa. Tuliangalie vizuri kwa interest za Taifa letu
Interests za aina hio hazijawahi kuwa za taifa bali za Royal families zilizopo kwenye System!

Hao wamasai wanatakiwa waondolewe sababu eneo lishauzwa uarabuni!
 
Waaarabu wanataka eneo la kuwinda. Wanyama watakwisha hadi Serengeti. Uongozi wa Juu wa Nchi uwe makinj sana katika hili.
Uongozi wa juu ni sawa na kichwa cha Mwendawazimu kwa sasa! Kila mtu anajifunzia kunyoa tu ile structure ya uongozi ni kama haipo.

Sasa mnafukuza wamasai kwa sababu watafanya population ya wanyama ipungue sababu watakimbia eneo ila at the same time kuna hoteli za kitalii ndani ya hifadhi, kuna ofisi ndani ya hifadhi, on top of all mnataka eneo ambalo wamasai wapo muwaondoe halafu mulete warabu waje kufanya poaching!

Laiti kama Nyerere angefufuka huko alipo leo angeweza kuzirai!
 
Back
Top Bottom