Tusipokuwa Makini, Kauli ya Nyerere ya Wabara na wale Wazanzibar inaanza kidogo kidogo

Tuanze na hili Tanganyika iko wapi? Naona mnaongelea kitu ambacho hakipo
 
wakifanya hivyo wamevunja sheria gani? unafikiri hawajui? pia, kuwa mkweli kabisa, muungano kwako wewe mtu wa bara una faida gani? wenzetu wanamiliki ardhi bara na wanaweza kufanya chochote ambayo wewe unafanya, pia wana haki ya kuwa wabunge huku na kule, na urais pia wana haki ya kuwa marais huku. Mwinyi alishawahi kuwa rais wa zanzibar na akawa rais wa bara. hakuna mtanganyika hata mmoja aliwahi kuwa rais wa zanzibar, basi tuache hiyo, hakuna mtu wa bara anastahili kumiliki ardhi zanzibar, wewe uliyepakana kiwanja na mzanzibar hapa Dsm ukienda kule unamiliki ardhi kama mwekezaji. sasa sema kwa moyo wako bila unafiki, muungano huu kwako wewe una faida gani? si una faida kwa wazanzibar peke yao? na kama uliingiwa ili waarabu wasirudi au kwa maslahi ya mabeberu, hayo maslahi yalishaishaga kitambo sana, chuki waliyokuwa nayo wabantu wa zanzibar dhidi ya sultan na waarabu iliishaga na sasaivi majority wa wazanzibar wanapenda kujiunga na waarabu ambao wengi ni ndugu zao. sema tukusikie na acha kutisha watu as if wewe unamiliki hii nchi au una mamlaka kuamulia watu maisha na nini cha kusema. udictator peleka kwenye familia yako uku nje kwa wengine utavuliwa suruari.
 
Msiwe mnapenda kuwa waongo.

Ni nani ambaye wakati wa utawala wa Nyerere aliyefungwa maisha kwa eti kuusema vibaya Muungano?

Sikuwahi kusikia kuwa kuna mwananchi wa kawaida amechukuliwa hatua yeyote eti ameusema vibaya Muungano. Mwalimu alipenda sana hoja zenye nguvu. Viongozi waliotaka Zanzibar kuwa na uhuru zaidi kwenye Muungano, waliondolewa kwenye nafasi zao za uongozi, na siyo kufungwa maisha. Huo ni uwongo mkubwa.
 
Hv unakumbuka alichofanyiwa Aboud Jumbe????
 
Ishu hii imefikia mahali hapo coz hata rais ajatoa tamko lake kuhus hili jambo sijui nini maane yake kuwa hivyo mpaka sasa
 
kuna watu wamekaa wanafikiri wakili Mwabukusi na Lisu hawajui wanachokiongea, na kwamba hawajajiandaa kujibu mashtaka mahakamani. kwa kifupi, maneno yao wanayachagua kwa umakini sana na wanajua hata wakishitakiwa wataishinda serikali mahakamani. waaacheni.
 
Halafu wanataka tuwe pamoja kwa lipi wakati wanajitenga wao wenyewe ?

Wakauze na Nungwi kwao huko wasianze kutuletea uswahili wao.
Nani amekudanganya kuwa wazanzibari wanataka kuwa pamoja na nyinyi mbona huo muungano wao wameukataa muda mrefu nyinyi ndio munawalazimisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…