mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 14,205
- 19,142
Watanzania wenzangu, nawasalimu katika jina lipitalo majina yote Jina la Yesu.
Chini ya rais wetu Magufuli tuliianza Vita dhidi ya Corona vizuri Sana kwa kumtanguliza Mungu. Tulielekezwa kutubu na kuomba rehema za Mungu ili aliponye Taifa letu dhidi ya janga la corona. Tuliomba kwa kufunga siku tatu na Mungu alijibu kwa kutuponya!
Hatukushuhudia vifo vya halaiki na waliokuwa wamelazwa walipona na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Vyuo na shule zilifunguliwa kwa haraka kuliko duniani kote na hazijafungwa tena na hazitafungwa tena. Tulielekezwa tena kufanya maombi ya shukrani ya siku tatu na tukamshukuru Mungu kwa kutuponya na corona. Hilo lilikuwa pigo kubwa Sana kwa ibilisi na mawakala wake. Lazima angetafuta namna nyingine ya kutushambulia tena! Tusiyumbe! tuendelee kukiri uponyaji wa Mungu kwa Taifa letu!
Hizi dalili tunazoziona Sasa zimelenga kutupa mashaka juu ya uponyaji wa Mungu kwetu, tuzikatae na tuendelee kumwomba Mungu na kumshukuru kwa uponyaji wake na corona itatukimbia! Tusifanye makosa ya kuyumba na kutilia mashaka uponyaji wa Mungu aliotufanyia.
Viongozi wa kiroho simameni imara katika hili. Watanzania wote tuendelee kumwombea Rais wetu Magufuli asimame imara Katika Imani ya uponyaji wa Mungu kwa Taifa letu. Aendelee kukiri hivyo, na itaendelea kuwa hivyo! Haya makelele yanayosikika Sasa punde yatatoweka na dunia itashangaa!! Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso!
Corona imeshindwa na haina namna nyingine zaidi ya kukimbia! Tusiruhusu hofu na woga. Kwa kufanya hivyo shetani hataweza kutupokonya ushindi wetu.