Tusipoteze dira kwenye janga la Corona: Tulianza na Mungu, tuendelee na Mungu

Tusipoteze dira kwenye janga la Corona: Tulianza na Mungu, tuendelee na Mungu

Hakika Rais Magufuli songa mbele! Usiwaogope kina Sanbalat, Thobia, Washidodi nk
Mungu hajawahi kushindwa. Hakika Mungu atajitwalia utukufu na hata sasa ametenda! Kama sio rehema zake wangalitumeza hai! Hakika Mungu hataitia Tanzania mikononi mwa watesi wa ndani na nje. Amen
Msilitaje bure jina la Mungu. Wewe unaamini ndani ya Serikali ya awamu hii na Bunge la awamu hii, kuna mcha Mungu? Ule ushetani uliofanyika wakati wa uchaguzi, mpaka mauaji, unaweza kufanywa na mu anayelitii neno la Mungu?

Msifanye dhihaka kwa mkuu wa nchi na mbingu. Ni aheri kutubu kuliko kulitumia jina lake katika kuuficha uovu wenu.

Hata yanayotokea haya yaweza kuwa ni sehemu ya laana. DHULUMA, MAUAJI, ULAGHAI NA HADAA, HUZAA LAANA.
 
Watanzania wenzangu, nawasalimu katika jina lipitalo majina yote Jina la Yesu.

Chini ya rais wetu Magufuli tuliianza Vita dhidi ya Corona vizuri Sana kwa kumtanguliza Mungu. Tulielekezwa kutubu na kuomba rehema za Mungu ili aliponye Taifa letu dhidi ya janga la corona. Tuliomba kwa kufunga siku tatu na Mungu alijibu kwa kutuponya!

Hatukushuhudia vifo vya halaiki na waliokuwa wamelazwa walipona na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Vyuo na shule zilifunguliwa kwa haraka kuliko duniani kote na hazijafungwa tena na hazitafungwa tena. Tulielekezwa tena kufanya maombi ya shukrani ya siku tatu na tukamshukuru Mungu kwa kutuponya na corona. Hilo lilikuwa pigo kubwa Sana kwa ibilisi na mawakala wake. Lazima angetafuta namna nyingine ya kutushambulia tena! Tusiyumbe! tuendelee kukiri uponyaji wa Mungu kwa Taifa letu!

Hizi dalili tunazoziona Sasa zimelenga kutupa mashaka juu ya uponyaji wa Mungu kwetu, tuzikatae na tuendelee kumwomba Mungu na kumshukuru kwa uponyaji wake na corona itatukimbia! Tusifanye makosa ya kuyumba na kutilia mashaka uponyaji wa Mungu aliotufanyia.

Viongozi wa kiroho simameni imara katika hili. Watanzania wote tuendelee kumwombea Rais wetu Magufuli asimame imara Katika Imani ya uponyaji wa Mungu kwa Taifa letu. Aendelee kukiri hivyo, na itaendelea kuwa hivyo! Haya makelele yanayosikika Sasa punde yatatoweka na dunia itashangaa!! Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso!

Corona imeshindwa na haina namna nyingine zaidi ya kukimbia! Tusiruhusu hofu na woga. Kwa kufanya hivyo shetani hataweza kutupokonya ushindi wetu.
Usitupoteze.
Hata Yesu alikuwa ana sali na kuusia mambo ya kufanya. Na akiona mambo hayaendi alikuwa ana litenga na kusali peke yake.
Hata Musaa alikuwa akisali na kushauriana na wana wa Israel. Sio nuie mna tuzuga hapa.
 
Tumeshaomba Rehema kwaajili ya taifa letu kwaajili ya makosa na uovu, uzuri Mungu akisamehe anasahau wewe endelea kushikilia tuu kwanza una uhakika wapinzani waliuliwa? Mungu wa Rehema atatuvusha salama

Nina uhakika kuwa wapinzani waliuliwa, unauliza au unapigia jibu mstari? Kwakuwa vyombo vya habari vimezimbwa mdomo ndio unadhani ukweli huo haufahamiki ama? Nasema hivi, corona piga chini hao wauaji na wezi wa kura, na kwenye hilo tutaiunga mkono corona fullstop.
 
Watumishi wa Mungu na watanzania wote kwa ujumla tuendelee kuliombea Taifa letu kwa mzigo mkubwa!! Hizi ni nyakati mbaya!! Shetani na watumishi wake wanaisagia meno nchi yetu!! Wanalenga kufuta utukufu ambao Mungu wetu ameupata kwa kuliponya Taifa letu na corona!! Wanataka kuiaminisha dunia kuwa Mungu hajaweza kuisaidia Tanzania, japo macho ya kila mmoja yameshuhudia uponyaji mkuu wa Mungu kwa Taifa letu dhidi ya Corona!!
Tumwombee Sana Rais wetu Mungu amtie nguvu, asiyumbe katika kumwamini na kumtumaini Mungu.
 
Usiturudishe nyuma Wewe!!!! Hatuwezi Kuendelea Kumjaribu Mungu kwa Maombi tu Bila Kuchukua Tahadhali. Njia za Kisayansi/Taalumu za kitibabu na preventive measures ndio suluhisho ya Changamoto iliyopo. Itafikia muda tusiwaamini Tuliowapa dhamana ya kutulinda sisi na Mali zetu. Tusiwe Wajinga Maana Maarifa yanatoka kwa Mungu na tusipoyafuata TUTAANGAMIA.

Take care my friend...b'se your safety begins with you. Wote Tunakumbuka historia ya Vita ya "MAJIMAJI"..Tusiwe wajinga maana tutapukutika kama Babuzetu waliodhani live ammo toka kwenye short gun zingeweza Kugeuka kuwa Maji .. Jibu Unalo kama maji yaligeuza lisasi kuwa Umande.....
Twambie hizo njia zimesaidia taifa gan

Sent from my SM-T355Y using JamiiForums mobile app
 
“Mwamini Mungu, lakini mfunge vizuri Ngamia wako”-Mtume Muhammad SAW.

Mungu huwa halipi maombi bali hulipa jitihada!Kupiga maombi wakati hakuna mipango pamoja na vitendo(Actions) madhubuti vya kupambana na Corona ni kumkejeli Mungu.
 
Mungu hawamtaki tena. Utaishia kutukanwa ukifanikiwa sana Uzi utafungwa kama wangu Leo Asubuhi
Hahaha hawajui Mungu ndo kila kitu? Wambie wamuulize Mussa pale Bahari ya shamu ilivyogawanyika kwa maombi tu wana wa israel wakapita nchi kavu hapo hapo ( A road in the sea) .
 
KASIMAME KATIKATI YA RELI UMUOMBE MUNGU WAKO TRENI
ISKUGONGE...
Hilo haliwezekani ni kukosa maarifa na kumujaribu Mungu. Ukifanya hivyo utakuwa huna maarifa ni kama kuywa sumu kwamba Mungu atanilinda. Wewe usijiletee baya lakini baya likitoka kwa mtu mwingine Mungu atakuepusha.
 
Back
Top Bottom