Niwakumbushe: Kumwamini Mungu kwa uponyaji ni hiari ya mtu! Lakini matokeo ya kuamini au kutokuamini hayaepukik!! Wana wa Israel walipokuwa wanatoka Misri kwenda Kanani ilifika mahali wakamnung'unikia Mungu na Musa kiongozi wao. Mungu alikasirika na kuwatumia nyoka wa Moto wawaue Jangwani.
Wote waliokuwa wameumwa na nyoka hatima yao ulikuwa Ni kufa. Musa aliwaombea rehema kwa Mungu na Mungu aliwaonea rehema. Mungu alimwagiza Musa kutengeneza nyoka wa shaba na amtundike kwenye mti. Musa akawaambia Wana wa Israel kuwa yeyote aliyekuwa ameumwa na nyoka inabidi ainue macho na kumtazama Yule nyoka wa shaba. Yeyote ambaye angefanya hivyo angepona hata kama alikuwa ameumwa na nyoka.
Wako wengi waliomtazama Yule nyoka wa shaba na wakapona. Lakini pia wako ambao hawakuona uhusiano Kati ya kumtazama Yule nyoka wa shaba na kupona kwao, waliona Kama vile Musa anawadhihaki! Walikataa kumtazama Yule nyoka wa shaba na walikufa! Kumtazama nyoka wa shaba ilikua Ni hiari, lakini kufa Kama matokeo ya kukataa kumtazama nyoka wa shaba baada ya kuumwa na nyoka haikwa hiari.
Hali kadhalika kumwamini Mungu kuwa ametuponya na corona Ni hiari ya mtu! Lakini matokeo ya kuukataa uponyaji huu si hiari kuyapata. Uchaguzi Ni wa binafsi!
Inashangaza sana kuona mtu anaona ni vigumu kumwamini Mungu aliyeumba mbingu na nchi lakini anaona ni rahisi kumwamini mtu mwezake asiye na uwezo wa kuumba hata sehemu ndogo tu ya mguu wa sisimizi, eti anaitwa mwanasayansi!
Nawaheshimu wanasayansi lakini namuheshimu Mungu zaidi ya wanasayansi! Neno la Mungu halibadiliki lakini neno la wanasayansi linaweza kubadilika wakati wowote!
Mungu ametuponya watanzania na corona, anayeamini hivyo, imekuwa hivyo, asiyeamini atabaki na corona yake na Kama hana corona itamfuata maana ameipa nafasi!! Huo ndio ukweli!!! Kupanga Ni kuchagua, kupanga kumwamini Mungu ni kuchagua uzima, kinyume chake Ni kuchagua maiti!
We