Tusipoteze dira kwenye janga la Corona: Tulianza na Mungu, tuendelee na Mungu

Mnaoamini Mungu kwanza hata kukubaliana Mungu wa kweli ni yupi mmeshindwa.

Unavyoanza tu kwa "nawasalimu katika jina lipitayo majina yote Jina la yesu" hapo ushawatenga wote wasio Wakristo.

Hebu jipangeni sawa kwanza mkubaliane Mungu wa kweli ni yupi, halafu ndiyo mrudi hapa kujadili habari zake.
 
Kumuomba mungu pekee bila kuchukua tahadhari ni sawa na mwanafunzi wa f4/f6 anayejibidisha kusali pekee(analala kanisani/msikitini) bila kupiga msuli akitarajia kufaulu NECTA..., (TUCHUKUE TAHADHARI+KUSALI/SWALI)
 
Kwahy Tanzania ni taifa teule badala Israel siyo?
Ila kweli, maana anayetazamiwa kuongoza malaika yupo nchi hii.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Huo utukufu atakaojitwalia utakuwa lini? Tusimsingizie Mungu, alitupa "dirisha " la kukabili adui wakati ule ili tuwe salama. Tuombe ili avifute kabisa virusi hivi toka uso wa dunia ila kama vipo tu itakuwa tabu. Tena tukikataa kabisa chanjo ya aina yeyote hicho kirusi ndiyo kitafyeka watu wengi maana hata ukijifungia ndani kitakufuata huko huko. Wakati wa misiba siyo muda wa kumwagiana sifa bali kushauriana namna ya kumkabili adui.
 
It's really real, when I feel the way that I do right now
I see all my brothers underground
Pushing up daisies, man, it amazes me
That you can't see where you gonna be
A statistic, everybody's gon' call ballistic
If you had a good day, damn, I must have missed it

NonChalant 5' O Clock in the Morning.....​
 
Mna mtest Mungu eee; ngoja mpukutike kama majani.
 

Atoe pesa zilizotolewa na wazungu kupambana na Corona zinunue vifaa tiba, msimtaje Mungu kujifanya ni wacha Mungu wakati mliagiza wapinzani wauwawe ili mkae madarakani kwa shuruti. Hamna ucha Mungu wowote, vinginevyo watu wasingekuwa wanateswa na kunyanyaswa kwenye shughuli zao za kuwaingizia kipato. Maibilisi mnamtaja Mungu ili kuhadaa wananchi wakati ni wauaji wakubwa. Corona piga chini hawa washirikina wenye ulevi wa madaraka.
 
Huu ni mtego wa kiroho Ila tumeshajua, Mungu aliyetuokoa wakati uke yupo hai atatuokoa tena, imeandikwa kila amwangaliay yeye ataokolewa, itakua hivyo kwa wote wanaomtegemea Mungu

Huyo Mungu wakati mnaua wapinzani ili muendelee kukaa madarakani hamkumuona? Mungu umbua hawa washirikina na wauaji kwa kuwatanguliza kaburini mmoja baada ya mwingine.
 
Nenda kasome kisa cha Nabii Ayoub
 
Ilitokea tauni, hatukuacha chanjo wala tiba

Ilikuja ndui, hatukuacha chanjo wala tiba

Kilikuja kipindupindu, hatukuacha usafi wala tiba

Kifua kikuu, hatujaacha chanjo wala tiba

Malaria, hatujaacha kutumia net wala dawa

Siku zote kwa magonjwa yote watu wamepata chanjo na tiba au tiba pekee bila chanjo, lakini hawakuacha kusali maana sala ni maisha ya muumini yeyote.

Sasa huu uwendawazimu wa kusema corona haihitaji kufuata taratibu za kisayansi za kujikinga/chanjo/ tiba lazima ni fikra za kishetani, na wanaolipigania hili ni mawakala wa shetani wasio na chembe ya Roho wa Mungu.

Wenye Roho wa Mungu wanajua kuwa matabibu yamekuwepo nyakati zote, na Mungu amegawa karama na maarifa ili tushiriki katika neema zake ikiwemo neema ya uponyaji.

Mungu humshirikisha mwanadamu katika uumbaji. Huwezi kuacha kuoa au ukioa ukaacha kujamihiana na mkeo, ukabaki katika maombi halafu siku moja ushtukie una mtoto.

Mungu anatushirikisha katika kuwakuza watoto. Huwezi kuacha kumlisha mwanao ukabakia katika maombi halafu utegemee awe na afya njema na akue.

Mungu hutushirikisha katika uponyaji. Huwezi kuugua ugonjwa wowote, hutaki tiba halafu utarajie uponyaji.

Mungu ametuumba, ametujalia karama mbalimbali ili tushiriki katika kazi zake. Na anataka tumwone yeye katika hizi karama anazozitoa.

Tusiwe wajinga, tusiwe wapumbavu, tusimjaribu Mungu wetu mwenye ukuu na hekima isiyopimika, bali tufanye kazi usiku na mchana kuyalinda maisha yetu, na tunapofanya hivyo tumwombe atuangazie ili tufuate njia ziizo sahihi, na azibariki jitihada tunazozifanya ili zilete uponyaji. Mwanasayansi mkuu ni Mungu, lazima tutumie utashi aliotupa kuyamudu maisha yetu ikiwa ni pamoja na kupambana na yanayotuzunguka.

Anayesema tusifanye kitu zaidi ya kusali, ni shetani, ni ibilisi, ni mjinga na mpumbavu mkubwa. Mungu anawachukia wajinga, anawachukia wapumbavu. Mungu wetu hujivunia watu werevu wanaolijua neno lake katika kweli na siyo katika upotofu. Tusipokuwa werevu, tutayakosa maisha ya Duniani, na mbingu hatutaipata maana upumbavu siyo sehemu ya utakatifu. Baada ya kifo cha mwii tutakumbana tena na hukumu ya Mungu kwa sababu tuliukumbatia upumbavu.
 
Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma hashughuliki na watu waliochagua kuishi kipumbavu kwa kupuuza matumizi ya akili alizowajalia bila malipo.
 
Silaha kubwa ya maangamizi shetani anayoitumia ni hofu. Hofu ni zaidi ya kifo, ushauri mzuri huu. Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿.
 
Una uhakika chanjo hazijawasaidia?

Israel mortality rate down by 94%

Uk mortality down by - 28 cases per day

US mortality rate down by 26%

Kwa nini unasema hazijawasaidia? Au umekariri?
 
Acha uwongo. Tanzania kutokana na umaskini wake, hawajawahi kununua chanjo yoyote. Kama ni biashara wanafanyiana wenyewe kwa wenyewe, kati ya makampuni na serikali zao.
 
Nyinyi ndio mnam
 
Nyinyi ndio mnampoteza Rais
 
Imani bila matendo imekufa. Nina uhakika kuwa hatujabarikiwa kivile kuliko nchi zingine Kama Israel.Sisi tuna ujinga mwingi zaidi ya nchi zingine.
 
Tunapaswa tuheshimu maelekezo ya viongozi wetu.
His honour Polepole alisema
"Tumekubaliana corona Tanzania iishi kwa heshima au iondoke"
Na yule mwanasayansi mchawi mwenye phd bila thesis alisema ameishinda corona kwa maombi..
Ila Tanzania jamani tuna MAPIMBI haswa..
Mapimbi ya kutupa !
 
Una uhakika chanjo hazijawasaidia?

Israel mortality rate down by 94%

Uk mortality down by - 28 cases per day

US mortality rate down by 26%

Kwa nini unasema hazijawasaidia? Au umekariri?
hawa ndio wale hawafiatalii statistics za hii kitu daily. halaf wanakuja na assumption za kujilinganisha na wenzetu wanaochukua hatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…