Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Tusipotoshane, ajira ina nafuu na uhakika zaidi kuliko kujiajiri

Ukitaka kujua Mambo kwa ground Ni tofauti huyo muuza chips Mpe Option mbili
1 - Mwambie Kuna kazi ya kulipwa mil moja kwa mwezi je Yuko tyari au
2 - aedelee kuuza chips

Uone atachagua kwenda wapi
....mind you ukilipwa mshahara wa mil moja kwa mwezi uwe unajua Apo Kati Kati Kuna hela nyingine ya sintofaham utaifaid Sana tu
Hiyo hela ya sintofaham ndio chanzo cha maendeleo duni ya taifa letu.
Kwani waziri, mkuu wa mkoa, mkurugenzi, rais, diwani nk,,, wangeridhika na mishahara yao serikali ingekuwa na baki kubwa ya fedha za maendeleo.
Raia wakimwona waziri kastaafu wa kawaida wanamsema kuwa hana akili lakini yule aliyetufisadi wakiona mijengo yake wanamsifia kuwa ana akili sana. -
Mawaziri ,wakuu wa mikoa kwa kuogopa fedhea kuonekana hawana akili huona ni angalau watufisadi kidogo ili mtaani aonekane ana akili.
Hili mwishoe imekuwa kasumba, bila kufisadi wewe hauna akili.

Ndipo sasa vihela vya sintofahamu vinapotafutwa.

 
Mawazo yako yanaweza kuonekana finyu kwa mtu ambaye ameshaingia kwenye biashara na kufanikiwa pakubwa.

Ni ngumu sana kumshawishi mtoto wa Bhakressa ambaye amekulia kwenye mazingira ya biashara na kuona hizi 500M-1B figures kama mauzo ya kila siku
Tatizo watu wengi wanajua biashara ni kuuza duka, yaani wanaiponda biashara kwa sababu kwanza hawaelewi biashara ni nini.
 
Daah wabarbaig bwana... Yani tangu kuzaliwa kwako Hadi miaka 60..unategemea kupata million 90 au 100 Kama kiinua mgongo...Yani inakua ndoto za maisha yako Ni kuwa na millioni 90 au 100 kutoka kuzaliwa Hadi kuzeeka[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...biashara ngumu lakini utatoka damu miaka 5-10..lakini growth yake iko sexy
Yaani kwangu kuajiriwa ni kipengele cha bahati nasibu. Napata nusu milioni kwa mwezi na mtaji ni laki mbili. Bado ninafanya mapumziko kwa muda na siku nitakazo leo eti nisubiri mpaka barua ya likizo ikubaliwe.[emoji3064] Sipingi kuajiriwa lakini ujasiriamali kwangu ni habari ya mjini. Hata wanangu nawajengea mazingira ya kujiajiri japo wanapata elimu kwa ajili ya TAALUMA.
 
Kiukweli ajira ni nzuri koz unapoanza tu ni kama umeanza na faida na hauna hasara yaan kama ww hupendi kusumbua kichwa chako ajira ni nzuri na kwa nature ya watanzania na Afrika kwa ujumla kama ajira zingekuwepo nje nje tungechagua kuajiriwa kuliko kujiajiri, Kujiajiri kwa mwanzo ni utumwa sana unaweza kukosa muda wa kulala na muda wakuwa na familia ila ikifika pointi nzuri hase ni jambo njema sana, Kama utachambua vizuri mwisho wa siku bado kujiajiri ni njia nzuri kuliko kuajiriwa, Kuajiriwa tunapenda lakin ukweli usemwe tu kuajiriwa ni utumwa mno
 
Kujiajiri sio kuuza duka tu.
Ajira ni nzuri lakini zipo chache. Asilimia kubwa ya waliojiajiri wangepata ajira wasingehangaika.
Mfanyakazi hata siku moja hawezi kuwa tajiri, labda awe anaiba mali za umma au kufanya udanganyifu wa fedha. Lengo hasa la kuajiriwa ni ili utumikushwe kwa ujira fulani kila mwezi unaokufanya ujikimu ili uendelee kutumikishwa wakati ukiwa na nguvu. Ukizeeka hawskutaki tena kwa sababu unageuka mzigo badala ya kuwa asset,so wanakulipa sehemu ya ujira wako ambayo walikuwa wanakukata kipindi chote cha ajira na pesa hiyo hiyo inakuwa mafao yako. Ndiyo maana duniani kuna watu binafsi wana hela kuliko serikali za baadhi ya nchi, imagine tajiri namba moja duniani anamiliki dola bilioni 350!!!
 
Mleta mada nitajie tajiri yeyote mkubwa nchini au duniani kote alietajirika kupitia mshahara
Mkuu huko duniani ni mbali, hapa hapa Bongo kati ya matajiri 100 kuna hata mmoja ambaye ameajiriwa labda benki kuu, TRA etc??
 
Kuna jamaa kaajiriwa anakunja kama 1.5m kwa mwezi ila kafungua kajenda frem kwake na amefungua duka ambalo kamuweka wife wake kwa siku hakosi 50 amekosa sana 35. Maisha yamebadilika tofauti na mwanzo ili ikifika tarehe 15 anakua na hali mbaya anaishia kukopa kopa hadi nafaka
 
Turudi kwajojo kipindi amejiajiri je alijiajiri kwa kupenda?? Na baada ya kuajiriwa vs kabla hajaajiriwa ni kipindi kipi Jojo anafuraha na kupendeza zaidi? Ajira tamu nyieeee.
Sasa hivi ana furaha sana weweee, ila siyo sababu ya ajira ni kwa sababu ya yaleee mambo yenu ya suukariiii...
 
utakapojaaliwa ndio hapo hapo komaa...

Japo kujiajiri kama mambo yanakuendea vizuri ni vizuri zaidi, turbo zikifunguka zimefunguka..

Mlio kwenye ajira, jitahidini kuwekeza kwenye non -risk businesses mkiwa angali mko kwenye ajira kuongeza kipato na kupata uzoefu... Mlioajiliwa na mna wake wanaojielewa ni vyema mkawekeza kwa wake zenu, mke anakuwa hata na kabiashara kakuleta hela ya kula nyumbani na kununua hata chupi zake...nk...
 
kujiajiri mziki upo kwenye kuanza then ukasimama....waliozoea kujiajiri kwao wengi sio tatizo balaa ni wale waliozoea kuajiriwa halafu wakaja kujiajiri....kumantain yale matumizi ndio mziki...

Mtu alikuwa ana matumizi ya 2mil kwa mwezi anarudi mtaani kugenerate hiyo 2mil kwa ajili ya matumizi then uweke na akiba ni balaa... unakuta 2mil ni matumizi ya lazima kabisa kama kula, umeme, maji nk....hapo usave kwa ajili ya ada za watoto nk..
 
Kwahio unafikiri waliojiajiri wengi wamejiajiri kwasababu ya kukosa ajira?! 3m profit per month nayo hela? Pita kariakoo Tafuta unao wajua wakwambie mshiko unaotembea kwenye biashara. Tatizo mnaposema biashara mnaanza kuzungumzia maduka ya Mangi mtaani.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
cc: jokate, nikiwapili

SIZITAKI MBICHI HIZI [emoji23] [emoji23]

Mtu anaamka kila siku miaka nenda rudi anafungua duka alafajiri mpaka usiku na faida yenyewe haizidi hata elf 30 kwa siku, Ni wapi anapata confidence ya kusema ajira ni utumwa kwa mwenzake anaeiingiza milioni 2 kila mwezi, siku 150 za kupumzika kila mwaka, akiumwa bado anapata mshahara, anaingia kazini saa 2 anatoka saa 11 jioni, kuna posho, n.k, Ni wapi anatoa hii confidence.

Kuponda ajira ni utumwa ni sawa na "sizitaki mbichi hizi", yaani ni kwa vile bongo ajira hazipo nyingi, nimeshushudia ajira zikitangazwa hata hao waliojiajiri wanazi shambulia sio mchezo, na hapo akipata ajira hata biashara yake ya zamani anaweza kuipiga chini
Kuna vijana wengi tu wana miaka 28 wameajiriwa wanakunja mshahara zaidi ya milioni 2 kila mwezi, jiulize je ni vijana wangapi wa huo umri waliojiajiri wanakunja faida zaidi ya milioni 2 kila mwezi??

Jiulize kwanini hata wazazi wengi wanaofanya biashara wanapeleka watoto kusoma na kuwaambia wasome ili wapate ajira?? kwanini wasiwaambie wasome ili wafanye biashara ?? hapa sizungumzii wafanya biashara wakubwa kama kina bakhresa, nazungumzia wafanya biashara kwa mfano wenye maduka ambayo faida kwa siku unakuta ni chini ya elf 20.

Biashara ni nzuri ikiwa kuna system ya kupigana jeki na kubebana, hapa bila kificho tunajionea kwa waarabu, wahindi, wakinga, wapemba na wachaga, hawa huwa wana mitandao yao ya vikundi vya kubebana, wanajenga system za kusaidiana, wanachangiana, mzazi akifa kuna mtoto kaandaliwa tayari , n.k unakuta mtu akitaka kusafirisha mzigo kuna mtu wao ana kampuni ya kusafirisha, akitaka mtaji kuna mtu wao anaweza kumsaidia, akianguka basi wenzake watamsaidia. Sasa jchanganye kuwaiga [emoji23] [emoji23] !!! unapambana kivyako vyako, fursa unazitafuta kivyako vyako na ukianguka unaanguka puuuh kivyako vyako!!
Hapa wanazungumziwa wanaolipwa 2M,tunaolipwa 300,000 to 500,000 tunacomment wanpi?
 
Hiyo hela ya sintofaham ndio chanzo cha maendeleo duni ya taifa letu.
Kwani waziri, mkuu wa mkoa, mkurugenzi, rais, diwani nk,,, wangeridhika na mishahara yao serikali ingekuwa na baki kubwa ya fedha za maendeleo.
Raia wakimwona waziri kastaafu wa kawaida wanamsema kuwa hana akili lakini yule aliyetufisadi wakiona mijengo yake wanamsifia kuwa ana akili sana. -
Mawaziri ,wakuu wa mikoa kwa kuogopa fedhea kuonekana hawana akili huona ni angalau watufisadi kidogo ili mtaani aonekane ana akili.
Hili mwishoe imekuwa kasumba, bila kufisadi wewe hauna akili.

Ndipo sasa vihela vya sintofahamu vinapotafutwa.

View attachment 2007404
Imekua tamaduni hyo Kaka hamna namna
 
Back
Top Bottom