Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

"English Is Like,,A Water",Mama yangu Mkwe Kipenzi
 
Unapotosha bibi
Hakuna lugha bora kuliko zingine duniani, hakuna!

Sifa ya lugha ni kujitosheleza yenyewe, na kuwezesha watumiaji kuwasiliana.

English kwa sasa ni International language na haikwepeki acha watu waishobokee tu

Mfano wewe umeishi Canada kama sikosei kwa muda mrefu na kufanya kazi na huko lugha kuu ni English..!

Sasa umestaafu ndio unaanza kuona kiswahili ndio dili, huna cha kupoteza. Bibi
 
Cha maana ni communication / mawasiliano, kwahio kama hivyo ndivyo basi ni bora kujua lugha ambayo waliokuzunguka wengi wanaizungumza, baada ya hapo unaangalia ni lugha zipi zinazungumzwa zaidi na katika top five ni zifuatazo: (Na ukishaangalia hio orodha sijui utasema nini kupinga watu wasijue lugha inayozungumzwa zaidi duniani..., kuhusu kushobokea nadhani hio ni argument nyingine)


RankLanguage# of Speakers (2023)
1English1,500,000,000
2Mandarin1,100,000,000
3Hindi609,500,000
4Spanish559,100,000
5French309,800,000
 

Kingereza hakijitoshelezi.

Usijidanganye.

Kjswahili ni kizuri na kinajitosheleza zaidi ya Kingereza, hatujielewi tu.
 
Kingereza hakijitoshelezi.

Usijidanganye.

Kjswahili ni kizuri na kinajitosheleza zaidi ya Kingereza, hatujielewi tu.
Kiswahili hakijitoshelezi..

Misamiati ya hovyo sana na inakuja na kuondoka tena watu wa BAKITA wanajitungia tu hapo ofisini.

Wakati Misamiati ya lugha yoyote inaibuka kutokana na shughuli za binadamu mfano kilimo nk
 
Hizo takwimu haziifanyi lugha kuwa tamu na nzuri.

Kingereza kililazimishwa kwenye makoloni yake ndiyo maana kinatumika sana, siyo kwa kuwa ni bora sana.
 
Koma, sina ukwe na wewe.
Kiislam hatuna I utani wa kijinga. Hunijuwi sikujuwi.
Punguza Jazba Mama Mkwe,,,kiislamu haipendezi Kumtusi Mkwe Wako,,,Tuzungumze kiistarabu Tu,,Naamini Kwa kuwa u Ustahadhati Safi wa Mifupa,,Damu na Nyama.....Roho,,Mwili na Nafsi hatutashindwa elewana,,Amiin!!
 
Hakika.....Yasemekana Kiingereza ni Kilatini/Kirumi kilichovurugwavurugwa...!
 
Utaingiaje mtandaoni Kama hujui hata Cha kunywea maji?
 
Hizo takwimu haziifanyi lugha kuwa tamu na nzuri.

Kingereza kililazimishwa kwenye makoloni yake ndiyo maana kinatumika sana, siyo kwa kuwa ni bora sana.
Kumbe unaongelea Utamu na Uzuri ? Mimi naongelea umuhimu wa lugha ambao ni mawasiliano hivyo kuweza kuwasiliana inabidi wote tuongee lugha moja (unaweza ukasema Kifaransa, Kijerumani, Kihispania, Kirusi au hata kiItaliano au Kiarabu) ni kizuri zaidi ila kama unakizungumza peke yako nadhani utakuwa una defeat the purpose)
 
Kingereza hakijitoshelezi.
Katika mizania ipi?
Usijidanganye.

Kjswahili ni kizuri na kinajitosheleza zaidi ya Kingereza, hatujielewi tu.
Hebu taja neno la kiswahili linaloanzia na herufi "X" au "Q" .

Pia wewe ndio unawapotosha vijana sasa , mimi wakati nafika ng'ambo miaka hiyo nilifanya mtihani wa ufahamu [English proficiency test], kama wewe hukufanya huo mtihani ni vyema ukawashauri vijana wajinoe vilivyo katika lugha ya kiingereza kwa fursa nyingi za maana ziko huko kwenye mataifa yanaongea kiingereza kama lugha ya kwanza iwe ni wanaoenda kusoma , kufanya kazi na kadhalika.

Huko kujisifiu tu eti bora kujua kiswahili ndio inatugharimu ni rahisi kukutana na wakenya au waganda wengi katika sehemu tofauti nilizotembelea kuliko watanzania.

Hapo sijaongelea mada ya ugumu wa kujaribu kutoka na kujifungia kulikoletwa na ujamaa ambao ndio ulitudumaza kabisa.
 
Hizo herufi za kubuni tu hazina asili ya maandiko yoyote.

Mfano hili neno linaanza na Q "quarter". Unalitanmka kota. Uwe Muingereza au mndengereko. Kwanini lisiwe kota tu hata kwa Kingereza?

Neno lenye x "sox" unalitamka "soks". Hizo herufi ulizoweka zote ni wao kujifanya kuwa wana ubora zaidi kwa kujitofautisha, hazina maana yoyote.

Elewa kuwa, bila "Alif Be Te" usingekuwa na alphabet.

Unafahamu "alif be te" zinapatikana wapi?
 
Katika lugha ya kiingereza maneno asilia ya kiingereza ni asilimia 24% tu, mengineyo yote yameazimwa kutoka kwenye Kigiriki, kilatini, kifaransa na Kijerumani ambayo ni mataifa yaliyowahi kutawala visiwa vya Uingereza.​
 
Kingereza hakijitoshelezi.

Usijidanganye.

Kjswahili ni kizuri na kinajitosheleza zaidi ya Kingereza, hatujielewi tu.
mara kadhaa tumesikia kuwa kiswahili kina misamiati michache, hili hudhihirika hata wataalamu na viongozi wetu mbalimbali wakiwa wanaongea kuna vitu fasta wanatamka kwa kutumia english, unavosema kinajitosheleza unamaanishaje hasa?

NB:uzi nimesoma mara mbili lakini sijaelewa lengo la kupendekeza kiswahili kifundishwe kwa herufi za kiarabu ni lipi?
 
Ndugu we ni mtaalam sana wa lugha uko vizuri chapisho lako hili litakupa PhD tukuka kwa utafiti wako wa chuki na kibaguzi. Kama mtaalam em nimbie lugha yako hiyo nzuri ya kiarabu kwa nini inapenda kutumika na walozi kuandika kwenye nazi na mayai viza yanayotupwa njia panda na siyo lugha ya kiingereza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…