Manabii /Mitume au viongozi hupangwa/Huletwa na Mwenyezi Mungu.Kama hukupangwa na Mwenyezi Mungu kuwa kiongozi , hata Kama una dhimira ya kuwa Rais/ kiongozi, utagombea Urais miaka nenda rudi na usipate.Kufikiria au kuomba/kugombea nafasi fulani haimaanishi kuwa wewe ndiyo unafaa au unauwezo sana. Kufaa au uwezo wako,wanaweza kuuona watu wengine ambao wamekuona katika utendaji wako au uongozi wako.Wakavutiwa na utendaji wako au staili yako ya uongozi , wakakuchagua au wakakupendekeza kwenye mamlaka za uteuzi uwe kiongozi wao. Viongozi wa aina hii wanakuwa wazuri sana kuliko wale wenye uchu wa madaraka/wanaotia nia,wakaweka matangazo kwenye kuta/madaraka ya barabara zote nchini Tanzania, kuunda kamati za kampeni na kulipa posho kwa wajumbe wa kampeni na wengine ili wapitishe jina lake kwenye mikutano mikuu ya uchaguzi. viongozi wa aina hii wakipata uongozi,kitu Cha kwanza ni kufikiria jinsi ya kulipa fedhila kwa watu waliomfikisha hapo na kulipa madeni. Mama katika moja ya hotuba zake wakati anaongea na umoja wa wanawake Tanzania ,aliwahi kusema kuwa dhamira iliyomsukuma kuomba uwakilishi kwenye Baraza la wawakilishi Zanzibar 2000 kwenye Jimbo moja - Mkoa wa kusini unguja ilikuwa kwenda kuwatetea wapiga kura na kuibana serikali ya Mapinduzi Zanzibar ipeleke maendeleo jimboni kwake.Lakini, baada ya kuchaguliwa,kuwa Mjumbe wa Baraza la wawakilishi akajikuta amechaguliwa kuwa waziri na Rais wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume ,hii inadhihirisha kuwa mama ana Elimu na sifa za kuongoza,na toka wakati huo amekuwa akichaguliwa kuwa waziri katika Baraza la serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi tofauti . Hii ni uthibitisho kuwa mama ana sifa na uwezo wa kuongoza.Na siyo mtu mwenye tamaa na uchu wa madaraka.