Tusitetee uovu, Mbowe hayuko juu ya sheria. Kama ana makosa tuache sheria ifuate mkondo

Nini maana ya 'rule of law'?
 
Ukiona mwenzio ananyolewa tia maji zako kiwembe kinakuja
 
Huyohuyo kiongozi akisema tukimwagiza askari apige risasi tatu hiyo siyo askari.Huyo ana tofauti gani na kauli ya wembe
Kwa hiyo yeye anamiliki polisi, nyinyi mnamiliki wembe😀😀😀😀
Sasa mwenzenu anatumia silaha yake(polisi) kuwasulubu na ninyi mnasubiri nini kuanza kuitumia silaha yenu?
 
Kaa kimya, nakujua vizuri empty minded person. Usitafute kujifanya una akili timamu.
EeenHeee!

Eti "empty minded" unaelewa maana yake?

"akili timamu" na "empty minded" wapi na wapi? Hili nalo unataka tumtafute kilaza ni nani?
 
Ni uovu gani ako nao mbewe? acha ujinga dogo!
 
Hizi sheria hazitumiki fisiemu.....maana tunawaona na wao wakiitisha mikutano na hatujawahi kushuhudia wakienda kusachiwa kwenye makazi yao na baadaye kuletewa madai ya ugaidi. Hebu tupe connection ya kongamano la katiba mpya, kwenda kusachiwa nyumbani na baadaye kutuhumiwa ugaidi, labda mwenzetu upo jikoni...
 
Usisahau pia, wanasema polisi walikuwa wakimfuatilia nyendo zake, lakini hawakuwa tayari kwenda kumsachi, hadi alipotorokea kwenda kujificha kwenye kongamano Mwanza, ndipo wakamwona na kmdaka hapo hapo!
 
kwa hiyo yeye anamiliki polisi , nyinyi mnamiliki wembe😀😀😀😀
Sasa mwenzenu anatumia silaha yake(polisi) kuwasurubu na ninyi mnasubiri nini kuanza kuitumia silaha yenu?
Ni kama wewe ndiye refa wa hiyo vita, utaamua ni nani mshindi na katika wakati gani!
 
Wewe ni mgeni na mambo yanayotendeka nchi hii. Hata mtoto mdogo anajua kwamba amebambikiwa kesi. Kuitwa “gaidi” aisee hapana hata kidogo. Wangetafuta hata kosa lingine. Hii itawatesa sana polisi maana dunia nzima wanajua hilo.
 
Sheria ipi polisi wametumia kumteka hotelini saa nane usiku na kukaa naye siku mbili bila kuliambia taifa
Kosa la ugaidi ni kubwa sana, unakamatwa popote, muda wowote na wanaweza kukaa na wewe muda wowote bila kukupeleka mahakamani. Tena walimuhurumia, nchi nyingine kosa kama hilo order ya kukamatwa kwako inakuwa ni "Shoot to kill".
 
Mbowe alifanya movement yake ya CDM digital, aliguswa na mtu? Hadi akawasifia polisi na Samia. Alipoona hajaguswa na kukosa kiki ya kuonesha tz hamna uhuru na demokrasia akaamua aanzishe movement nyingine haraka haraka, na alilifanya hili akitafuta njia wakamatwe ili waitangaze tz vibaya, mtu kama Mbowe si wa kuchekea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…